Je, ni kweli Rushwa imepungua?

Mk54

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2016
Posts
1,996
Reaction score
3,962
KABLA YA KUTOA MAAMUZI YA MWISHO YA KURA YAKO, TAFADHALI TAFAKARI!​

1. Je, ni kweli RUSHWA imepungua?
TAFITI sizizo rasmi ni kwamba RUSHWA bado ipo kwenye taasisi za UMMA na viongozi wetu bado wanakula rushwa. Inaonekana haipo kwa sababu hakuna chombo cha habari chenye GUTS za kuripoti UFISADI unaoendelea kwa viongozi na taasisi za UMMA. Kura yako ni sauti yako, fanya maamuzi sahihi.
-
2. Je, ni kweli hakuna AJIRA?
Suala la kujiajiri au kutoka nje ya BOX ni UZUSHI kama hutowezeshwa. wewe kama mzazi unajisikiaje kumuona mwanao amemaliza chuo na yupo yupo tu anacheki FILM?
-
Malalamiko mengi juu ya AJIRA nyingi kupewa WANAJESHI huku wenye taaluma wakiendelea kusugua. Hata hivyo, TAFITI zisizo RASMI zinaonesha ya kwamba asilimia kubwa ya WANAJESHI hawafanyi vyema kwenye TAASISI HIZO kutokana na ukosefu wa Management and Leadership Skills. Wao wanachojua ni KOMANDI TU, Tumeona kwenye ishu ya Mkurugenzi wa TAKUKURU huku maafisa zaidi ya 5 wakifukuzwa kazi yeye akiendelea kuwepo kwenye nafasi yake. Kuna yule Brigedia mwingine aliharibu na kuingia kwenye kashfa ya UFISADI, Badala yake alipewa UBALOZI huku watumishi wengine wakitumbuliwa na kuozea segerea, je usawa upo wapi? Kura yako ni sauti yako, fanya maamuzi sahihi.
-
3. Je, ni kweli watumishi wa UMMA hawajaongezewa mishahara?
TAFITI za kibenki zinaonesha watumishi wa UMMA wengi wanaishi chini ya thelusi ya mshahara ghafi kwa wingi wa madeni huku wengine wakikimbilia kwenye MICROFINACE na mwishowe kuuziwa mali zao kama GARI na NYUMBA. Aidha, inasemwa PAYEE imepungua kutoka asilimia 15 hadi 11 ambayo ni sawa na ongezeko la kati ya 9 000 hadi 12,000 katika mshahara ghafi kwa kipindi cha miaka 5. Kura yako ndio sauti yako, fanya maamuzi sahihi.
-
4. Je, ni kweli Sheria ya Manunuzi ya Umma Na.7 ya mwaka (2011) na Kanuni zake (2013) sambamba na Marekebisho (2016) haifuatwi

