Je, ni sahihi kumpiga mfiwa anaposumbua msibani?

Kapigwa naamini waliompiga wanajua kwanini walimpiga na kumtoa mzobe mzobe!
Yawezekana alikuwa kishajitwika mizigo ya pombe kichwani!
Misibani kunakuwaga na drama SANA, sijajua kwanini shetani huwa kama kajiinua!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Siyo sawa, nilipoteza dogo wangu mmoja nnampenda sana, ikatokea rafiki yake akawa analia sana msibani, mara ang'oe maua ya msalaba, mara apige kelele, kuna jamaa walikuwa wanataka kumzingua wazee wakasema muelekezeni asiharibu vitu kisha mumuache aomboleze kwa namna yake, huyu mtoto wa kiume akitaka pombe mpeni, hakika hamjui ni nini kimemkumba...

Ila wanawake wananifurahisha sana kwenye msiba hata kama nimefiwa, unakuta mtu mko naye kwenye gari mnacheka ghafla mmefika kwenye msiba, kilio chake ni balaaa, dk 2 anacheka akija mwingine akilia analianzisha...drama!
 
Back
Top Bottom