Je, ni White Cement, Wall Putty au Gypsum Powder kwenye skimming ndani ya nyumba?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,523
27,019
Ndugu zangu!

Nyumba ipo eneo ambalo sidhani kama kuna fungikuvu wala bakteria wala unyevu, (hapa najifariji kuwa sihitaji binder) kwa maana nyumba za huko nyingi ni za udongo na ziko poa tu.

Hata zile za angalau unakuta ni plasta ya simenti tu. Sema mimi nataka kuifanya finishing ya kimjini kabisa.

Hebu nipeni chaguo na sababu zake, kwa kuzingatia ubora na gharama zake.

Karibuni.
 
Tumia JK wall putty,
Inatumika ndani na nje. Unachanya na maji tu na haigandi haraka kama powder au white cement. Haiitaji uchanganye na Emulsion paint kama hizo zingine. Skim coat zako mbili acha ikauke piga msasa namba 120 thank me later.

Asante sana mkuu, nilikuwa nasubiri ushauri huu nifanye maamuzi... nasema asante tena na tena.

Pamoja na majibu mazuri kwenye swali la msingi, nina swali la nyongeza:

Msasa namba 120! Ni nini hii?
 
Asante sana mkuu, nilikuwa nasubiri ushauri huu nifanye maamuzi... nasema asante tena na tena.

Pamoja na majibu mazuri kwenye swali la msingi, nina swali la nyongeza:

Msasa namba 120! Ni nini hii?
Misasa (sand paper) Ina number kutegemeana na smoothness ya ukuta wako au surface yako unayotaka kupaka rangi, kwa ukuta ambao haujaskimiwa vizuri uko rough Sana huwa tunatumia misasa yenye namba ndogo i.e namba 60 au namba 80 hiyo tunaita misasa mikali YAni inafaa kwenye rough surface, but kama fundi wako wa kuskim ni mzuri na surface ni nzuri tunatumia kuanzia msasa namba 100 au 120 au ukitaka smoothness ya kioo tumia 150. Hizo namba ni grade tu za msasa kutegemeana na ukuta wako. Nenda duka la vifaa vya ujenzi kkoo imejaa kibao na wanapima kwa mita buku nadhan.
 
Misasa (sand paper) Ina number kutegemeana na smoothness ya ukuta wako au surface yako unayotaka kupaka rangi, kwa ukuta ambao haujaskimiwa vizuri uko rough Sana huwa tunatumia misasa yenye namba ndogo i.e namba 60 au namba 80 hiyo tunaita misasa mikali YAni inafaa kwenye rough surface, but kama fundi wako wa kuskim ni mzuri na surface ni nzuri tunatumia kuanzia msasa namba 100 au 120 au ukitaka smoothness ya kioo tumia 150. Hizo namba ni grade tu za msasa kutegemeana na ukuta wako. Nenda duka la vida vya ujenzi kkoo imejaa kibao na wanapima kwa mita buku nadhan.

Nakushukuru sana mkuu, pamoja.
 
======

Mrejesho:

Nilitumia WALLPUTTY kampuni ya ANDIKA, Ee bwana wee! Kazi imekuwa tamu kishenzi, mafundi wameskimu nje ndani kwa ustadi mkubwa.

Hapa bado rangi tu.
 
Asante sana mkuu, nilikuwa nasubiri ushauri huu nifanye maamuzi... nasema asante tena na tena.

Pamoja na majibu mazuri kwenye swali la msingi, nina swali la nyongeza:

Msasa namba 120! Ni nini hii?
Mkuu wewe umekulia wapi hata msasa hujui ??, acha mzaha basi !!
 
======

Mrejesho:

Nilitumia WALLPUTTY kampuni ya ANDIKA, Ee bwana wee! Kazi imekuwa tamu kishenzi, mafundi wameskimu nje ndani kwa ustadi mkubwa.

Hapa bado rangi tu.
WALLPUTTY ni nyingine sio JK PUTTY?

Uliipata wapi hii Kariakoo? Na mafundi wazuri je uliwapata hukohuko?
 
Naijua misasa mkuu, ila ajabu sikuwahi kujua hizo namba…. pia sikuwahi kujua kama inatumika kwenye ukuta nilidhani mbao tu.

Elimu haina mwisho.
Sio ukutani TU mkuu hata kwenye miguu yenye mipasuko MIKUBWA aka kenya au machacha
 
Wakuu, tayari zoezi la skimming limeisha vema… sasa nipo kwenye hatua ya rangi.

Naendelea kujifunza bure hapa JF, kwa faida ya wengi.

Sasa naomba kujua kuhusu kitu kinaitwa SILKCOAT, ni kama RANGI ila ni chenga chenga fulani hivi.

Je, inafaa kutumika kwa ukuta mzima nje ndani au ni nakshi ya vipande tu?
 
Back
Top Bottom