Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Kwa jinsi teknolojia inavyokua katika maisha yetu, haiwezekani kumweka mtoto wako mbali na mtandao. Hata ukimzuia muda si mrefu ataingia kwenye ulimwengu huo. Kwa hivyo, ni umri gani unaofaa kumtambulisha mtoto kwa vifaa hivi, na vipi?

Vifaa vya watoto: Subiri mpaka shule ya chekechea
Wataalamu wengi wanapendekeza kusubiri hadi mtoto awe na umri wa miaka miwili. Wanaamini kwamba ni bora kwa mtoto mdogo kutumia muda wake kuchunguza ulimwengu unaomzunguka na kuchezea na vitu halisi ambavyo anaweza kushika na kuhisi. Shughuli za mtandaoni humzuia kufanya hivi, na hivyo kupunguza uzoefu wake wa ulimwengu halisi. Kwa hiyo, unaposubiri kwa muda mrefu, itakuwa bora zaidi kwa mtoto wako.

Dk Carolyn Jaynes, mbunifu wa kujifunza wa Leapfrog Enterprises, anasema, "Hata hivyo, kufikia umri wa miaka mitatu, watoto wengi huwa watumiaji wa mtandao na wanaweza kufaidika na vyombo vya kielektroniki vyenye maudhui ya elimu.

Maudhui haya mara nyingi hutumia mikakati kama vile kurudia jambo, kuwasilisha picha na sauti zinazovutia watu, na kutumia sauti za watoto badala ya watu wazima kwa wahusika. Kuna michezo mingi na shughuli shirikishi kwenye vifaa vya mkononi ambazo si lazima zihusu masomo ya shule lakini bado ni muhimu kwa watoto na zaidi ya burudani."

Simamia matumizi ya kifaa chake
Mtoto lazima achezee na simu au kompyuta akiwa chini ya uangalizi wa wazazi/walezi. Kumsimamia mtoto wako anapotumia vifaa hivi hukupa fursa ya kuunda/kutengeneza uzoefu wake. Mtoto wako anapojaribu programu mpya au anatazama kipindi kwenye TV, unaweza kumuuliza maswali na kuelezea jinsi ya kutumia programu kwa njia bora zaidi, au kuzungumzia kinachoendelea kwenye kipindi. Hii itasaidia kufungua mazungumzo na kukupa wazo la kile anachofikiri na jinsi anavyohisi kuhusu watu na hali

Punguza muda wa kutumia kifaa
Je, ni saa ngapi kuwa na kifaa? Jeannie Galindo, msimamizi wa teknolojia ya kufundishia Manatee County School District, Manatee huko Florida, anasema, "Ningependekeza isizidi nusu saa mtandaoni kwa mtoto wa miaka minne hadi mitano, si zaidi ya saa moja mtandaoni kwa mwenye umri wa miaka sita hadi saba." Lakini kadiri mtoto wako anavyokua, unaweza kumruhusu kutumia wakati mwingi na vifaa. Japokua, kumbuka kuwa kusoma vitabu na kuvinjari nje ya nyumba pia ni muhimu kwa ukuaji wake wa jumla.

Chagua maudhui yanayofaa
Simu au kompyuta humsaidia mtoto kuunganishwa na ulimwengu na kumpa fursa za kujifunza mambo mbalimbali. Michezo ya kumbukumbu, mafumbo, kuchora na programu za muziki, n.k, kunaboresha ujuzi wake wa kufikiri na ubunifu. Kwa hivyo, ni muhimu kwako kujua tofauti kati ya maudhui ya elimu na burudani. Kumbuka, uzoefu wenye thamani unategemea maudhui ambayo mtoto wako anaoneshwa.

Madhara mabaya ya vifaa vya mtandao kwa watoto

~ Matumizi yaliopitiliza ya mtandao yanaweza kudhuru afya ya akili na kimwili ya mtoto wako.

~ Watoto ambao wanajishughulisha na vifaa hata wakati wa kucheza hawawezi kupata kiasi kinachohitajika cha shughuli za kimwili zinazohitajika kwa umri wao. Hii inaweza kusababisha matatizo ya afya kama vile uzito mkubwa.

~ Imeonekana kwamba watoto wanaotumia muda wao mwingi kwenye vifaa mara nyingi huwa na tabia ya fujo.

~ Kuwa muda mrefu kwenye skrini kunaweza kusababisha kutoona vizuri kwa watoto.

~ Matumizi kupita kiasi ya vifaa huwafanya watoto kukosa muunganiko wa wakati halisi wa kibinadamu.

Kuingiza teknolojia katika maisha ya kila siku ya mtoto wako kwa njia sahihi kunaweza kumpa manufaa makubwa. Inaweza kubadilisha jinsi anavyofikiri, kujifunza, kuelewa, na kuingiliana na mazingira yake.

Parent Circle
 
Back
Top Bottom