Je, ni kweli Mungu yupo mahali popote?

Je, ni kweli Mungu yupo mahali popote?

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,392
Reaction score
7,863
Wote wanatuambia Mungu ni "Omnipresent" yaani yuko mahali popote mda wowote,
Yuko hapa, yuko pale, na kule kwa mda mmoja yuko sehemu zote; hakuna sehemu ambako hayupo, kila sehemu yupo.!

Sasa hii sehemu inayoitwa Jehanamu inawezekana vipi ikawepo? Au kama ipo mbona wanasema Mungu hayupo huko?

Mungu yuko mahali popote na kila kitu kilichopo ni chake, kwa hiyo kila kitu kitakachotajwa kuwepo basi Mungu yuko kwenye kitu hicho, hawezi kuwa nje ya hapo.

Atakuwa wapi kama hayupo ndani ya vitu vilivyopo kama anatakiwa kuwa mahali popote na kwa muda wote.!?

Inaonekana hawezi kuwa nje ya sehemu yoyote, hivi nje ya sehemu yeyote ni wapi?

Hakuna nje ya sehemu yeyote, yaani kama kuna kitu hakuna sehemu hakuna kitu kwa hiyo Mungu atakuwa mahali pote. Sasa huyu anayeitwa Shetani sio kitu kusema Mungu anatakiwa kuwa ndani yake.!?

Wao wanasema; Shetani ni kitu kingine tofauti na Mungu, na wanasema Shetani sio Mungu na hana uMungu ndani yake, na sehemu anayopatikana –jehanamu– huko hakuna Mungu.

Basi hapo Mungu amekosa sifa za kuwa Mungu, amekosa sifa ya kuwa mahali popote kwa muda wowote – Omnipresent.

Wewe ni kitu (Matter) hivyo manifestation ya Mungu inatakiwa kuwepo kwenye kitu chochote, sasa kama Mungu anaweza kuji-manifest kwenye kila kitu hakuna namna utaniambia Mungu yuko NJE yangu.

Ukiniambia hakuna uungu ndani yangu basi Mungu amekosa sifa ya kuwa Omnipresent.

Kwa hiyo Mungu kama ana sifa ya kuwa popote yupo NDANI yangu, na kwenye nyama zangu na kwenye kila kitu ambacho ni MIMI.

Ndio, Mimi ni Mungu.
Mungu ni Mimi, kwa hiyo Mimi ni Mimi
I am I, I am Who I am, I am God.!

Je, Hamsadiki?

Yohana 14:10-11
[10]Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.

[11]Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.

Sasa kama mtasubiri mpaka niwaoneshe kazi ambao naweza kuzifanya kama Mungu, nitafanya kazi ambazo hata ni zaidi ya hizo

Yohana 14:12
[12]Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.

Baada ya kuwa nishazifanya sasa hizo kazi

Yohana 14:20
[20]Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu.

Anyway, mimi sio Yesu, hapa nilikuwa nawapa mafundisho ambayo ni sawa kwa kila mtu.
Kwenye Physics kuna kitu kinaitwa
"Zeroth Law of Thermodynamics"
Huwa kinahusu uwiano wa joto kinasema hivi: Kama A ni sawa B, alafu B ni sawa na C basi A itakuwa sawa na C.

Sasa, kama Yesu yu ndani ya Baba yake, na baba yake yu ndani yake, tena Yesu yu ndani ya Sisi, basi Baba yake yu ndani yetu.

Hata hivyo Sisi tu ndani ya Yesu, na Yesu yu ndani ya Baba yake, kwa hiyo sisi tu ndani ya Baba, na Baba yu ndani ya Sisi.

Hakuna Namna sisi na Baba tunaweza kutengana, sisi na Baba ni kitu kimoja kama alivyo Yesu na Baba kwa sababu Yesu ni kitu kimoja na Sisi.

Hivyo basi, Sisi sio tu kuwa ndani ya Baba na Baba kuwa ndani yetu, Bali sisi ndio Baba.!
 
Wote wanatuambia Mungu ni "Omnipresent" yaani yuko mahali popote muda wowote

Yuko hapa, yuko pale, na kule kwa mda mmoja yuko sehemu zote; hakuna sehemu ambako hayupo, kila sehemu yupo.!

Sasa hii sehemu inayoitwa Jehanamu inawezekana vipi ikawepo.!? Au kama ipo mbona wanasema Mungu hayupo huko.!?

Mungu yuko mahali popote na kila kitu kilichopo ni chake, kwa hiyo kila kitu kitakachotajwa kuwepo basi Mungu yuko kwenye kitu hicho, hawezi kuwa nje ya hapo.!

Atakuwa wapi kama hayupo ndani ya vitu vilivyopo kama anatakiwa kuwa mahali popote na kwa muda wote.!?

Inaonekana hawezi kuwa nje ya sehemu yoyote, hivi nje ya sehemu yeyote ni wapi.!?

Hakuna nje ya sehemu yeyote, yaani kama kuna kitu hakuna sehemu hakuna kitu kwa hiyo Mungu atakuwa mahali pote.

Sasa huyu anayeitwa Shetani sio kitu kusema Mungu anatakiwa kuwa ndani yake.!?

Wao wanasema; Shetani ni kitu kingine tofauti na Mungu, na wanasema Shetani sio Mungu na hana uMungu ndani yake, na sehemu anayopatikana –jehanamu– huko hakuna Mungu.

Basi hapo Mungu amekosa sifa za kuwa Mungu, amekosa sifa ya kuwa mahali popote kwa mda wowote– Omnipresent.

Wewe ni kitu (Matter) hivyo manifestation ya Mungu inatakiwa kuwepo kwenye kitu chochote, sasa kama Mungu anaweza kuji-manifest kwenye kila kitu hakuna namna utaniambia Mungu yuko NJE yangu.

