Je ni kweli Serikali imeshindwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni kweli Serikali imeshindwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MwanajamiiOne, Oct 27, 2009.

 1. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #1
  Oct 27, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Habarini ndugu zangu.

  Leo ninaomba nijumuike nanyi katika jukwaa hili.

  Ninaomba ufafanuzi juu ya hili suala la mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino). Tangu suala hili lilipoanza kutangazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari naona kama bado halijatatuliwa ipasavyo. Pamoja na kuwepo ushahidi wa waliokamatwa na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria bado tunashuhudia mauaji yakiendelea na ndugu zetu hawa wakiendelea kuishi maisha ya mashaka. Ninavyohisi mimi ni kuwa serikali yetu tukufu haijalitendea haki suala hili kwa kulipa kipaumbele hafifu yaani haijalipa high priority kwa sababu ninaamini kabisa serikali ikiamua kuvalia njuga suala fulani halishindwi si wanasema mkono wa sheria mrefu? Mbona wale majambazi walovamiaga TEMEKE NBC Limited, au wale waliofanya tukio la uninja pale Ubungo walikamatwa tena within seconds? Kipi kinachozuia kukamatwa kwa wahusika wakuu wa mauaji haya?

  Ninasema wahusika wakuu kwa sababu waliokamatwa na kufikishwa mbele ya sheria ni wale wazee wa vijijini waliokamatwa na viungo lakini walikuwa wanapeleka wapi? na inakuwaje watolewe hukumu pasipo kumpata aliyewatuma? Hii si kutibu ugonjwa wakati chanzo chake bado kipo? Serikali hii ya mheshimiwa sana itatuhakikishiaje kuwa suala hili lina tofauti na lile suala la madawa ya kulevya na vinara wake?

  hata sijui kwa kweli naombeni mnisaidie kunielewesha.
   
Loading...