Je, Ni sahihi kusema watumishi walio masomoni ni hewa?

bomouwa

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
1,149
798
Habari wanajamvi?

Ni jambo la kusikitisha sana hasa ukiwa mwadilifu katika kazi kwa kuzingatia kiapo cha uaminifu na uzalendo kwa nchi yako.

Kuna mtu yeye yupo idara ya serikali (ofcourse ni nyeti) sasa katika idara yao wao kuna ngazi ambazo idara inasomesha isipokua BACHELOR DEGREE tu.

Watu wengi katika hii idara hua wanajisomesha kwa hela zao mfukoni bila kupata hata senti 1 kutoka serikalini.Napongeza sana zoezi la kuwatoa watumishi hewa lakini hapa naomba nikosoe.

Kwamujibu wa sheria za utumishi wa umma,zinamtaka mtumishi aende kusoma "kama atakua ndani ya mpango wa mafunzo" na kama hayupo katika mpango wa mafunzo bsi anapaswa aandike barua wa katibu mkuu kuomba likizo a bila malipo.

Huyu ndugu aliomba ruhusa na immediate bosses wake wakaipitisha na baadae ruhusa ikadelay sasa akaamua kwenda kusoma huku akitumia ruhusa ya immediate bosses na ikumbukwe alikua akitumia hela ya mfuko na kwake.

Miezi kadhaa nyuma amepandishwa cheo ilhali yupo chuo na juzijuzi akasimamishiwa mshahara kwa tuhuma kwamba ni mtumishi hewa.

Suala hili nlipoambiwa nimejiuliza haya.

1. Kwanini serikali haioni mtumishi huyu amewapunguzia gharama kwa kiasi kikubwa maana anajisomesha kwa hela yake?

2. Kama mtumishi aliandika barua ya ruhusa na hakujibiwa ni kosa la mtumishi au kosa la ofisi ya utumishi?

3. Agizo la rais kuhusu watumishi hewa limekua misunderstood?

MY TAKE
Ifike wakati mambo yafanyike kitaalamu maana kama immediate boss amepitisha ili mkuu aruhusu hizi bureaucracy zitasababisha kutia hatiani watumishi wenye moyo na ari ya kazi ikizingatiwa ujuzi wanaoongeza ni katika fani zao husika na ucheleweshwaji wa ruhusa itoshe kusema hata ofisi ya utumishi ni "hewa".

Namsikitikia sana ndugu yangu maana kajitoa kwa ajili ya taifa ila taifa limejitoa na kumkacha.

JE, UNALOLOTE?
 
Ruhusa yake ni kwenda masomoni kwa likizo bila malipo... Amepandaje cheo na mshahara wakati umesitishwa
 
RUHUSA YAKE NI KWENDA MASOMONI KWA LIKIZO BILA MALIPO... AMEPANDAJE CHEO NA MSHAHARA WAKATI UMESITISHWA
Yani barua aliandika hakujibiwa na alikua anapata mshahara mpaka walipomsitishia mwezi may.
 
kisheria huwezi kwenda kusoma bila kupata ruhusa ya mkuu wa shirika, taasisi au katibu mkuu wa wizara la sivyo yatakuwa ni maamuzi yako mwenyewe
 
amesimamishwa mshahara au amefukuzwa kazi???kama amesimamishwa mshahara maana yake taratibu za nidhamu zinaendelea maelezo yote ayatunze ataenda kuyatoa huko ikumbukwe kuwa hakuna atakaye onewa kama mtu atatolewa kimakosa basi atarudishwa kwa mujibu wa Rais so hasiwe na wasiwasi tatizo lilikuwa kubwa mnooo kuliko tunavyozani na katika msafara wa mamba na kenge hawakosi
 
Ngongongare "gate"? Rudi kama ni double rodger ova.
 
"Mpka walipomsitishia mshahara wa mwezi May" hiv kumbe mishahara ya mwez huu wa tano imetoka?
 
unaenda masomoni na mashahara unabeba na bado unapanda cheo...

hii nayo inahitaji digrii kweli kujua ni ufisadi huuu..

only in tanzania.. yaani mtu anapanda cheo wakati hata ofisini hayupo... hiyo performance yake wameionaje na hayo majukum ya cheo kipya anayafanyaje??
 
