je ni mwanamke au mwanaume?

Iron Lady

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2008
Posts
4,071
Reaction score
1,381
hivi ukiwa unawasiliana na mtu katika hali ambayo huwezi kumuona ama kumsikia nini kitakutambulisha kuwa huyu mtu unayewasiliana nae ni mwanamke au mwanaume.

lugha- je ni maneno gani hupenda kutumiwa na mwanamke au mwanaume.

ikiwa huwasiliani nae matendo gani yatakufanya ujue huyu ni mwanamke au mwanaume?

nisaidieni wanajamvi.
 
mfn wanawake wengi hupenda kutumia maneno kama jamani, yani, sasa si rahisi kukuta mwanaume anatumia maneno kama haya kama unawasiliana na mtu humuoni na akawa anaongea sana maneno ya namna hii mimi nitajua kuwa huyo ni mwanamke.
mambo mengine ni yapi yatakayosaidia kutambu jinsia kwa urahisi?
 

Uzuri wa mwandiko, kama wa Preta. . .unajua huyu bila shaka ni KE.
 

Wengine wako smart hata kwenye kuandika wanachagua maneno. Mfano ni mimi mwenyewe! Je unaweza kabashiri kama ni KE au ME? Vinginevyo labda uangalie jina maana majina mengi humu JF yanaonyesha jinsia wazi wazii!
 
Jaman anataka kujua u never no labda yamemkuta.....

Iron lady ni kweli kuna maneno wanawake wanapenda kuyatumia, kwa mfano karembo ni ke, ameanza na jamani moja kwa moja.
 
Iron lady ni kweli kuna maneno wanawake wanapenda kuyatumia, kwa mfano karembo ni ke, ameanza na jamani moja kwa moja.


kuna wanawake wengine wanapenda sana kusema ai wewe
 
ukiona mtu anatukana sana utajua tu huyu ni mwanaume wanawake ni nadra sana kutukana tukana.
 
Wengine wako smart hata kwenye kuandika wanachagua maneno. Mfano ni mimi mwenyewe! Je unaweza kabashiri kama ni KE au ME? Vinginevyo labda uangalie jina maana majina mengi humu JF yanaonyesha jinsia wazi wazii!

kwa sababu wanakuwa na sababu ya kuigiza hivyo wanavyoigiza lakini mbali na kuigiza yapo mameno ambayo wanawake huyapenda na namna wanavyoyatumia unajua kabisa ni mwanamke huyu au huyu ni mwanaume.
maneno kama oya ee bwana ee huyu ni mwanaume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…