Je, Nyumbu aweza kula chakula pamoja na Simba?

Je, Nyumbu aweza kula chakula pamoja na Simba?

manking

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2014
Posts
1,306
Reaction score
316
Ni swali ambalo jibu lake ni gumu kidogo kwakuwa nyumbu ni kitoweo cha simba japo yawezeka ikawa kwasababu tu aidha simba ameng'olewa meno au ni mgonjwa hajiwezi. Katika harakati za siasa na madaraka na kuutaka ungozi kumekuwa na watu kugeuka kondoo kwa nje hali yakuwa ni mbwa mwitu wakali ndani yake.
Uchaguzi mwaka huu watu tuliowaona ni simba na mbwa mwitu (yaani maadui kwa ufisadi na uongzi mbaya) leo wanatulaghai kuwa wao sio simba tena ni wanyama wapole wao ni nyumbu si maadui tena na twaweza kula nao tukanywa nao bila madhara yeyote. ukweli ni kwamba hao ni simba kwa asilia wamevaa ngozi ya nyumbu wako mawindoni kuwala nyumbu wanyama wapole wasio na hila.

MWANANCHI AMKA UTAKUJA INGIA MTEGONI KATAA KUSHIRIKIANA NA MAFISADI SIMAMA IMARA IKULU NI PATAKATIFU.
 
Ujumbe umetulia. Ila mda si mlefu. Utasikia wanaanza kukukosoa na wakati apo haujatja chama. Na watakao kukosoa utawajua tu ni chama gani
 
Ujumbe umetulia. Ila mda si mlefu. Utasikia wanaanza kukukosoa na wakati apo haujatja chama. Na watakao kukosoa utawajua tu ni chama gani
Mkuu kwa wapenda mabadiliko ya kweli hatuna budi kusema, na kuutangaza ukweli.
 
Lumumba viti vya moto havikaliki tena lowasa anawapausua vichwa sana.
 
Back
Top Bottom