Je Prof. Shivji ni Mtanzania?

Je Prof. Shivji ni Mtanzania?

Lugha ya mtu aimwondolei haki yake ya kuwa Mtzd tembea uone hahapa TZ wako watu hawajui kiswahili, Labda unalako weka wazi

Huyo ana shetani la ubaguzi wa rangi.Kwani lafudhi gani ndiyo inaonyesha utanzania halisi?Mbona watanzania wote tunaongea kiswahili kila mtu kwa lafudhi ya kabila lake?kwa hiyo na sisi wote si raia??Huyo mkabila sana.
 
Mmmmh!!! Hivi mkuu kweli kuna sehemu tz hii wanatumia ligha za makabila kufundishia masomo ya darasani?

Na wewe acha USHAMBA kwani ukijua kiswahili ndio umefuta ujinga?hiyo ni lugha tu kama ilivyo kisukuma,kichaga,kihaya,kiha n.k.Lugha haina uhusiano na elimu.Nyie ndio wenye mawazo kuwa mtu akijua kiingereza ni msomi???!!!.Mtu anaweza kuwa msomi kwa kutumia lugha yake ya mama na mfano mzuri ni nchi za China,Japan,Korea,Urusi,Ujerumani,Ureno n.k
 
Hoja yako ni bubu. Sema utakalo ueleweke hoja ni hoja tu bila kujali inatoka wapi- kwa nini hata uulize swala hili au unataka kujenga 'biased opinion?
 
Nimeengalia kipindi chake cha ITV
nimeshidwa kuelewa kama kweli ni mtnzania

Inakuwa Prof mzima kiswahili kinampiga chenga?

Je utaifa wake ndo mana Rais hajamueka kwenye kamati ya katiba?

Wikipidia wanasema hivi

Born in Kilosa, Tanzania in 1946, Professor Shivji was for 36 years a distinguished professor in Constitutional Law in the University of Dar es Salaam's Faculty of Law. He is a professor of international renown, having built his reputation through the publication of over 18 books, numerous articles and book chapters. Shivji has served as advocate of the high court and the Court of Appeal of Tanzania since 1977 and advocate of the high court in Zanzibar since 1989. He has received several national and international distinguished scholar awards, including an honorary doctorate from the University of East London, UK.

Ama kweli dunia ina mambo.
 
Suala la lugha lisikuumize kichwa mkuu,wengi wetu hatukifahamu Kiswahili fasaha mfano mzuri ni mitihani ya Kiswahili ni nani anaweza kupa 100%

Hata mama yangu hajui kiswahili. Wanajua kiswahili nchi hii ni kama 70% tu. Kijijini huku watu wa umri kuanzia miaka 60 wengi hawajui kiswahili.
 
Jibu kwa swali lako ni: Ndio Prof. Issa Shivji ni mtanzania mzalendo na mwenye uchungu na nchi hii.
 
Lugha ya mtu aimwondolei haki yake ya kuwa Mtzd tembea uone hahapa TZ wako watu hawajui kiswahili, Labda unalako weka wazi

Ingekuwa kujua lugha ya Kiswahili ni kigezo cha kuwa Mtanzania, basi wengi tungeshawatimua nchini. Mleta mada, Prof Shivji ni Mtanzania halisi. Kwenye katiba hakuna mahali panaposema kwamba, ili uwe Mtanzania lazima ujue Kiswahili. Pole sana
 
Mkuu nenda Usukumani au nenda Bukoba kuna Watanzania hawajawahi kuongea kiswahili kabisa.


Wengi hawajui kuwa lugha inayozungumzwa zaidi Tanzania ni Kisukuma kikifuatiwa na Kiswahili
 
Shivji sio tu mtanzania, ni mtanzania mzalendo wa kweli. Suala la lugha, mimi mpaka leo sijui tofauti ya l na r kwani kabila letu hatuna r kama walivyo wakulya hawana l. ni inapokuja kwenye kizungu imebidi niwe na kufomula kangu kuwa zinapokuja herufi zote mbili daima r hutangulia kama ilivyo kwenye neno pearly. Lugha sio mchezo mrahisi kama tunavyodhani wengi
 
Utanzania sio rangi ya mtu ni uzalendo tu unaotakiwa Prf. Shivji ni mbogo kabisa amesimama ni mfano kwa jamii.
Hee, mara hii Prof. wa watu kawa mnyama wa porini? Kwahiyo ni Mtanzania wa mbuga gani za kwetu hapa Tz? Watu wengine bwana, sijui miili yao imetengana na akili?????!!!!!!!!!!
 
Hebu tuache ubaguzi,tusome vyema Ibara ya 12 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Prof. Shivji ni mtanzania mzalendo mwenye kujivunia utanzania zaidi ya asili yake ya kiasia aliyonayo. Tukumbuke kuwa kujua au kutokujua kiswahili hakumfanyi mtu ashindwe kuwa mtanzania.

Je, ni wabunge wangapi huwa wanachapia kiswahili bungeni kwa kubadili msimbo pasipo na sababu ya msingi??? Je,nao tuwaite si watanzania kisa tu hawajui kiswahili ipasavyo(vyema)???? Mfano; hapa kwetu Rorya waluo hawawezi kusema neno "kiberiti" wanasema "kubriti" lakini bado ni watanzania na wanajivunia utanzania wao. Tofauti za rangi hazina msingi katika taifa lenye tunu za kutukuka kama Tanzania.

Kitendo cha kutojumuishwa kwake katika tume ya kuratibu mabadiliko ya katiba,haikuwa ni kwa sababu yeye si mtanzania,bali ni kuwa si sote tungepata nafasi hiyo. Wachache watuwakilishe. Pia tukumbuke kuwa taasisi na watu walitakiwa kutoa mapendekezo ya majina ya watu wanaofaa kuwa katika Tume,huenda Prof. Shivji hakupendekezwa.
 
Back
Top Bottom