Je ni lini wa-bara wataongoza Zanzibar? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni lini wa-bara wataongoza Zanzibar?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Nov 23, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Wapendwa Wakuu

  Muundo wa uongozi Tanzania unaelekea kuibua maswali mengi. Pamoja na kuwa tumo ndani ya Muungano bado Watanzania Bara hawana nafasi ya Uongozi huko Zanzibar.

  Juzi tumeshuhudia Zanzibar imepata Rais na Makamu wawili wa Rais wote wazanzibar. Je kwanini Wa-bara hakuna hata mmoja huko Zanzibar?

  Lakini: Wazinzabar wanatawala Bara, na kuwatungia sheria Wa bara. Tunaona makamo wa Rais Mzanzibar, wabunge wengi tu Wazanzibar; na Mawaziri kadha kutoka Zanzibar watatangazwa hivi karibuni KUJA KUWAONGOZA WA-BARA. ILIHALI HAKUNA HATA WAZIRI MMOJA WA HUKO ZANZIBAR AMBAYE ANATOKA BARA.

  Je, kama Tanzania ni moja ni lini Wa-Bara watatawala Zanzibar kama wa Zanzibar wanavyotawala Bara?

  Mimi Binafsi napata maswali mengi; ninapoona hakuna hata MBUNGE mmoja Msukuma huko Zanzibar

  Tutarajie nini kwa mfumo huu?

  Nakaribisha maoni Yenu Asanteni.
   
 2. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maswali ni mengi, je Zanzibar wanachangia kwa uwiano uliosawa bajeti ya muungano au Tanzania bara ndio wanawabeba tu wazanzibar?. Kama ni hivyo kwa nini wawabebe wakati ni nchi inayojitawala? Ingekuwa mkoa wa Tanzania bara sawa, lakini ni nchi inayojitegemea hivyo sijui kama kuna usawa katika kuchangia bajeti ya muungano
   
 3. Nipigie

  Nipigie Senior Member

  #3
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 121
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wenyewe ni wengi mno kutawala , sasa na sisi tukisema tutawale, si zitakuwa ni vurugu. Tukiona wanakosea we are ready kuwakosoa.
   
 4. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2010
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Karata zilizochezwa wakati wa kuunda "Tanzania" zilizaa utata ufuatao: Zanzibar ni nchi ndani ya muungano - Tanzania bara si nchi bali ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyo Zanzibar . Kwa "equation" hii ni wazi wazanzibari wanaweza kuongoza bara kwani ni raia wa 'Zanzibar" na pia ni raia wa "Tanzania". Si rahisi kwa mtanzania kutoka bara kuongoza Zanzibar kwani yeye ni raia wa Tanzania lakini si raia wa Zanzibar!
   
 5. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mathematically

  Muungano =Zanzibar+Bara

  but

  Bara>>>>Zanzibar

  therefore

  Bara{zanzibar} and not Zanzibar{Bara}

  For that reason Bara{zanzibar} will exist and Zanzibar{Bara} will not exist
  "impossible set" or true "Null set"

  However Bara kuiongoza zanzibar is logicless, kwa sababu sehemu ndogo ndio huhitajika kuiongoza sehemu iliyo kubwa and not vise versa. (i.e kikundi kidogo cha watu kitaongoza kundi kubwa na sio kundi kubwa liongoze mtu moja au kikundi kidogo cha watu)

  So,
  Bara will need Zanzibar na Zanzibar will not need Bara. Hence proved

  Japo ni kinyume cha katiba buti kwa maslai fluani fulani ya kichama na kitaifa itaaminika iwe hivyo. But in reality Katiba lazima iheshimiwe.
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Kwa majibu yako ni kuwa sisi Wabara hatuwezi kuwaongoza Wazanzibar?
   
 7. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kama ni hivyo kwa nini kila leo Wazanzibari hawaachi kulalamika kuwa wanatawaliwa na Watanganyika ? Hivi sasa wana Raisi wao, Makamu Raisi wawili wao na huku Tanganyika wanaye Makamu wa Raisi. Kwa mahesabu rahisi ni kuwa kati ya viongozi wakuu (maraisi) wanne ndani ya Jamhuri ya Tanzania, watatu wanatoka Zanzibar ! Hii ina maana kwamba kila wakaazi 250,000 huko Zanzibar wanamtoa Raisi wakati huku Tanganyika ni Raisi moja kwa wakazi 40,000,000 ! Talk of the absurdity of it all !!
   
 8. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sina uhakika ila labda uhakika tutaupata katika historia ya uongozi wa Zanzibar kama waliwahi kuwepo wabara. May be wakati wa Nyerere otherwise sidhani kama ipo au itakuwepo tena.
   
 9. M

  Mkubwa Dawa Member

  #9
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 13, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wa Bara hawataongoza Zanzibar kwani hiyo ni nchi inayojitegema kwa kuwa na raisi wake, na hamna nchi kama Tanzania Bara "Tanganyika" ilikwenda na maji na kumezwa na Tanzania wakati wa muungano hivyo sidhani kama itakuwa rahisi kwa Mbara kushika hatamu Zanzibar.
   
 10. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #10
  Nov 23, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Unapotaja Tanzania ni ' Tanganyika na Zanzibar''. Kama ungetumia maneno hayo hoja yako ingeskosa mashiko. Zanzibar ni sehemu ya JMT vinginevyo Zanzibar ni Zanzibar na Tanganyika ni Tanganyika. Unaposema Tanzania tayari umeshaua Tanganyika na Zanzibar. Hakuna nchi inayoitwa Tanzania bila Zanzibar au Tanganyika. Kwahiyo raia wa Tanzania ni wale wa Tanganyika na Zanzibar. Kama Zanzibar ni nchi, Tanganyika imefia wapi? na kama hakuna Tanganyika,Tanzania inatoka wapi?
   
 11. MKANDYA

  MKANDYA Senior Member

  #11
  Nov 23, 2010
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ahsante mtoa hoja!! Wabara kutawala Zanzibar ni mpaka pale tutakapofumbua hili fumbo" Chao ni chao kwa nini?Na chetu ni chao kwa nini? Lakini chao si chetu kwa nini??
   
 12. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #12
  Nov 23, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nadhani it is a question of minority and majority. Zanzibar ni kanchi kadogo sana ikilinganishwa na Tanganyika (Tanzania Bara). Hata idadi ya watu zanzibar haizidi idadi ya watu kwa jiji la DSM. Kutokana na ukweli huo, wazanzibari wanajisikia wamemezwa zaidi kwenye muungano kuliko tunavyojisikia sisi waTZ bara. Sasa, inapotokea mTZ bara anaenda kuongoza zanzibar hali ya kujisikia kumezwa ndiyo inakuwa kubwa zaidi. Hivyo, ndivyo ninavyofikiri kwamba wazee wetu waasisi wa muungano walitaka waepushe manung'uniko miongoni mwa wazanzibari ya kujisikia wamemezwa. Kumbuka hata wazo la kuungana lilitolewa na Nyerere. Hivyo, Mwl. alikwepa kuonekana ana agenda ya kuimeza zanzibar.

  Pamoja na hayo, kama kutakuwa na 'national dialogue' ya kuwa na katiba mpya, itakuwa ni muhimu pia suala la muungano likajumuishwa ili kuweka fursa ya wananchi ambao ndiyo wadau wakuu wa muungano kutoa mawazo yao ya namna ya kuuboresha.
   
 13. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #13
  Nov 23, 2010
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Hivi kweli eeh!, unajua linawezekana hili ni taifa la viongozi. Inawezekana wenzetu wamebarikiwa kutawala, kati ya viongozi wakuu 5 wa nchi yetu 3 wanatoka Z'bar na 2 ndio bara. Z'bar inawatu wasiozidi 1mil na bara si chini 40mil du!, halafu majaji wakuu wote Z'bar. Hawa jamaa wana kipaji cha uongozi.
   
 14. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #14
  Nov 23, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sasa mnasema mnaibeba Znz, na ni mzigo, kwanini hamuitui?

  Ukweli ni kwanza hata waznz pia hawawataki, sasa cha kujiuliza ni nani ana-provide 'gundi' ya huu Muungano? CCM na now CUF..sasa hao ndio wakuulizwa.
   
 15. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #15
  Nov 23, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni katiba ambayo hairuhusu asiye mkazi/ mzanzibari kugombea nafasi yoyote huko Zanzibar. Ndo maana wanasema kuwa ni nchi inayojitegemea lakini ukisema Tanganyika ni nchi vilvile unaweza kunyongwa kwani utaitwa mhaini. Mkuu haya ni mapungufu kama yalivyo mengine ndani ya katiba zetu. Niulize kwanini Tanganyika tusiwe na serikali yetu badala ya kutumia ila ya muungano?
   
 16. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #16
  Nov 23, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Kila siku huwa nasema, Wazanzibar ondokeni bara muone kama mtu atawafuata. Nusu yenu mnaishi na kufanya kazi bara, wabara walioko znz si zaidi ya 5,0000. Kwahiyo, ni simple kama hamtaki muungano, fungeni maduka, acheni ajira za bara, rudisheni mashamba na majengo, enendeni kwa amani mkaijenge nchi yenu. period!
   
 17. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #17
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Binafsi nafikiri kuwa, endapo tunahitaji kuleta uwiano sawa, ni vema kuangalia mambo makuu matatu yafuatayo
  • Pato la taifa: Je shughuli za bara na Zenji zinachangiaje kwa pamoja kwenye pato la taifa. Na mgawanyo wa rasilimali na nafasi za uongozi ziendane na kigezo hicho kwanza
  • Idadi ya watu: Idadi ya watu iwe sehemu muhimu katika kuleta mgawanyo huu, lakini pia (LABDA) tunaweza kuongeza kiwango cha umaskini ili kuleta uwiano wa maendeleo kwa Tanzania
  • Maeneo kimkakati! Hili ni suala nyeti, lakini ni vema kujua - na kwa pamoja kukubaliana kwa kiwango gani Zenji ina-ihitaji bara na vivyo hivyo bara kwa Zenji. Suala la kujiuliza hapa ni je Zenji ni strategic area - eneo mkakati kwa bara? Hapa ndo itabidi kubainisha maslahi ya kila eneo
  Kisha tusema kwa mfumo huu, tunahitaji wabara wakatawale Zenji! Bila shaka ni vema hiyo inafikiriwa endapo tunahitaji umoja huo, ambao kwa sasa binafsi naona unaelekea kuzikwa
   
Loading...