Je, nifanye nini?

Je, nifanye nini?

Lukaku marata

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2019
Posts
448
Reaction score
752
Habari za humu wanaForum,

Kwanza kabisa nitoe pole kwa watanzania wote katika msiba huu mzito wa rais wetu mstaafu Benjamin WIlliama Mkapa. Niende moja kwa moja katika suala langu labda nitapata mawazo ya kunisaidia katika muktadha mzima wa maisha yangu kwani ninaamini humu kuna watu mbali mbali wenye uzoefu mbalimbali na wameshapitia mambo mengi magumu na makubwa tena zaidi yangu.

Kiumri nina miaka 26, ninaishi hapa Dar es Salaam nikijishughulisha na shughuli za hapa na pale. Katika maisha yangu kuanzia nilipokuwa chuo miaka 20 nilijiingiza katika mapenzi ya jinsia moja nikiwa ninafanya kama mfanyaji (yaani katika hii society anaitwa “Top”)

Katika kujiingiza kwangu katika huu mchezo sijui hata hiyo nguvu ilitoka wapi japo mwanzoni nilikuwa naogopa ila kutokana na mitandao hii ya kijamii imefanya nikutane na watu ambao tunafanya nao hayo mapenzi, kimsingi katika nchi yetu hata hapa Dar es Salaam watu wanaofanya ni vijana ages ya 20’s to 30’s ambao mimi nilikuwa ninakutana nao japo pia kuna watu wazima mimi hao nilikuwa sipendi kuwa nao.

Tena unakuta hawa vijana huwezi gundua kwamba wanajihusisha na haya mapenzi ya jinsia moja kwa sababu hana viashiria vyoyote vya kuonekana kike au la wengine nikiwemo mimi tuna mademu kabisa lakini bado hivi vitendo vinafanyika.Watu wanaweza dhani kwamba ni tamaa ya pesa lakini kwa watu niliokutana nao 70% hawafanyi sababu ya kusosa hela hiyo inadhihirisha kuwa tamaa ya pesa ndo chanzo,mpaka naandika uzi huu nimeshakutana na watu 20 ambao tumefanya nao haya mambo.

Lengo la kuanzisha huu uzi, kimsingi mimi nimechoka kufanya hivi vitendo kwani ninajua ninaikosea nafsi yangu,Mungu wangu,wazazi wangu na wale watu wote ambao wananiheshimu kwani hukiniona huwezi dhania kabisa kwamba ninafanya huu uchafu nina marafiki wengi tu lakini hakuna hata mmoja anayejua,wengi wanaonijua ni ambao nipo nao kwenye hii industry ambao nikiwa ninawaambia mimi nataka niache haya mambo wananiambia siwezi acha wakisema ninaweza kupunguza lakini sio kuacha.

Maana nimekutana na watu wengi sana kila nikijaribu kuwaambia nataka niache wanasema watu wamejaribu kuacha lakini inashindikana wakisema wengine wamesha wahi hata kwenda makanisani kuombewa lakini wapi,wengine washawahi mpaka kutoa kafara za wanyama lakini wapi.

Sasa nilichoamua naomba ushauri wenu mnisaidie labda ninaweza kupata mawazo tofauti kutoka kwenu because kwa kule nilipokuwa naomba ushauri wote tupo kwenye same boat labda ndo maana wanasema siwezi. Kati ya vitu nilivyokuwa ninafikiria kufanya:

1. Kwenda kwa watu wa psychology labda nikapate ushauri may be
2.Kujitoa uhai maana mateso ninayopata nafsini mwangu najua mimi na roho yangu

NOTE:
Huu uzi hauna lengo la kuvutia mtu yoyote katika hayo mambo,napia najua kuna watu watakuja hapa kunitukana na etc lakini niwaambie kitu kama wewe ni kijana unaweza kupata mtoto akawa anahiyo changamoto au hata pia mzazi wako yupo kwenye haya mambo au kama wewe ni mzazi na una mtoto wa kiume huwezi jua maana mimi hata wazazi wangu hakuna anayejua hata ndugu zangu so takecare
 
Pole na hongera kwa kuliweka wazi tatizo linalo kutesa (ingawa kwa utamaduni wetu, wapo watakao kuchukia, kukubeza na kukuhukumu pia).
1. Jaribu kujiepusha zaidi/kaa mbali na hao unao wafanya.
2. Futa mawasiliano ya watu wote wanao jiushisha na ufirauni.
3. Tubu dhambi hii na kisha jiwekee utaratibu wa kusali/kuomba kila wakati.
4. Jiweke karibu na Mungu, na hudhuria kila ibada (kwa imani yako).
5. Anza kufanya kitu chochote (chema) ambacho kitakuweka kuwa busy kwa masaa mengi kilasiku.
6. Kama ukiweza hama hili eneo/mkoa/wilaya ili kujiweka mbali na hao mafirauni.
 
Mkuu unasumbuliwa na jini mahaba huyo ndo huleta ufirauni wa namna hiyo, cha msingi jiingize rasmi katika kumtumikia mungu ili unasuke na mtihani huo, japo huyo jin mahaba atakutia uzito sana utakapofanya mikakati ya kumkataa we kaza buti mpaka pale utakapohisi upo huru.
 
1: Futa mawasiliano ya wote unaowafanya na Top wenzio / ikiwezekana tupa line sajili mpya
2: Hama mkoa au mji uliopo kakake mbali na eneo wanalokujua
3: Nenda katubu dhambi zako. Ongea na mchungaji kama muislam bas nenda msikitini ukapewe somo na kuslim
4: Tafuta shuguli itakayokuweka bize kuanzia asubuhi mpaka jioni
 
Tiba ya kwanza na ya kuzingatia ni Mental upset yako, uki ikataa tabia ndani ya Nafsi+Roho akili huonesha matokeo, ila kujiepusha mbali na vishawishi vyote vya kishoga, mshirikishe Allah ataongeza nguvu ya kujikana nafsi kwa hilo jambo, Pole sana, "Dunia haina fundi"
 
Pole na hongera kwa kuliweka wazi tatizo linalo kutesa (ingawa kwa utamaduni wetu, wapo watakao kuchukia, kukubeza na kukuhukumu pia).
1. Jaribu kujiepusha zaidi/kaa mbali na hao unao wafanya.
2. Futa mawasiliano ya watu wote wanao jiushisha na ufirauni.
3. Tubu dhambi hii na kisha jiwekee utaratibu wa kusali/kuomba kila wakati.
4. Jiweke karibu na Mungu, na hudhuria kila ibada (kwa imani yako).
5. Anza kufanya kitu chochote (chema) ambacho kitakuweka kuwa busy kwa masaa mengi kilasiku.
6. Kama ukiweza hama hili eneo/mkoa/wilaya ili kujiweka mbali na hao mafirauni.

Asante sana, mawasiliano huwa ninafuta changamoto ni kwenye mitandao...Mimi ni blogger hivyo muda mwingi nipo na internet so nirahisi kuingia kwenye mitandao hiyo
 
Tiba ya kwanza na ya kuzingatia ni Mental upset yako, uki ikataa tabia ndani ya Nafsi+Roho akili huonesha matokeo, ila kujiepusha mbali na vishawishi vyote vya kishoga, mshirikishe Allah ataongeza nguvu ya kujikana nafsi kwa hilo jambo, Pole sana, "Dunia haina fundi"

Naipataje hiyo mental upset?
 
1: Futa mawasiliano ya wote unaowafanya na Top wenzio / ikiwezekana tupa line sajili mpya
2: Hama mkoa au mji uliopo kakake mbali na eneo wanalokujua
3: Nenda katubu dhambi zako. Ongea na mchungaji kama muislam bas nenda msikitini ukapewe somo na kuslim
4: Tafuta shuguli itakayokuweka bize kuanzia asubuhi mpaka jioni

Mawasiliano sina changamoto ni internet
 
mkuu unasumbuliwa na jini mahaba huyo ndo huleta ufirauni wa namna hiyo, cha msingi jiingize rasmi katika kumtumikia mungu ili unasuke na mtihani huo, japo huyo jin mahaba atakutia uzito sana utakapofanya mikakati ya kumkataa we kaza buti mpaka pale utakapohisi upo huru.
Hivi kwanini jini mahaba husumbua waafrika tu?
Mbona wazungu wenye addiction za ngono hutibu na was psychology?
Kwani majini hawawajui wazungu?

