DullyJr
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 13,993
- 11,878
Habari zenu wakuu?
Leo nimeamua kuja na swali ambalo kiukweli limekuwa likinitatiza ila kwa kuwa hapa tunakutana watu mbalimbali wenye upeo tofauti naweza kutoa sintofahamu iliyopo kichwani mwangu na kwa baadhi ya wadau........
SWALI: NI SERA IPI YA ELIMU INAYOTUMIKA NCHINI KWA SASA?
JE, NI HII ILIYOZINDULIWA NA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE MWAKA 2014 AU KUNA NYINGINE?
Nakumbuka katika mwaka 2014 serikali ilifanya mabadiliko ya Sera na kuja na Sera mpya ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 ,Sera hiyo ilikuja na miongozo,matamko na mikakati ya utekelezaji wake.
Sera hiyo ilikuja na vitu kama
KUTILIA MKAZO KKK
ELIMU YA AWALI KUWA NI YA LAZIMA
ELIMUMSINGI ambayo iliweka wazi mfumo wa elimu mpya utakaotumika kuwa ni kufanya darasa LA kwanza mpaka kidato cha nne kuwa ni lazima ambapo walipendekeza mfumo wa 1-10-2-3+ na kuachana na ule wa 2-7-4-2-3+ ambapo kigezo kikubwa kilichotumika ilikuwa in kupunguza muda wa mwanafunzi kukaa shuleni ili kupata graduate wenye umri mdogo ili walitumikie Taifa kwa muda mrefu..........
Sasa Sera hiyo INA mambo mengi sana ambayo tukiorodhesha hapa tutakesha ila kwa uchache wake ni hivyo.
Sintofahamu imekuja baada ya serikali iliyoingia madarakani kuja na mambo mapya ambayo ni tofauti kabisa na Sera hiyo katika utekelezaji wake kwa mfano,
KURUDISHWA KWA MFUMO WA ZAMANI WA ELIMU NCHINI wa 2+7+4+2+3+ ambao unarudisha moja kwa moja ufanywaji wa mitihani ya darasa LA saba.
Kurudisha usimamiwaji na uendeshwaji wa mafunzo ya ualimu NECTA badala ya NACTE
Kurudisha grade a na stashahada ya uailimu wa sekondari na kufuta ODPE na ODECE zilizoletwa na Sera mpya.Matokeo yake wamewaweka katika sintofahamu kubwa hawa wahitimu wa ODPE na ODECE ambao kiuhalisia ndio matakwa ya Sera hiyo ambao walikuwa wanakuja kutekeleza mtaala mpya hasa wa awali wa mwaka 2016, ina maana kama mtaala huu haupo nini hatma ya hawa graduate?
Badala yake tunashuhudia kupelekwa kwa walimu wa sekondari katika shule za msingi kufanya utekelezaji wa mtaala ambao hatujausomea, ikiwa waliosomea mtaala huo wapo mitaani.....
Inamaana hili kundi kubwa LA watoto waliopo shule za msingi kwa sasa wakimaliza na kuanza kidato cha kwanza serikali itaturudisha tena maana lazma kutakuwa na uhaba wa walimu tu sasa hizi danadana mpaka lini??maana juzi naona TAMISEMI wameweka tangazo kuwa walimu 11000 was sekondari watapelekwa msingi mwaka huu....
AU NDIO WANAPELEKWA KULE WAZOEE MAZINGIRA MAPEMA YA KUFUNDISHA DARASA LA 8 - 10 YA ELIMU MSINGI,TUFAFANULIENI HILI FUMBO
Karibuni kwa michango......
Sent using Jamii Forums mobile app