Yani barua aliandika hakujibiwa na alikua anapata mshahara mpaka walipomsitishia mwezi may.
Huyu ni mtumishi hewa kwa sababu alijiondoa kazini mwenyewe baada ya kuondoka bila kibali cha mwajiri. Baada ya muda uliopangwa kisheria kutoonekana kazini alikuwa tayari amejifukuzisha. Kama alikuwa anapikea mshahara ni makosa na yeye ni sahihi kuitwa mtumishi hewa. Kwa salary slip ilikuwa inaenda kwa mwajiri kila mwezi, huyo mwajiri ni jipu la kutumbua.
 
Habari wanajamvi?

Ni jambo la kusikitisha sana hasa ukiwa mwadilifu katika kazi kwa kuzingatia kiapo cha uaminifu na uzalendo kwa nchi yako.

Kuna mtu yeye yupo idara ya serikali (ofcourse ni nyeti) sasa katika idara yao wao kuna ngazi ambazo idara inasomesha isipokua BACHELOR DEGREE tu.

Watu wengi katika hii idara hua wanajisomesha kwa hela zao mfukoni bila kupata hata senti 1 kutoka serikalini.Napongeza sana zoezi la kuwatoa watumishi hewa lakini hapa naomba nikosoe.

Kwamujibu wa sheria za utumishi wa umma,zinamtaka mtumishi aende kusoma "kama atakua ndani ya mpango wa mafunzo" na kama hayupo katika mpango wa mafunzo bsi anapaswa aandike barua wa katibu mkuu kuomba likizo a bila malipo.

Huyu ndugu aliomba ruhusa na immediate bosses wake wakaipitisha na baadae ruhusa ikadelay sasa akaamua kwenda kusoma huku akitumia ruhusa ya immediate bosses na ikumbukwe alikua akitumia hela ya mfuko na kwake.

Miezi kadhaa nyuma amepandishwa cheo ilhali yupo chuo na juzijuzi akasimamishiwa mshahara kwa tuhuma kwamba ni mtumishi hewa.

Suala hili nlipoambiwa nimejiuliza haya.

1. Kwanini serikali haioni mtumishi huyu amewapunguzia gharama kwa kiasi kikubwa maana anajisomesha kwa hela yake?

2. Kama mtumishi aliandika barua ya ruhusa na hakujibiwa ni kosa la mtumishi au kosa la ofisi ya utumishi?

3. Agizo la rais kuhusu watumishi hewa limekua misunderstood?

MY TAKE
Ifike wakati mambo yafanyike kitaalamu maana kama immediate boss amepitisha ili mkuu aruhusu hizi bureaucracy zitasababisha kutia hatiani watumishi wenye moyo na ari ya kazi ikizingatiwa ujuzi wanaoongeza ni katika fani zao husika na ucheleweshwaji wa ruhusa itoshe kusema hata ofisi ya utumishi ni "hewa".

Namsikitikia sana ndugu yangu maana kajitoa kwa ajili ya taifa ila taifa limejitoa na kumkacha.

JE, UNALOLOTE?
Huyo jamaa alijifukuza kazi mwenyewe baada ya kutofika kazini siku 5 mfululizo. Hiyo ni sheria ya utumishi wa umma. Kwa kumlipa mshahara ilikuwa ni HEWA. Anayetoa kibali cha kuondoka kazini ni MWAJIRI na wala si mkuu wa idara. Una la ziada?
 
Aliomba likizo bila malipo halafu akawa analipwa! Akawa anazichukuwa halafu wewe huoni kuwa ni mtumishi hewa. Ajabu!
 
Hii kali. Kuna ndugu yangu yeye pia kaenda kusoma wamemwita mtumishi hewa. Ila yeye alipewa barua ya masharti kutoka kwa mkurugenzi, na akayatimiza. Baadae amekuja mkurugenzi mwingine akatengua wakati mpaka mkataba wa kwenda masomoni mwanasheria kasaini. Sasa pia wanasema ni mtumishi hewa. Ila mshahara wake ulikuwa unakuja yani salary slip lkni bank hakuna mshahara. Kawafungulia kesi ipo CMA, iko kwenye hatua ya abtration, na pingamizi la mwajiri kuwa ni mtoro lilipigwa chini na kesi inasikilizwa. Pole sana ndugu
 
unaenda masomoni na mashahara unabeba na bado unapanda cheo...

hii nayo inahitaji digrii kweli kujua ni ufisadi huuu..

only in tanzania.. yaani mtu anapanda cheo wakati hata ofisini hayupo... hiyo performance yake wameionaje na hayo majukum ya cheo kipya anayafanyaje??
mkuu bila shaka hujawahi kufanya kazi serikalini
 
Kwa isheria za utumishi huyo ni mtoro. Barua ya maombi iliyopitishwa na Bosi wake siyo kibali cha kwenda kusoma. Yeye alitakiwa apambane hadi bosi mwenye mamlaka ya kuruhusu mtumishi kwenda masomoni aijibu barua yake kuwa amekubali huyo bwana aende masomoni ndiyo angeondoka kwenda huko masomoni. Watumishi wengi wa umma walioruhusiwa rasmi na mamlaka husika kwenda masomoni (Nawafahamu wengi tu) wanaendelea kupiga kitabu tu bila zengwe.
 
