sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,032
Kuna watu wenye noti zilizoungua, kufubaa, kuchanika chanika, zenye matobo, n.k kwa kukosa maarifa huziona hizi noti hazifai na huzikacha, kuzitupa ama kuziuza kwa hasara kwa wanaokusanya noti mbovu mitaani
kuna mdau aliangusha waleti anapovuka barabara, waleti yake ilikanyagwa kanyagwa na magari mengi sana, alipofanikiwa kuiokoa alikuta pesa zake zilikuwa zimechanika vibaya mno basi akazitupa jalalani, Hayo maamuzi hayakuwa sahihi.
Noti ni karatasi tu ila thamani yake ipo kulingana na idadi ya noti zilizomo kwenye mzunguko, Kwa kulitambua hili Benki kuu ya taifa watakupa noti mpya na kuzichukua zile zilizoharibika.
Jambo la msingi ni kuhakikisha noti zako hazijaharibika upande wa namba hizo nilizozizungushia kwenye p[icha nliyoweka kwenye maada hii,
Iwapo pande zote mbili zipo basi utaenda benki kuu na utabadilishiwa fedha zako kwa kiasi chote, mfano ukipeleka elfu kumi utarudishiwa elfu kumi mpya.
Endapo upande moja wa namba hizo umeharibika sana au haupo basi utapewa nusu ya hela uliyopeleka, mfano ukipeleka elfu kumi utapewa elfu tano.
Pia unaweza kupeleka noti hizi benki ya posta au vituo vya mafuta.