Wengi hawakuridhishwa na MAELEZO ya msemaji wa SERIKALI. IKama ilikuwa ni Restrictive Tendering Method ndiyo iliyotumika kumpata MSHITIRI, na kwakuwa MANUNUZI ya ndege yanahusisha Maslahi ya Taifa, kwanini hakukuwa na TRANSPARENCY? Inawezekana wazo la kununua ndege kwa CASH lilikuwa ni zuri, lakini tukubali kuwa UTEKELEZAJI wake umefeli. 90% ya mashirika ya ndege duniani yanajiendesha kwa hasara. Je la kwetu vipi? Kura yako ni sauti yako, fanya maamuzi sahihi.
-
5. Je, Ni kweli bodi ya Mikopo imeshindwa kusikiliza wanufaika?
Makato ya MKATABA wa awali baina ya BODI na WANUFAIKA yalikuwa ni asilimia 8 katika mshahara ghafi, mwaka 2015 ilipandishwa kutoka asilimia 8 hadi 15 kinyume na mkataba wa awali huku tozo ya asilimia 6 ikiwa ipo pale pale. Barua pamoja na malalamiko yalipelekwa Bodi ya Mikopo huku barua za malalamiko zikienda IKULU bila mafanikio. Kura yako ni sauti yako, fanya maamuzi sahihi. Tumia fursa ya kuomba karatasi nyingine ya kupigia kura kubadili maamuzi na mtazamo wako.
-
6. Je, ni kweli familia ya Mwalimu imesahaulika?
Mpinzani alipofika BUTIAMA, familia ya Mwalimu ilimkaribisha, akala na kulala kisha wakampeleka kuhani kaburi. Katika chakula cha usiku, familia hiyo ilimueleza Mpinzani huyo masikitiko yao juu ya kusahaulika na kusisitiza kwamba watampigia kura Mpinzani huyo ikiwa ni sehemu ya CHUKIZO. Alisikika Mama Maria akisema, kwenye kampeni ameenda kuongeza idadi tu. Kura yako ni sauti yako, fanya maamuzi sahihi.
-
7. Je, ni kweli TANROADS ni mtoto wa mwisho anaedekezwa?
Changamoto za TANROADS zinajulikana kwa ujenzi wa barabara chini ya viwango kwa takribani miaka yote 25, barabara ambazo kila mvua zikinyesha ni lazima ziwekewe VIKARA. Je kuna siri gani nyuma ya pazia ya TANROADS? Kila siku barabara zinajengwa na kila siku barabara hizo hizo zinaharibika, je huu ni mradi wa mtu binafsi katika kutumia kodi zetu isivyo halali? Raisi halijui hili? Kura yako ni sauti yako, fanya maamuzi sahihi.
-
8. Je, BIMA ya Afya kupitia NHIF, haikidhi haja za waTanzania?

Wanaofaidika na NHIF ni wale ambao wapo katika AJIRA. Ikiwa hujaajiriwa, ili upate Bima ya NHIF, ni lazima uwe na pesa taslimu 1,550,000 kwa kila mwaka ambayo kimsingi mkulima wa kawaida hawezi. Suala la Bima ya Afya kwa kila Mtanazania lipo kisheria, kuendelea kuweka kiwango cha pesa hiko ni kuwanyima watanzania haki zao za msingi. TAFAKARI SANA. Kura yako ni sauti yako, fanya maamuzi sahihi. Achana na ma TV na MATANGAZO, angalia hali halisi ya MTANZANIA WA LEO
-
9. Je, ujenzi wa SGR hauna uhalisia?

Ni takribani miaka 4 mpaka leo hii ujenzi huu haujaweza hata kufika Morogoro, je itachukua miaka mingapi kufika DODOMA? TAFAKARI, kura yako ni Sauti yako, fanya maamuzi sahihi

Mwisho, Tuliombee Amani taifa letu na usikubali kuaminishwa kuwa kila unapotoa maoni yaliyo kinyume na UTAWALA basi wewe ni MSALITI au SIO MZALENDO. Huenda wewe ni MZALENDO ZAIDI. Aidha, Taifa letu tukufu linaweza kuongozwa na mtu yoyote mwenye SIFA. Hakuna watu maalumu kuwa wao ndio FIMBO ni lazima kuongoza. Yoyote anaejaribu kupata ridhaa hiyo hutengenezewa mazingira aonekana MSALITI AU SIO MZALENDO. TUMIA Neema ya akili yako kutafakari.

Fanya maamuzi sahihi, just decide, make a difference make a choice. Dunia ni yako na wote sisi ni MAVUMBI. TUAMUE KWA MANUFAA YA VIZAZI VYETU. TUAACHANE NA MATV NA MATANGAZO TANGAZO, KITU KIZURI HAINA HAJA YA KUTANGAZWA, KINAONEKANA, HIVYO, TUANGALIE HALI HALISI YA MTANZANIA WA LEO.
 
Rushwa imepungua sana Tanzania

Hongera kwa Rais Magufuli kwa kutuondolea rashwa
 
Huwezi kudeal na rushwa bila ya kuwepo uwazi( transparency). So watu wanaweza kuhisi rushwa haipo lkn kwa sababu hamna uwazi wa matumizi ya fedha ni vigumu kujua hilo.
 
Rushwa imepungua sana Tanzania

Hongera kwa Rais Magufuli kwa kutuondolea rashwa

Hata Mimi ni muumini wa JPM, linapokuja suala la maslahi ya nchi tuangalie uhalisia.

