Je, ni nani anayewadanganya wananchi?

Je, ni nani anayewadanganya wananchi?

franci45

Member
Joined
Nov 8, 2023
Posts
61
Reaction score
93
Kuna jambo linahitaji kutazamwa kwa jicho la tatu. Mara kwa mara tumekuwa tukisikia baadhi ya viongozi wakisisitiza kuwa Watanzania waliopo nje ya nchi au wanaokosoa mwenendo wa serikali wanatumika na “mabeberu.” Kauli hizi zimekuwa zikitumika kama njia ya kuzima hoja badala ya kujibu hoja zenyewe.

Lakini tukijiuliza kwa undani: Je, kila anayekosoa ni adui wa taifa? Au ni raia anayejali mustakabali wa nchi yake?

Vilevile, viongozi hawa hawa wanapozungumza juu ya “kutunza amani” kwa kuwatisha wananchi kwamba machafuko yakitokea hawatakuwa na pa kukimbilia, ni muhimu kujiuliza ukweli uliopo nyuma ya pazia. Wananchi wa kawaida hawana njia mbadala lakini je, viongozi wenyewe hawana access ya kusafiri muda wowote? Wengine wana pasipoti za nchi nyingine, mali nje ya nchi, na fedha kwenye mabenki ya kimataifa.

Mfano wa wazi ni Andry Rajoelina ambaye alishawahi kuhusishwa na uwekezaji na maisha ya nje ya nchi wakati wa uongozi wake. Hili linaonyesha kuwa hali hii si ya Tanzania pekee.

Swali la msingi linabaki: Je, ni haki kwa viongozi kuwaambia wananchi wabaki watulivu kwa gharama yoyote, huku wao wakiwa na “plan B” za maisha nje ya nchi?

Nchi haiwezi kujengwa kwa hofu, bali kwa uwazi, uwajibikaji, na kuheshimu maoni tofauti. Kukosoa si uhaini ni sehemu ya demokrasia.

Wananchi wanapaswa kupewa nafasi ya kuuliza, kujadili, na kushiriki kikamilifu bila kuwekewa lebo au vitisho. Amani ya kweli inatokana na haki, si ukimya wa kulazimishwa
 
hakuna haja ya kubabaika na vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi, pamoja na mamaluki wao malofa mno humu nchini.

Nchi yetu inaheshimu sana uhuru wa maoni ya watu wake wote, iwe wa nje au ndani ya nchi,
lakini kamwe, haitavumilia uropokaji wa vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi unaokiuka sheria kwa makusudi na unaolenga kuchochea fujo, vurugu na uvunjifu wa amani miongoni mwa waTanzania.

Na kama wewe ni moja ya miongoni mwa vibaraka au maluki wao malofa, tafadhali achana na hiyo nonsense mara moja.
 
hakuna haja ya kubabaika na chawa!
 
Kuna jambo linahitaji kutazamwa kwa jicho la tatu. Mara kwa mara tumekuwa tukisikia baadhi ya viongozi wakisisitiza kuwa Watanzania waliopo nje ya nchi au wanaokosoa mwenendo wa serikali wanatumika na “mabeberu.” Kauli hizi zimekuwa zikitumika kama njia ya kuzima hoja badala ya kujibu hoja zenyewe.

Lakini tukijiuliza kwa undani: Je, kila anayekosoa ni adui wa taifa? Au ni raia anayejali mustakabali wa nchi yake?

Vilevile, viongozi hawa hawa wanapozungumza juu ya “kutunza amani” kwa kuwatisha wananchi kwamba machafuko yakitokea hawatakuwa na pa kukimbilia, ni muhimu kujiuliza ukweli uliopo nyuma ya pazia. Wananchi wa kawaida hawana njia mbadala lakini je, viongozi wenyewe hawana access ya kusafiri muda wowote? Wengine wana pasipoti za nchi nyingine, mali nje ya nchi, na fedha kwenye mabenki ya kimataifa.

Mfano wa wazi ni Andry Rajoelina ambaye alishawahi kuhusishwa na uwekezaji na maisha ya nje ya nchi wakati wa uongozi wake. Hili linaonyesha kuwa hali hii si ya Tanzania pekee.

Swali la msingi linabaki: Je, ni haki kwa viongozi kuwaambia wananchi wabaki watulivu kwa gharama yoyote, huku wao wakiwa na “plan B” za maisha nje ya nchi?

Nchi haiwezi kujengwa kwa hofu, bali kwa uwazi, uwajibikaji, na kuheshimu maoni tofauti. Kukosoa si uhaini ni sehemu ya demokrasia.

Wananchi wanapaswa kupewa nafasi ya kuuliza, kujadili, na kushiriki kikamilifu bila kuwekewa lebo au vitisho. Amani ya kweli inatokana na haki, si ukimya wa kulazimishwa
Ni chukua chako mapema na chawa wao!9
 
Back
Top Bottom