Je, ni nini kinachosababisha utasa na tiba yake ni ipi?

lwambof07

JF-Expert Member
Jul 12, 2016
4,593
5,203
Kutoweza kupata mtoto ni chanzo cha unyanyasaji wa kijamii na nyumbani kwa wanandoa nchini Bangladesh, bila kujali sababu ya kasoro za kuzaliwa au ugonjwa wowote, bila kujali masuala ya jinsia au jinsia.

Waathiriwa zaidi ni wanawake. Ingawa mara nyingi wanaume wana shida.

Mohammad Abul Kalam, 55, wa Kishoreganj, wakati fulani alijua kwamba yeye na mke wake walikuwa na matatizo katika kupata watoto.

Lakini hata hivyo mke wake alilazimika kuvumilia mateso hayo. Abul Kalam alikuwa akizungumzia jinsi kutoweza kupata watoto kulivyosababisha yeye na mke wake kufadhaika kiakili.

"Kijamii hakuna aliyeniambia chochote zaidi ya mke wangu. Hasa wazazi wangu. Alikuwa anaumwa wakati huo. Najua nimepungukiwa na nguvu za kume kwa sababu daktari aliniambia hilo."

Mwandishi wa BBC alitembelea kliniki moja mjini Dhaka ambako alikutana na mwanamke aliyejawa na msongo wa mawazo jioni moja. Kulikuwa na wanandoa kadhaa waliokuwa wakisubiri kumuona daktari.

Wamekuja kutoka Dhaka na wilaya zingine nchini. Wengi wao wako katika miaka yao ya thalathini au zaidi.

Mwanamke huyu anayetokea eneo la Baufal huko Patuakhali walikuwa amekaa nyuma yawatu wote. Mwanzoni alisita kuzungumza.

Lakini wakati mmoja, alisema kuwa hana uwezo wa kupata mtoto, mume wake huenda akao mke mwingine. Baada ya kusikia minong'ono kutoka kwa wakwe zake, aliamua kuja Dhaka kutafuta tibaakisaidiwa na jamaa zake.

Akielezea changamoto anazopitia katika familia kwa kukosa mtoto, anasema, "Nimeolewa kwa miaka minane. Nimeambiwa umeolewa kwa miaka mingi lakini hujapata watoto.

Tatizo ni nini? Kwanini huwezi kumzalia watoto mume wako, ambaye ana mali nyingi?" Utakula peke yako? Nakabiliana na maswali ya aina hiyo kila siku.

Baba yake mume wake amesema atamuoza mwanawe mke mwingine. Kwani hujali kuwa huna watoto? Ndio maaana nimeamua kuja Dhaka Mungu akinijaalia nipate mtoto. "

Nchini Bangladesh, wanawake hunyanyaswa sana kutokana na utasa.

Mwanamke huyo alisema amekuwa chini ya shinikizo tangu mwaka wake wa pili wa ndoa. Hatimaye, alitafuta msaada wa daktari ili kudumisha familia yake.

Lakini utasa unaweza kuwakumba wanaume na wanawake. Madaktari wanasema idadi ya wanaume na wanawake wasioweza kushika mimba ni sawa.

Hata hivyo, nchini Bangladesh, wanawake wana uwezekano mkubwa wa kuwa waathirika wa unyanyasaji wa nyumbani na kijamii.

Kuna matibabu mbalimbali ya utasa nchini Bangladesh sasa. Hata hivyo, ni ya muda mrefu, ya gharama kubwa na ngumu.

Sababu za utasa kwa wanawake

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema mtu yeyote ambaye atashindwa kushika mimba baada ya mwaka mmoja wa kujaribu kushika mimba anahesabiwa kuwa hana uwezo wa kuzaa.

Asilimia kamili ya wanandoa wanaosumbuliwa na utasa nchini Bangladesh haijulikani.

Kulinagana na Dkt. Selina Akhter sababu zinazofanya wanawake washindwe kupata watoto ni hizi:

Makovu katika mirija yake ya uzazi au kwa tumbo lake. Makovu haya yanaweza kuzuia yai kupita kwenye mrija, au mbegu kufikia yai.

Mwili wake hautengenezi yai. Hii ni kwa sababu labda mwili wake hauna kiwango tosha cha homoni inayohitajika kwa wakati ufaao.

Vimelea tumboni (fibroids). Vimelea hivi vinaweza kuzuia kushika mimba, au kumfanya mwanamke asiweze kubeba mimba.

Njia za kupanga uzazi pia hulaumiwa kwa shida za utasa. Lakini mbinu za kupanga uzazi (isipokuwa sterilisation), hazisababishi utasa, isipokuwa wakati fulani ambapo IUD haijawekwa vizuri na kusababisha maambukizi kwenye tumbo au mirija.

Kuna magonjwa mengine, kama vile: cyst ya chokoleti ya ovari, ambayo inaweza kuwa kutokana na endometriosis.

Na magonjwa ya zinaa huharibu viungo vya uzazi vya mwanamke. Ndiyo maana utasa unaweza kutokea.

Sababu za utasa kwa wanaume

Fazal Nasser, profesa mshiriki katika Taasisi ya Kitaifa ya Figo na hospitali, anasema uzoefu wao ni kwamba wanaume huenda kwa daktari wakiwa wamechelewa sana kwa matatizo ya ugumba.

Kwa sababu ikiwa hakuna mtoto, mke ndio hukimbilia kwa daktari mwanzoni.

Lakini ni nini sababu kuu za ugumba kwa wanaume?

Ukosefu wa homoni za kiume za kutosha mwilini:Testosterone ni homoni za kiume zinazowafanya wanaume kuhisi kuwa wanaume huku estrogen zikiwa homoni za kike ambazo humsaidia mwanamke kupata ujauzito.

Msongo wa mawazo:Shinikizo la kiakili ni miongoni mwa sababu kuu zinazosababisha ugumba miongoni kwa wanaume. Msongo wa mawazo unaweza kutokea iwapo mwanaume hana kazi, iwapo mwanaume hana fedha ama iwapo kuna changamoto katika ndoa yake ama kutoka kokote kule.

Kushiriki mazoezi mbali na tendo la ndoa mara kwa mara: Hili ni suala linalohitaji msisitizo ili kuzuia ugumba. Mtu anapaswa kujifunza kufanya mazoezi kwa muda mfupi kila siku.

Unyanyasaji wa kingono:Wanaume kushiriki katika tendo la ndoa mara 21 kwa mwezi. Inadaiwa kwamba kushiriki katika tendo la ndoa mara kwa mara kunasaidia kuzuia saratani ya tezi dume.

Ukosefu wa maji safi: Suala hili linaonekana kama la kushangaza kwa watu wengi, kulingana na wataalamu. Hata hivyo ukosefu wa maji safi , ambayo hayana virutubisho , huathiri afya ya uzazi ya wanaume.
download (1).jpg
download (2).jpg
download (3).jpg
 
Back
Top Bottom