Je, Rais Magufuli ni mbinafsi?

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,219
6,650
Tumesikia, tunasikia na tutasikia mengi kwenye kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu. Moja katika hayo mengi ni la ujenzi wa kiwanja cha ndege, Chato. Ni suala ambalo Lissu, mgombea wa CHADEMA wa Urais, aachi kulitaja. Na hata leo katika mkutano wake na waandishi wa habari, limechukua sehemu muhimu na kupewa uzito mkubwa. Ni nini nyuma ya shutuma hiyo.

Naiita shutuma kwa sababu Lissu anataka Watanzania na hasa wapiga kura wafahamu na kuamini kuwa Magufuli si mwaminifu na ni mtu binafsi. Ili kuamini hicho ni vyema tukazingitia misingi ya ujenzi wa kiwanja hicho na mengineyo.

1) IlanI ya uchaguzi Mkuu, 2015, CCM iliiagiza Serikali yake katika kipindi cha miaka mitano (2015/20) kutekeleza mikakati ya kukuza utalii nchini kwa kuhakikisha mojawapo ikiwa ni kuongeza msukumo katika utalii wa kihistoria kwa kuboresha miundombinu kwenye maeneo ya malikale na kuyatangaza maeneo hayo. Mkoa wa Geita, Chato ikiwa ni Wilaya, ina hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo na na Burigi. Kwa mkoa wa Geita, Wilaya ya Chato ndiyo yenye eneo linalofaa kwa ujenzi wa uwanja wa ndege wenye kiwango kinachokidhi mahitaji hayo.

2) Kwamba ni mbinafsi, hoja hii inatia shaka kwa anayetaka jamii ya Kitanzania ielewe hivyo. Magufuli akiwa Rais, amekuwa akitekeleza Ilani ya Uchaguzi ya chama ipasavyo. Mifano ni kama:

√ Mikoa 20 Serikali itenge Maeneo Maalumu ya Uwekezaji ili yawekewe miundombinu ya msingi itakayovutia Sekta Binafsi kujenga viwanda na kufanya biashara katika maeneo hayo;

√ Katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2020, Chama Cha Mapinduzi kimeielekeza Serikali kuendelea kutekeleza miradi ya
ujenzi wa barabara na madaraja, vivuko, nyumba na majengo ya Serikali kwa lengo la kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi na huduma za kijamii. Aidha, kipaumbele katika ujenzi wa barabara kitazingatia barabara zinazounganisha nchi yetu na nchi jirani; barabara zinazounganisha mikoa; na barabara zinazokwenda kwenye maeneo yenye fursa za kiuchumi. Watanzania ni mashuhuda kuwa siyo tu miundo mbinu ya barabara na vivuko imekuwa ikiimarishwa, kumekuwepo pia na ufufuaji wa reli ya zamani (Tanga-Moshi-Arusha), ufufuaji na ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makubwa nchini (Victoria, Tanganyika na Nyasa). Bila kusahau upanuzi wa viwanja vya ndege kila mkoa ili ndege ziweze kutua na kuruka kwa usalama, ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), na mradi wa kufua umeme wa uhakika na wa bei nafuu. Kwa hili napenda kutofautiana na Mh Lissu ambaye anadai mradi wa kufua umeme kwa gesi uwekwa kando. La, hasha. Kama ana ufahamu kidogo wa uchumi, anapaswa kujua kuwa gharama za kufua umeme wa gesi ni kubwa, isitoshe ni nishati isiyo endelevu na gesi pia inajitajika kwa matumizi mengine.

Yako mengi yaliyoainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi 2015 yaliyotekelezwa na yanaendelea kutekelezwa km ukarabati wa shule kongwe bila ubaguzi wa aina yoyote wala ubinafsi wa Rais Magifuli, anavyotaka Lissu Watanzania waamini.
 
Ana roho mbaya sana watz hatuna roho hizo. Angepewa haki ya kugawa pumzi Hakuna ambae angebaki duniani.
Kuwabomolea nyumba wanadamu wenzako, kuwafukuza kazi, kuwakomoa wafanyakazi kisa eti walichagua upinzani sijaona roho hii
 
Maendeleo yana chama lkn udikteta hauna chama sote tunasulubiwa pamoja
 
..angewapatia wananchi wa Chato mradi wa maji, au mwingine wowote ule wenye uhitaji nao, na siyo kuwajengea uwanja wa ndege wasiouhitaji.
 
Tumesikia, tunasikia na tutasikia mengi kwenye kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu. Moja katika hayo mengi ni la ujenzi wa kiwanja cha ndege, Chato. Ni suala ambalo Lissu, mgombea wa CHADEMA wa Urais, aachi kulitaja. Na hata leo katika mkutano wake na waandishi wa habari, limechukua sehemu muhimu na kupewa uzito mkubwa. Ni nini nyuma ya shutuma hiyo.