#YNWA
 
28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi
Lukaku marata, YESU anakupenda, Ni yeye anayetutakasa na kutubadilisha, sio kwa juhudi na akili zetu.
Muombe yeye akubadilishe, nipo tayari kushirikiana na wewe ili Mungu aweze kujidhihirisha maishani mwako.
Hamna aliye Mtakatifu chini ya jua, Ila Kuna vitu Ni lazima kuviacha Sasa ikiwemo ufiraji.
Mungu ana nguvu ya kukufanya uwe kiumbe kipya Sasa.
Pokea nguvu mpya iletayo wokovu Sasa, katikati jina la YESU anayeishi na kutawaliwa. Amen
 
Hivi kwanini jini mahaba husumbua waafrika tu?
Mbona wazungu wenye addiction za ngono hutibu na was psychology?
Kwani majini hawawajui wazungu?

#YNWA
Unazungumzia wazungu wapi? hawa hawa ambao wamehalalisha kulawitiana na michezo michafu ya kila aina? ushetan tulionao waafrica haujafikia hata robo ya walio nao wazungu...

Kitu usichokijua ni kua hakuna binadam anaeweza kutenda mambo ya kishetani bila kutenzwa nguvu katika ulimwengu wa roho na mashetan, na hapa ndo ulipo mzizi wa fitna wa matendo yote yakishetani.

Hebu kaa kitaalam mkuu, wazungu hao hao wanatumia nguvu za giza katika kufanikisha mambo chungu nzima ya kisayans na tecnolojia bt mbona hawajawah tutangazia kua wanatumia? kua huru kifikra upate kuelimika.
 
unazungumzia wazungu wapi? hawa hawa ambao wamehalalisha kulawitiana na michezo michafu ya kila aina? ushetan tulionao waafrica haujafikia hata robo ya walio nao wazungu...

kitu usichokijua ni kua hakuna binadam anaeweza kutenda mambo ya kishetani bila kutenzwa nguvu katika ulimwengu wa roho na mashetan, na hapa ndo ulipo mzizi wa fitna wa matendo yote yakishetani.

hebu kaa kitaalam mkuu, wazungu hao hao wanatumia nguvu za giza katika kufanikisha mambo chungu nzima ya kisayans na tecnolojia bt mbona hawajawah tutangazia kua wanatumia? kua huru kifikra upate kuelimika.
Hawajatangaza... Halafu unaongelea... Umejuaje ""Are you there coworker?""

Babu Huyu jamaa anasumbuliwa na addiction kama addiction nyengine.
Ana njia mbili...
1. Aingia sobber
2. Akutane na Psychologist kwa ratiba watakayo pangiana.

FULL STOP.

Ingia google soma habari za hao wazungu ambao walipona sex addiction kwa kuonana na psychologist.
Hawakusomea kisomo sijui jini mahaba asepe wala sijui nini "IT IS JUST ADDICTION""

Kwahiyo..

Mtumia smartphone (Nomophobia) Sana ana = Jina Android
Mtumia pombe ana = Jini TBL
Anaye sex na wanawake sana = Jini papuchi.
Work addiction = Jini high pay..!!!

Hayo ya jini mahaba sijui jini kisirani TUACHE KUAMINI UJINGA.
Na tupunguze kumsingizia shetani dhambi zisizo muhusu.

#YNWA
 
Akili isipoutawala mwili ni sawa na basi kuacha barabara...
Tumia akili, imani, dhamira halisi kuacha taratibu. Kila kitu kinawezekana penye nia.
 
Back
Top Bottom