Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,719
- 215,830
Habari za leo Alhamis wakuu,
Shost huyu si shost mpya ni yule shost yangu tunaefanya nae jogging, nimemfahamu mwaka wa pili huu, pamoja na hayo nilipo waona watoto wake wana weupe si wa kwetu wa kibantu, lakini kuogopa kuonekana mbea nilikaa kimya. Tulivyokwenda kwenye Christmas Do ya office ndiyo nilimuona mume wake ni 0.5.
Tulivyo mashost, story za kila siku ndiyo nimekuja kufahamu kuwa, bwana shemeji baba yao ni raia wa Switzerland aliyekuja kufanya kazi kwa mkataba Tanzania, alikuwa kwenye mahusiano na mama wa ki-Tanzania na kupata watoto wawili, baba yule baada ya mkataba wake kwisha aliondoka bila kuonyesha nia yeyote ya kuwasidia wale watoto.
Mama alijitahidi kuwalea, watoto walipokuwa na miaka 10 na mwingine 7, mama aliaga dunia, watoto wale ilikuwa wapelekwe kwenye kituo cha kulele watoto yatima. Mama mmoja alijitolea kuwalea, mama huyo ndiye mama washost yangu.
Shost ananiambia waliazna mapenzi ndani ya nyumba, kijana alimaliza chuo na alipata kazi hivyo alishahama nyumbani lakini bado ni sehemu ya familia. Shost amekaa nyumbani anaanza kutapika, dada yake mkubwa kumuuliza ndiyo wanagundua shost ana kimimba.
Ilibidi dada amuweke chini amuulize mimba ni ya nani, alimtaja mhusika, ujumbe ulitumwa , alifika kwenye kikao, kuulizwa alikubali na alisema yuko tayari kuoa na harusi ilifungwa shost akiwa na mimba ya miezi mitano.
Wanaishi kama marafiki wakubwa kwa kweli, mpaka ninaona raha, shost ananiambia amemfahamu huyu mwanaume tangia akiwa na miaka mitano jamaa akiwa na miaka 10. Lakini nimebaki kujiuliza mtu uliekuwa nae nyumba moja na aliasiliwa kama mtoto wa familia unaweza kufunga nae ndoa?