Habari wanajamvi?

Ni jambo la kusikitisha sana hasa ukiwa mwadilifu katika kazi kwa kuzingatia kiapo cha uaminifu na uzalendo kwa nchi yako.

Kuna mtu yeye yupo idara ya serikali (ofcourse ni nyeti) sasa katika idara yao wao kuna ngazi ambazo idara inasomesha isipokua BACHELOR DEGREE tu.

Watu wengi katika hii idara hua wanajisomesha kwa hela zao mfukoni bila kupata hata senti 1 kutoka serikalini.Napongeza sana zoezi la kuwatoa watumishi hewa lakini hapa naomba nikosoe.

Kwamujibu wa sheria za utumishi wa umma,zinamtaka mtumishi aende kusoma "kama atakua ndani ya mpango wa mafunzo" na kama hayupo katika mpango wa mafunzo bsi anapaswa aandike barua wa katibu mkuu kuomba likizo a bila malipo.

Huyu ndugu aliomba ruhusa na immediate bosses wake wakaipitisha na baadae ruhusa ikadelay sasa akaamua kwenda kusoma huku akitumia ruhusa ya immediate bosses na ikumbukwe alikua akitumia hela ya mfuko na kwake.

Miezi kadhaa nyuma amepandishwa cheo ilhali yupo chuo na juzijuzi akasimamishiwa mshahara kwa tuhuma kwamba ni mtumishi hewa.

Suala hili nlipoambiwa nimejiuliza haya.

1. Kwanini serikali haioni mtumishi huyu amewapunguzia gharama kwa kiasi kikubwa maana anajisomesha kwa hela yake?

2. Kama mtumishi aliandika barua ya ruhusa na hakujibiwa ni kosa la mtumishi au kosa la ofisi ya utumishi?

3. Agizo la rais kuhusu watumishi hewa limekua misunderstood?

MY TAKE
Ifike wakati mambo yafanyike kitaalamu maana kama immediate boss amepitisha ili mkuu aruhusu hizi bureaucracy zitasababisha kutia hatiani watumishi wenye moyo na ari ya kazi ikizingatiwa ujuzi wanaoongeza ni katika fani zao husika na ucheleweshwaji wa ruhusa itoshe kusema hata ofisi ya utumishi ni "hewa".

Namsikitikia sana ndugu yangu maana kajitoa kwa ajili ya taifa ila taifa limejitoa na kumkacha.

JE, UNALOLOTE?
It is very bad. Ila kiutumishi huyu bwana/ bibib alikuwa hajaruhusiwa. nadhani wafanyakazi warudi kwenye mstari. Inaeleweka vijana hutaka mabo kwa haraka lakini kama hujaruhusiwa rasmi kamwe usinyanyue mguu kuondoka kutoka kwenye kitui=o cha kazi. ( of course hapa mambo ya utumishi kitaratibu yaangaliwe lakini hilo ni onyo na fundisho, poe ake mambo yatarekebishwa naamini.)
 
Huo ni ukuda tu kwa baadhi ya mabosi. Inawezekana jamaa anaenda kufanya master ambayo boss wake hana..!!! Ni roho mbaya tena zenye umasikini.
 
Kwa isheria za utumishi huyo ni mtoro. Barua ya maombi iliyopitishwa na Bosi wake siyo kibali cha kwenda kusoma. Yeye alitakiwa apambane hadi bosi mwenye mamlaka ya kuruhusu mtumishi kwenda masomoni aijibu barua yake kuwa amekubali huyo bwana aende masomoni ndiyo angeondoka kwenda huko masomoni. Watumishi wengi wa umma walioruhusiwa rasmi na mamlaka husika kwenda masomoni (Nawafahamu wengi tu) wanaendelea kupiga kitabu tu bila zengwe.
Hv ni mtoro ama hewa?
 
Back
Top Bottom