Je, noti zako zimeungua, kuchanika, matundu, kufubaa nk? Usizitupe, fanya haya upewe mpya

dudu jeupe

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
739
1,000
1589813213573.png


Kuna watu wenye noti zilizoungua, kufubaa, kuchanika chanika, zenye matobo, n.k kwa kukosa maarifa huziona hizi noti hazifai na huzikacha, kuzitupa ama kuziuza kwa hasara kwa wanaokusanya noti mbovu mitaani

kuna mdau aliangusha waleti anapovuka barabara, waleti yake ilikanyagwa kanyagwa na magari mengi sana, alipofanikiwa kuiokoa alikuta pesa zake zilikuwa zimechanika vibaya mno basi akazitupa jalalani, Hayo maamuzi hayakuwa sahihi.

Noti ni karatasi tu ila thamani yake ipo kulingana na idadi ya noti zilizomo kwenye mzunguko, Kwa kulitambua hili Benki kuu ya taifa watakupa noti mpya na kuzichukua zile zilizoharibika.

Jambo la msingi ni kuhakikisha noti zako hazijaharibika upande wa namba hizo nilizozizungushia kwenye p[icha nliyoweka kwenye maada hii,

Iwapo pande zote mbili zipo basi utaenda benki kuu na utabadilishiwa fedha zako kwa kiasi chote, mfano ukipeleka elfu kumi utarudishiwa elfu kumi mpya.

Endapo upande moja wa namba hizo umeharibika sana au haupo basi utapewa nusu ya hela uliyopeleka, mfano ukipeleka elfu kumi utapewa elfu tano.

Pia unaweza kupeleka noti hizi benki ya posta au vituo vya mafuta.
 

dudu jeupe

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
739
1,000
Vile vile unaweza kwenda kuziweka kwenye account yako bank au kununulia mafuta kwenye vituo vikubwa eg Camel, total, lake n.k.
Au unaweza kuibadirisha bank ingawa huwa wanasumbua kidogo but nimebadiri Mara 6 katika bank za NMB & CRDB
zilipatwa na tatizo gani noti zako
 

lufungulo k

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
2,260
2,000
Bank ya Posta nimeona kuna dirisha maalum la kupokea na kubadilisha Pesa chakavu.
 

Benhorta

Member
May 8, 2016
64
400
Kuna mtu aliwahi kuchana note ya shiling elfu 10 vipande vipande kisa ugomvi na hasira, Unaweza kufafanua je mtu akienda bank na hivi vipande anaweza kupewa pesa mpya?
 

Cute shy

JF-Expert Member
Apr 27, 2015
1,135
2,000
Kuna mtu aliwahi kuchana note ya shiling elfu 10 vipande vipande kisa ugomvi na hasira, Unaweza kufafanua je mtu akienda bank na hivi vipande anaweza kupewa pesa mpya?
Anaipanga vizuri unagundisha unapeleka bank yeyote siku hizi siyo mpaka bank kuu
 

Savimbi Jr

JF-Expert Member
Sep 23, 2011
6,754
2,000
Shukrani sana kumbe wale wanaonunua hela mbovu wanapiga pesa sana......Maana unatoa Buku bovu kwa jero.
 

dudu jeupe

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
739
1,000
Kuna mtu aliwahi kuchana note ya shiling elfu 10 vipande vipande kisa ugomvi na hasira, Unaweza kufafanua je mtu akienda bank na hivi vipande anaweza kupewa pesa mpya?
Akiiunganisha na hizo namba zikaonekana atapewa
 

Vitalis Msungwite

Verified Member
May 11, 2014
2,117
2,000
zilipatwa na tatizo gani noti zako
Sio kwa Sikh moja ni katika kipindi cha miaka mitano. Noti nyingine zilikuwa zimechanika na kuungwa kwa soltep, nyingine zilichakaa, nyingine not ya 5000 ilichanika vipande viwili katika ugomvi wa mpangaji mwenzangu na mkewe nikaokota nikaenda kuexchange CRDB nikapewa mpya.
 

nduza

JF-Expert Member
Feb 7, 2019
491
500
huwezi pata msaada wowote unatakiwa uwe nazo zote kuepuka janja janja
Unapewa nusu ya pesa mkuu
Niliuziwa laki mbili iliyoliwa na panya pale feri kwa elfu 80 nilienda BoT katika hizo pesa noti nne zilikuwa namba zipo upande mmoja tu kwa hiyo nilichukua laki na 80
Kuna dirisha maalumu kwa pesa chakavu pale

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom