Je, ni kweli sheria inatambua wapenzi wa jinsia tofauti ambao hawajaoana rasmi kuwa mme na mke?

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
32,375
29,729
Habari zenu.
Kuna hizi habari zimezagaa mitaani kuwa wapenzi wawili wa jinsia tofauti ambao hawajaoana rasmi (Yaani kuozeshwa rasmi na taasisi ya serikali au ya kidini inayotambuliwa na serikali) kuwa ni mme na mke endapo watakuwa wamekaa kwa kuishi pamoja zaidi ya miezi sita,
WANASHERIA na wenye kufahamu hili, je kuna ukweli wowote kuwa endapo mwanaume ataishi na mwanamke ambaye hajamuoa rasmi kutambulika kuwa huyo mwanamke ni mke wake kisheria baada ya kuishi nae zaidi ya miezi sita??
Asanteni.
 
Si kweli. Sheria ya Ndoa ina dhanio la ndoa ambalo kati ya sifa zake ni wawili hao kuishi miaka miwili na kuendelea. Dhanio la ndoa hutumika pale ambapo kuna mgogoro kati ya wawili hao na lengo ni kumpatia chochote kitu mwanamke. Dhanio hili huthibitishwa kimahakama na hutumika kimahakama tu.
 
Alichokujibu petrol ndo sahihi..watu wengi nmesikia wakisema ni miezi sita ni miaka 2 mara nyingi inakua appricable mahakamani kwenye mashauri ya devorce....
 
Asante sana kwa maelezo simple and clear!
 
Alichokujibu petrol ndo sahihi..watu wengi nmesikia wakisema ni miezi sita ni miaka 2 mara nyingi inakua appricable mahakamani kwenye mashauri ya devorce....
Ha ha ha sorry umesema petrol badala ya petro nimepata kicheko
 
Back
Top Bottom