Je ni marafiki au wapambe nuksi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni marafiki au wapambe nuksi?

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Nazjaz, Dec 4, 2011.

 1. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  Siku za nyuma niliajiriwa na benki moja ya biashara hapa mjini nikiwa idara ya mikopo. Thanks God, vijisenti vya kutumia vikawa havinipigi chenga. Nikapata marafiki kedekede, wake, waume, watoto na hata wazee.

  Ikatokea bahati mbaya, nikapata matatizo kazini, marafiki wote wakakimbia. Hata nikiwapigia simu kuna ambao walikuwa hawapokei kabisa simu zangu, nabaadhi wakipokea walikuwa wanasema , ngoja kidogo ntakuigia, na wasipige tena.
  Sasa nafanya kazi shirika moja la UN, ninaishi nyumba nzuri, nina gari zuri..... Yaani Mungu amenifungulia milango.
  Marafiki wa zamani ndio wanajidai kunipia, na kuniomba tukutane.
  Nikikomenti chochote kwenye FB, wanashadadia kwa nguvu zote.
  Kila commenty yangu ina pambwa na like kibao.
  Jamani wana JF wenzangu, jifunzeni namna ya kutafuta marafiki bora, na si bora marafiki.
   
 2. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Dada, sio king'aacho ni dhahabu. Vingine ni bosheni tu. Hao marafiki ni wa kuwaogopa kama ukoma. Fanya urafiki na ibada nawe utaona nguvu za muumba wako.
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hahaha..kazi ya UN sio? ndio ile ya u-Line Manager??

  Tupo pamoja
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mkono mtupu haulambwi
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  hapendwi mtu mpaka awe na kitu dada. Kwa hiyo hapo akili kichwani mwako
   
 6. Tumaini Jipya

  Tumaini Jipya JF-Expert Member

  #6
  Dec 5, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0


  Ha ha ha ha ha,Yaani Nazjaz umezungumza katika Mawazo yangu Mkuu!! Niliwahi kuajiriwa Airtel,nilikuwa na wallet nene,nikawa na wanaoitwa marafiki kedekede,nilitoka Airtel mwaka jana mwezi wa sita ili kujiajiri,mambo hayakuniendea Vizuri nimeyumba sana!!

  Sasa hivi ndiyo naanza kujikusanya adoado,"Marafiki" wote walinikimbia,hawataki kusikia kutoka kwangu,waliokaribu yangu ni watu ambao hawakuufaidi Ufalme wangu,how ironic life can be!! "Marafiki" wachache ambao ni wajanja ana-pretend kama anataka kujua unaendeleaje kumbe kimsingi anataka kujua kama Mambo yameanza kukaa sawa,ukitaka kujua kama ni Mnafiki tu mpigie simu the following day HAPOKEI na wala harudishi call yako!!

  Hakuna sababu ya kuumia ndugu yangu,cha msingi hapo ni kujifunza somo kwamba kuna "washkaji"(Acquintances) na marafiki(Friends),wengi wetu huwa tuna Washkaji tu,umesoma nae,unasali naye,jirani yako hiyo tu ndiyo sababu ya Uhusiano wenu,hawa wanapenda tu good time,Kitimoto,Beer,kuwalipia kiingilio mkienda Club,kuja kukukopa na kuomba misaada ya hapa na pale,ukiwa hauna Vitu hivyo they dont see a friend in u!!

  What u nd to do now,ni kuwapotezea moja kwa moja na wasiijue rangi ya wallet yako,maana hicho ndicho wanachokihitaji,wati wa Tumbo na mambo yake!!
  Stay away frm them,spend ur time with people ambao walikuwa upande wako hata wakati ambao ulikuwa "unanuka",Usiruhusu Upweke ukurudishe kwa hao kenge maana huwa Wazuri katika mazungumzo na since hawana "pride" hawaoni hasara kurudi kupitia mlango wa mbele!!!
   
 7. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2017
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  kawaida
   
 8. Miiku

  Miiku JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2017
  Joined: Oct 8, 2014
  Messages: 3,108
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  2011
   
Loading...