je serikari yetu imekuwa ikiwajibika ipasavyo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

je serikari yetu imekuwa ikiwajibika ipasavyo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makene, Jul 19, 2011.

 1. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Inatia shaka kuona jinsi mambo yanavyokwenda katika serikari yetu,
  tunasikia habari za wizi wa fedha za serikari, hatuoni hatua za dhati zikichukuliwa tofauti na viini macho kufanyika.

  Tunasikia juu ya rushwa ambazo zinahatarisha uchumi wa taifa, lakini hatuoni kama uongozi wa juu unaonyesha kuchukua hatua madhubuti.

  Hata maamuzi ya serikari yamekuwa ya lelemama, kwa malengo ya kusaidia kuficha ukweli au kwa malengo ya kuwasafisha baadhi ya wanaotuhumiwa au kwa lengo la kutetea maslahi ya chama.

  Tumeshuhudia michango yenye tija ikipuuzwa na kubezwa kwa lengo la kutafuta ushindi wa chama bila kuzingatia maslahi ya taifa.
  Maneno ya kukejeli na kuzoofisha jitihada za kweli yamekuwa yakitolewa na wasemaji wa serikari, hata baadhi ya vyombo vya habari kutetea uozo kwa kuuficha au kuutetea.

  Hili la kukataliwa kwa budget ya wizara ya nishati na madini nalo ni kiini macho. PM kuingilia kati ni kwa maslahi ya kumuokoa waziri mwenye dhamana, ili aendelee na ulaji. Nina hakika iwapo budget hiyo ingetolewa wazo la kukataliwa na wapinzani, jambo hilo lingepingwa na wabunge wote wa ccm na puppet wao na spika angetumia mbinu ile ya kilevi ya sasa nitawahoji. Nina hakika budget hiyo ingepita.

  Sasa kama serikari ina uwezo wa kuingilia kati jambo ambalo ni la kwao kwa kuona kelele zimezidi, je si wakati muafaka kwa serikari hiyo kukili kutowajibika na kuchukua hatua madhubuti ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha baadhi ya watendaji wake ili kuliokoa taifa na aibu ya maamuzi mabovu ya mara kwa mara yanayofanywa na wabunge wakosoaji kisha wanaunga mkono.

  Hawa wabunge wetu wanatia aibu pale wanapopiga meza kila wakati kabla hata ya kujua hitimisho la msemaji, mfano mzuri ni pale wabunge wa ccm wanapoanza kuongea na kupewa ushabiki wa kugongewa meza kisha mwisho msemaji anaposema haungi mkono hoja wanabaki midomo wazi.

  Tunataka wabunge wanaowajibika kwa maslahi ya nchi na wananchi, na watendaji wa serikari wenye lengo la kukwamua hali duni za wananchi walio wengi.

  Tusubiri tuone!
   
Loading...