Je niwakati wa samia kuunda Samia gang au bado?

Je niwakati wa samia kuunda Samia gang au bado?

kimfly

Member
Joined
Aug 27, 2021
Posts
16
Reaction score
50
Binafsi namshauri Samia kuunda gang yake kwa sasa ili aweze kupata uungwaji mkono katika harakati zake za kuutaka urasi 2025-2030 kama jinsi yeye alivyotamka hadharani,tumeshuhudia katika awamu zilizo pita viongozi wakuu wa nchi na ndiyo wenye viti wa chama waliweza kupata [emoji817] ya uungwaji mkono ndani ya chama Chao kutokana na gang walizo kuwa wamezitengeneza ndani ya chama na serikalini
Tumeshudia msoga gang ambayo mpaka sasa bado ipo ikiwa na wafusia kibao ikiongozwa na
Jk
Kinana
Nape
Mzee makamba
January makamba
Mizengo pinda na wengine kibao
Hali kadhali tumeshudia sukuma gang ambayo ilikuwepo katika awamu iliyopita ambayo kwass imeelemewa na mzigo na kuanza kuyumba na kupoteza mweleko kabisa ambyo ilikuwa ikiongoza na
Jpm
Bashiru Ali
Polepole
Kasimu majaliwa
Ndugai
Gang hizi ziliwezesha kiongozi mkuu kufanya kazi huku akila kachori na mkate wa kumimina kiraini kabisa kwa sababu ndani ya gang hizo kazi yao nikuweka mambo sawa pindi kiongozi wao unapochafuliwa vibaya, kitu ambacho sijakiona baada ya ndugai kumsema hovyo Samia, hivyo basi ni mda wa Samia sasa kuunda Samia gang kama anautaka uraisi 2025-2030
 
Back
Top Bottom