Je: Serikali za nchi za Afrika mashariki zinabana Uhuru wa habari, au Uhuru huo unatumiwa vibaya?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Swali hili limejadiliwa kwenye chombo cha habari cha kimataifa, idhaa ya kiswahili BBC, katika mjadala wa wiki.

Walikuwepo washiriki kutoka nchi za Africa, ambapo Kwa Tanzania alikuwepo mwenyekiti wa jukwaa la wahariri bwn. Makunga, na katibu wa CCM itikadi na uenezi, bwn. Humphrey Polepole. Kwa Uganda alikuwepo mwanahabari mkongwe bwn. Ally Mutassa, na washiriki kutoka nchi zilizosalia.

Mjadala ulikuwa wa moto, lakini ulikuwa unaboa sana kutokana na aina ya washiriki kutoka Tanzania. Ukweli bwn. Makunga hakuwa hur kuwatetea waandishi wa habari, na amekuwa akipata kigugumizi cha kutafuta nini azungumze pindi anaposhindwa kuusimamia ukweli, katika kujibu hoja nzito.

Sikumuelewa kaka yangu Polepole alishiriki katika mjadala ule kama nani, lakini Kwa urahisi naweza kusema kuwa alishiriki kama msemaji wa CCM, na pia mtetezi wa serikali ya Tanzania juu ya ukandamizaji wa Uhuru wa habari.

Ndugu Polepole ameonekana akijenga hoja za kimakusudi kabisa kujaribu kuuaminisha umma kwamba nchini Tanzania Uhuru wa habari ni Mkubwa wa kujitosheleza na mahusiano Baina ya serikali na vyombo vya habari ni mazuri.

Aliyeukataa unafiki ni mwanahabari kutoka Uganda, bwn. Ally Mutassa, ambaye amesema kwamba mgogori Baina ya serikali na waandishi wa habari huja pale vyombo vya habari vinapoandika masuala ambayo serikali haitaki kuyasikia, hususan migogoro ya ardhi, ufisadi, matumizi mabovu ya Mali ya umma na rasiilimali za nchi, n.k. ambapo ndugu yangu Polepole yeye alipoulizwa kuhusu mambo gani yanayoweza kuhesabiwa yanakiuka maadili ya uandishi au yanavuka mipaka, yeye alitolea mfano habari za mtu kuonekana mtupu (bila nguo), na kudanganya au kusema uwongo, lakini hakuzungumzia serikali kutokutaka kusikia habari za siasa za upinzani, migogoro ya ardhi, n.k.

Ndugu yangu polepole ninayemheshimu sana, alikwenda mbali akatoa tafriri isiyo sahihi Kwa kauli ya Rais Magufuli dhidi ya vyombo vya habari, kauli ambayo moja Kwa moja inakandamiza Uhuru wa habari, lakini ndugu Polepole akasema kwamba hakuna mmiliki wa tafriri, kwamba anaweza kutafsiri vyovyote, alimradi alinde maslahi ya chama chake na serikali yake.

Ally Mutassa alifafanua pia mgawanyiko wa kisiasa ambao unajengwa na serikali yenyewe Kwa kutokuvipa Uhuru vyombo vya habari vya umma kutoka taarifa zote za habari bila kujali habari kutoka upande UPI wa siasa, yaani mfano gazeti LA habari leo hakiwezi kuandika habari za upinzani au za kuikosoa serikali, hivyo kupelekea wananchi kununua magazeti ambayo yako huru kuandika hata habari ambazo haziifurahishi serikali lakini Kwa maslahi ya umma, mfano gazeti la Tanzania daima nchini Tanzania.

Je: sisi watanzania Kwa ujumka wetu ambao hatukupata fursa ya kushiriki mjadala huo, tuna maoni gani juu hili?

Naomba kurudia swali: Serikali za nchi za Afrika mashariki zinabana Uhuru wa habari, au Uhuru huo unatumiwa vibaya?

Wenu katika demokrasia na maendeleo
 
Demokrasia nini,?.Kwanini serikali za bara la afrika nyingi hazipendi kukosolewa?kwanini ben sita kapote,na tunda wa Lisa alipigwa risasi uko kijiji cha panya?jf naomba mawazo toka kwenu
 
demokrasia ni kufanya kazi kwa bidii na kutofuatilia maslahi ya nchi yetu, ukikiuka inakuhusu
 
Back
Top Bottom