Naiita shutuma kwa sababu Lissu anataka Watanzania na hasa wapiga kura wafahamu na kuamini kuwa Magufuli si mwaminifu na ni mtu binafsi. Ili kuamini hicho ni vyema tukazingitia misingi ya ujenzi wa kiwanja hicho na mengineyo.
1) IlanI ya uchaguzi Mkuu, 2015, CCM iliiagiza Serikali yake katika kipindi cha miaka mitano (2015/20) kutekeleza mikakati ya kukuza utalii nchini kwa kuhakikisha mojawapo ikiwa ni kuongeza msukumo katika utalii wa kihistoria kwa kuboresha miundombinu kwenye maeneo ya malikale na kuyatangaza maeneo hayo. Mkoa wa Geita, Chato ikiwa ni Wilaya, ina hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo na na Burigi. Kwa mkoa wa Geita, Wilaya ya Chato ndiyo yenye eneo linalofaa kwa ujenzi wa uwanja wa ndege wenye kiwango kinachokidhi mahitaji hayo.
2) Kwamba ni mbinafsi, hoja hii inatia shaka kwa anayetaka jamii ya Kitanzania ielewe hivyo. Magufuli akiwa Rais, amekuwa akitekeleza Ilani ya Uchaguzi ya chama ipasavyo. Mifano ni kama:
√ Mikoa 20 Serikali itenge Maeneo Maalumu ya Uwekezaji ili yawekewe miundombinu ya msingi itakayovutia Sekta Binafsi kujenga viwanda na kufanya biashara katika maeneo hayo;
√ Katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2020, Chama Cha Mapinduzi kimeielekeza Serikali kuendelea kutekeleza miradi ya
ujenzi wa barabara na madaraja, vivuko, nyumba na majengo ya Serikali kwa lengo la kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi na huduma za kijamii. Aidha, kipaumbele katika ujenzi wa barabara kitazingatia barabara zinazounganisha nchi yetu na nchi jirani; barabara zinazounganisha mikoa; na barabara zinazokwenda kwenye maeneo yenye fursa za kiuchumi. Watanzania ni mashuhuda kuwa siyo tu miundo mbinu ya barabara na vivuko imekuwa ikiimarishwa, kumekuwepo pia na ufufuaji wa reli ya zamani (Tanga-Moshi-Arusha), ufufuaji na ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makubwa nchini (Victoria, Tanganyika na Nyasa). Bila kusahau upanuzi wa viwanja vya ndege kila mkoa ili ndege ziweze kutua na kuruka kwa usalama, ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), na mradi wa kufua umeme wa uhakika na wa bei nafuu. Kwa hili napenda kutofautiana na Mh Lissu ambaye anadai mradi wa kufua umeme kwa gesi uwekwa kando. La, hasha. Kama ana ufahamu kidogo wa uchumi, anapaswa kujua kuwa gharama za kufua umeme wa gesi ni kubwa, isitoshe ni nishati isiyo endelevu na gesi pia inajitajika kwa matumizi mengine.

Yako mengi yaliyoainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi 2015 yaliyotekelezwa na yanaendelea kutekelezwa km ukarabati wa shule kongwe bila ubaguzi wa aina yoyote wala ubinafsi wa Rais Magifuli, anavyotaka Lissu Watanzania waamini.
Mbona maelezo yako ya
ufafanuzi wa umuhimu wa kiwanja cha ndege Chato hayajitoshelezi? Ongeza nyama kidogo mkuu tuone faida za kiuchumi za huo uwanja. Ili watu wabaya waache kuulinganisha na ule wa dikteta Mobutu aliojenga kijinini kwao Gbadolite
 
Ni hivi, Magufuli ni mbinafsi na hilo halina mjadala wala halihitaji elimu ya chuo kikuu kulitambua. Sisi watanzania hilo tunalijua muda mrefu, anachofanya Lisu sasa hivi ni kulisema tu hadharani, ila kila mtanzania hilo analijua.
 
Mbona maelezo yako ya
ufafanuzi wa umuhimu wa kiwanja cha ndege Chato hayajitoshelezi? Ongeza nyama kidogo mkuu tuone faida za kiuchumi za huo uwanja. Ili watu wabaya waache kuulinganisha na ule wa dikteta Mobutu aliojenga kijinini kwao Gbadolite

Si yeye tu, mtetezi yoyote wa huo uwanja wa ndege wa Chato huwa anaanza kama anajenga hoja, kisha anachomekea mambo mengine ili kufunika hiyo aibu. Fuatilia vizuri maelezo ya MATAGA wote.
 
Back
Top Bottom