Je, nimshitaki au nimuache tu?

Je, nimshitaki au nimuache tu?

happy amos

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
251
Reaction score
434
Wazima jamani?

Naombeni ushauri nina mzazi mwenzangu tumezaa nae mtoto 1.Hapo nyuma alikua anahudumia tu mtoto wake tangu mi nilipopata mume akabadilika akaanza kutuma meseji za kujua hali ya mtoto usiku.

Nikamzuia nikamwambia hata kama ungekua wewe mkeo atafutwe na mzazi mwenzie usingejisikia vizuri, kabla ya Christ- mass aliniambia anataka nimpeleke mtoto kwao nikamkubalia tunaishi mikoa tofauti.

Tarehe 23/12 Mr akaniambia twende kwao tukale sikukuu nikashindwa kumpeleka mtoto ikabidi nimwambie tusubiri wakati mwingine akawa kachukia na hela ya matumizi kasitisha kutoa.

Naombeni mnishauri nimpeleke ustawi wa jamii au niachane nae tu
mtoto ana 3yrs kwa sasa binafsi najua matunzo haina shida nawaza uko mbele akianza shule je nitaweza? Vipi huyu Mr atakubali kumsomesha?

Vipi akimsomesha jamaa mbeleni akaja kumdai mtoto wake?

Naombeni mawazo yenu
 
Kwani wewe umeamuaje? Mr mpya yeye ulivyomuambia kuhusu hilo swala nakuambiaje?

Kama uwezo unao fanya kumtunza mtoto wako..
 
Pole kwa yaliyokukuta mpendwa kwanza nataka uelewe kuwa huyo mwanaume uliyezaa nae anawivu wa ajaabu yaan lengo lake anataka avuruge ndoa yako pili kuhusu malez pamoja na kumsomesha mtoto so vibaya kama huyo Mr atahusika maana kapenda boga na lazima apende ua lake usije ukahofia hata kidogo kuwa jamaa uliyenae akimsomesha je huko mbele itakuaje kumbuka huyo ni mtoto wenu huyo jamaa unaeishi nae hawez kukwepa kwa lolote na kwa maana kwamba huyo uliyezaa nae hawezi kutoa kila kitu kwa huyo mtoto ndio maana kuna mlez na mzaz hivyo ushauri wangu ni kwamba mzazi mwenzako usimpeleke ustawi na kama analengo la kumuhudumia mtoto wake atafanya tyu wewe lakin kama akikuwa anamuhudumiwa mwanawe kwa lengo la kuvuruga mahusiano yako ndo utajua ustawi hakuna mashiko sana maana tayar umeolewa na bwana mwingine hivyo tunachukulia huyo bwana uliye nae ndo baba wa mtoto
 
Nah. Usimshitaki. Ana sababu ya kukasirika. Alikuwa na hamu ya kwenda na mwanae akawasalimie ndugu zake wengine.

After some time he will be okay, hasira zikishapungua.

On the other hand mbali na financial support unayopata kutoka kwa baba ya mtoto hakikisha anapata emotional support pia kutoka kwa baba yake na ile bond iwepo.

Please ,never come between a father and his kids especially akiwa na interest na mtoto wake.
 
Acha kutegemea mtu mwingine kwny malezi ya mtt especially km una mume mwingine cz utakuja kuleta shida kwny ndoa yako


Mtoto ni wako pambana tu mwenyewe
 
Mhhhhh haya masuala ya kuoa mtu aliezaa na mtu mwingine huwa nichangamoto toka nikiwa mdogo had leo nina akili zangu sijawah kuona yakitulia
 
Baba anahitaji mapenzi ya mtoto pia sio kuhudumia tu maana naona ndicho ulichoshikilia tu.

Kama hautaki kumpeleka mtoto kwake walau hizi sikukuu basi mnaoshinda naye mmhudumie.

Amekasirika.
 
MPE jamaa mtoto wake ,ubaki na mumeo ..mchezo uishe !!!.

Alafu acha kulia lia ivo ,,hata uyo Mumeo naye anakuhesabia target !!....
 
Acha Maujinga.!

Huyo alie kuoa si ulimweleza kuwa una mtoto na mpaka amekuoa inamaana amekubaliana na hali aliyo kukuta nayo. Kwahiyo kuhudumia mtoto yampasa amuhudumie ata kama si wakwake maana kigezo tosha ni ww na huyo ni mwanao ingekuwa si mwanao hapo sawa. Sikatai na wala sipingi kwamba huyo mlie zaa nae ni wajibu kwake kumuhudumia mwanae lakin kama hataki achana nae, ww si una bwana basi acha huyo bwana wako amuhudumie mtoto.

Na usituletee ushamba hapa eti akihudumiwa huko mbeleni kutatokea mgogoro eti kisa tu amemuhudumia huyo mtoto. Inamaana huyo alie kuoa alitaka Papuchi tu ashindwe kukubeba kama ulivyo? Ata ahudumie vp mtoto atabaki kuwa wa yule ulie zaa nae . kama vp mpe mtoto wake.
 
Kwanini mliachana? Tatizo huanzia hapo! Na kuachana inabidi hata mawasiliano yasiwepo, aliyekuchukua abebe mizigo YOTE uliyonayo
 
Utashindwa kumpeleka mtoto shule ya msingi ya kawaida?? Afu unaenda kula X mass kwao?
 
Kwahiyo hapo ulipo uliishaona dushele mbili tofauti tena katika dunia moja.....jamani!!!
 
hukutakiwa kwenda na mtoto kwa mume mwingine,angetakiwa umuache kwenu au kwa mama yake jamaa,kuishi na mtoto huko kutakuletea matatizo tu kwa njia yyte ile maana ni lazima utakuwa na mawasiliano na mtu mlie zaa nae.
hata huyo mume uliyenaye akimusomesha mtoto,bado baba wa huyo mtoto ana haki ya kuja kumchukua mtoto wake wakati wwte.haya mambo yanatokea sio kwako tu.
mimi nakushauri mtoto akifika miaka 5 mpeleke kwa mama yako-lasivyo ndoa yako hiyo itakuwa mashakani mwanume uliyenaye nae atakuwa anapata wivu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom