Je, ni sahihi kumgombeza mtu mbele ya mke/mme wake?

MusuKuma

Member
Jan 30, 2021
33
87
Wana jamvi habri zenu,

Mwenzenu nimeoa Mimi ni kifunga mimba kwahiyo Niko na Kaka zangu. Kuna Kaka yangu mmoja huwa ni afisa wa usalama kwahiyo kulingana nawao walivyo anaweza kukupigia simu anytime nakuanza kukugombeza haijarishi ni kitu kidogo au kikubwa, nimekuwa hivi kwa mda mrefu mwishowe nikaona huu ni upuuzi yaani maisha yangu harafu watu wawe wananigombeza au kunikejeri mbele ya mkewangu au akiwa anasikia.. kiukweli Mimi ni mtu nisiyependa maneno sipendagi kuongea sana. Sasa nimeanza kuwa mkali make naona nidhamu yangu kwakila mtu inaleta ukakasi kwenye nyumba yangu.

Nimeanza kubadirika Sana iwe mzazi akionekana kunigombeza Kama ni Jambo halina mashiko nakata simu Kisha nampigia baadae au anaongea Mimi siongee naitikia tu

Sasa watu walionizoea kuwa munyenyekevu kwao baada ya kuanza kuwa mkali wameanza kusema kuwa nimepata hela ooh nimeanza kuwa na kiburi oooh masikini akipata yaani maneno mengi kedekede.

Hebu tushauriane hivi vitu kama hivi vya kugombezwa kwenye simu na ndugu zako wao wapo na wake zao mda huo wanasikia unagombezwa na wewe na mkewako anasikia je ukikaidi utaonekana wewe sio?

Je, ufanye je kuishi na ndg wa dizaini hii au majirani?
 
Kama ni kwenye simu wanajuaje kuwa upo karibu na mke wako?

Kuna simu ukipigiwa unajua huyu kichaa unasogea mbali na watu maana watu wa hivyo unakuta unapokea tu ye ashakuambia "we karunguyeye unapumua tu" hapo yanaanza matusi tu.

Mkuu si vizuri kugombezwa mbele ya mtu wako.
 
Ndugu zako nao wamezidi me ukija juu haki ya nani nakugeuzia kibao huto amini yaani mgombeza unageauka mgombezwa
 
Mtu anaejielewa hawezi kukutokea mbele ya mkeo hata kama ni mzazi wako
 
Haya uliyoongea hapa mwambie na yeye.

Unajua kuna muda kaka zetu kwa vile alikulea udogoni alikuwa anakufulia na uniform, basi anataka akufanye mtoto daima.

Anaanza kukuamrisha hata mbele za watoto wako.
 
Back
Top Bottom