Rushwa imepungua kwa kutumia matangazo, yaani tunalazimishwa kuamini hivi kinyume na uhalisia! Ukiona mtu kapiga na kafikishwa Takukuru ujue huyo mtu kuna Bifu . Wasio kuwa na Bifu wanapeta kama kawaida . Yupo wapi Kangi ? TAKUKURU ilitoa tamko lolote ? Na yule aliyezawadiwa Ubalozi je ?

Utaondoaje wafanyakazi wa TAKUKURU na kumuacha Mkurugenzi wao ? Raisi ndiyo aliyefichua ule uozo kupitia special auditing , je Mkurugenzi Mkuu alikuwa wapi kushindwa kuona hiyo RUSHWA? Kama watendaji wameondolewa yeye anafanya nini ! ?
 
Huwezi kudeal na rushwa bila ya kuwepo uwazi( transparency). So watu wanaweza kuhisi rushwa haipo lkn kwa sababu hamna uwazi wa matumizi ya fedha ni vigumu kujua hilo.

Vyombo vya Habari ni kufichua uozo. Leo Hii ni nani mwenye guts za kuripoti Uozo? Utawezaje kutenganishwa Rushwa na Transparency ?
 
Baada ya kusoma huu uzi nimemkumbuka mkaguzi mkuu wa serikali aliyepita/kuondolewa.

Ustadhi alikuwa anaamini katika UWAZI. Kwa sasa hutosikia hoja za msingi. Fanya maamuzi sahihi!
 
Rushwa ipo na itaendelea kuwepo. Ata swala la kuajir kwa connection pia ni rushwa, Kusifia ata unapoona mapangufu ili uonekane na ww upewe nafasi ni rushwa pia.

Sema Tumezibwa macho na masikio alaf tunaambiwa hakuna kelele wala hakuwa kinacho onekana
 
Umeeleza vizuri sana.
Tanzania kuna vitu vya ajabu sana leo hii tunawaambia vijana wajiajiri huku watu kama wakina mkuchika, kimei, fred lowasa, Nape, Anton mavunde hawa wote wanauwezo wa kujiajiri lakini tunawaambia vijana wa kimaskini wajiajiri huku wao wakiendelea kula mema ya nchi.

Wanaosema rushwa imeisha sijui wanaishi tanzania ipi hiyo? Wakati zahanati tu utaingia kumuona dokta kama umetanguliza pesa.
 

Na hakuna kitu KIBAya kama kumnyima Mtu uhuru wake wa kuhoji na kufichua uovu kwa maslahi ya wengi. Muda mwingi umetumika kuNYAMAZISHA watu badala ya kujenga nchi kwa Maslahi ya wengi.

Na hizo nguvu zilizotumika kunyamazisha watu hazijazaa matunda, badala yake wengi wameumizwa na wengi wanazidi kusema.

Mtu kama JK, Mwinyi unawajengea Nyumba like serious ? Na hiyo nyumba wala hatoishi yeye, Atampa Mpwa wake akae.

Mtu ambae anakula 80% ya mshahara wake kila mwezi unamjengea nyumba kwa kodi zetu huku baadhi ya vijiji mpaka leo hakuna Maji safi, hakuna Madawati. JK is rich ana miradi mingi Mason ya kufa mtu Msoga na mjini .

Ana share nyingi Kwenye makampuni ya simu na miradi mbalimbali. Huku raia wa kawaida anaoneshwabDaraja la Ubungo kama ishara ya maendeleo, wanajeshi wanakamata nafasi za Umma na wataalam wana kaa pembeni, Bodi ya Mikopo imekuwa ni Utapeli , NHIF haimuhusu Mtanzania wa Hali ya chini. Kura yako ni Sauti yako , Amua !
 
Ka naona unavoumia kaka ila ndo hivo
 
Rushwa inaishaga kwenye vitengo vya polisi na mahakama??
Nenda ardhi, NHC Dar, wanaita facilitation,

Nenda hospital na zahanati za serikali, inakeraa!

Tunahitaji mifumo imara dhabiti,

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…