Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,947
- 74,429
Rais huyu wa Tanzania ametokea katika kundi (hama) kubwa la utawala wenye itikadi za kubagua wananchi wengine, wasio taka maridhiano, wenye wivu na nongwa na wengine wakatili kwa wenye itikadi tofauti.
Lakini yeye katikati yao amejitokeza na kuwa tofauti nao kabisa. Huku wenzake wakionyesha wazi kuwa hawafurahishwi na hizo tabia njema alizo nazo za kutaka maridhiano kama taifa na mabadiliko na bila kupepesa maneno kinachomsaidia kufanya haya ni nguvu ya mamlaka ya Urais tuu sio support ya wenzake kwenye chama maana hiyo hana.
Kwa wana historia wanakumbuka tabia za kisiasa za makaburu wa SA, ubaguzi wao, ukatili nk hadi ujio wa Rais F W de Klerk ambaye ndiye alimuachia toka Jela Mandela na wanamapinduzi wengi. Kisha Katiba ya muda ikapita na uchaguzi huru kufanyika.
Ukiangalia kwa makini Rais Samia ana kila sifa za kuonekana kuwa ni F W de Klerk mpya wa Tanzania ya sasa. Hivyo CCM wakae mkao wa kutulia afanye kazi yake kwa kushirikiana na wenye nia njema na taifa.