Ukiniambia hakuna uungu ndani yangu basi Mungu amekosa sifa ya kuwa Omnipresent.!

Kwa hiyo Mungu kama ana sifa ya kuwa popote yupo NDANI yangu, na kwenye nyama zangu na kwenye kila kitu ambacho ni MIMI.

Ndio, Mimi ni Mungu.
Mungu ni Mimi, kwa hiyo Mimi ni Mimi
I am I, I am Who I am, I am God.!

Je, Hamsadiki.!?

Yohana 14:10-11
[10]Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.

[11]Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.

Sasa kama mtasubiri mpaka niwaoneshe kazi ambao naweza kuzifanya kama Mungu, nitafanya kazi ambazo hata ni zaidi ya hizo

Yohana 14:12
[12]Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.

Baada ya kuwa nishazifanya sasa hizo kazi

Yohana 14:20
[20]Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu.

Anyway, mimi sio Yesu, hapa nilikuwa nawapa mafundisho ambayo ni sawa kwa kila mtu.
Kwenye Physics kuna kitu kinaitwa
"Zeroth Law of Thermodynamics"
Huwa kinahusu uwiano wa joto kinasema hivi: Kama A ni sawa B, alafu B ni sawa na C basi A itakuwa sawa na C.

Sasa, kama Yesu yu ndani ya Baba yake, na baba yake yu ndani yake, tena Yesu yu ndani ya Sisi, basi Baba yake yu ndani yetu.

Hata hivyo Sisi tu ndani ya Yesu, na Yesu yu ndani ya Baba yake, kwa hiyo sisi tu ndani ya Baba, na Baba yu ndani ya Sisi.

Hakuna Namna sisi na Baba tunaweza kutengana, sisi na Baba ni kitu kimoja kama alivyo Yesu na Baba kwa sababu Yesu ni kitu kimoja na Sisi.

Hivyo basi, Sisi sio tu kuwa ndani ya Baba na Baba kuwa ndani yetu, Bali sisi ndio Baba.!
 
Wote wanatuambia Mungu ni "Omnipresent" yaani yuko mahali popote mda wowote,
Yuko hapa, yuko pale, na kule kwa mda mmoja yuko sehemu zote; hakuna sehemu ambako hayupo, kila sehemu yupo.!

Sasa hii sehemu inayoitwa Jehanamu inawezekana vipi ikawepo? Au kama ipo mbona wanasema Mungu hayupo huko?

Mungu yuko mahali popote na kila kitu kilichopo ni chake, kwa hiyo kila kitu kitakachotajwa kuwepo basi Mungu yuko kwenye kitu hicho, hawezi kuwa nje ya hapo.

Atakuwa wapi kama hayupo ndani ya vitu vilivyopo kama anatakiwa kuwa mahali popote na kwa muda wote.!?

Inaonekana hawezi kuwa nje ya sehemu yoyote, hivi nje ya sehemu yeyote ni wapi?

Hakuna nje ya sehemu yeyote, yaani kama kuna kitu hakuna sehemu hakuna kitu kwa hiyo Mungu atakuwa mahali pote. Sasa huyu anayeitwa Shetani sio kitu kusema Mungu anatakiwa kuwa ndani yake.!?

Wao wanasema; Shetani ni kitu kingine tofauti na Mungu, na wanasema Shetani sio Mungu na hana uMungu ndani yake, na sehemu anayopatikana –jehanamu– huko hakuna Mungu.

Basi hapo Mungu amekosa sifa za kuwa Mungu, amekosa sifa ya kuwa mahali popote kwa muda wowote – Omnipresent.

Wewe ni kitu (Matter) hivyo manifestation ya Mungu inatakiwa kuwepo kwenye kitu chochote, sasa kama Mungu anaweza kuji-manifest kwenye kila kitu hakuna namna utaniambia Mungu yuko NJE yangu.

Ukiniambia hakuna uungu ndani yangu basi Mungu amekosa sifa ya kuwa Omnipresent.

Kwa hiyo Mungu kama ana sifa ya kuwa popote yupo NDANI yangu, na kwenye nyama zangu na kwenye kila kitu ambacho ni MIMI.

Ndio, Mimi ni Mungu.
Mungu ni Mimi, kwa hiyo Mimi ni Mimi
I am I, I am Who I am, I am God.!

Je, Hamsadiki?

Yohana 14:10-11
[10]Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.

[11]Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.

Sasa kama mtasubiri mpaka niwaoneshe kazi ambao naweza kuzifanya kama Mungu, nitafanya kazi ambazo hata ni zaidi ya hizo

Yohana 14:12
[12]Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.

Baada ya kuwa nishazifanya sasa hizo kazi

Yohana 14:20
[20]Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu.

Anyway, mimi sio Yesu, hapa nilikuwa nawapa mafundisho ambayo ni sawa kwa kila mtu.
Kwenye Physics kuna kitu kinaitwa
"Zeroth Law of Thermodynamics"
Huwa kinahusu uwiano wa joto kinasema hivi: Kama A ni sawa B, alafu B ni sawa na C basi A itakuwa sawa na C.

Sasa, kama Yesu yu ndani ya Baba yake, na baba yake yu ndani yake, tena Yesu yu ndani ya Sisi, basi Baba yake yu ndani yetu.

Hata hivyo Sisi tu ndani ya Yesu, na Yesu yu ndani ya Baba yake, kwa hiyo sisi tu ndani ya Baba, na Baba yu ndani ya Sisi.

Hakuna Namna sisi na Baba tunaweza kutengana, sisi na Baba ni kitu kimoja kama alivyo Yesu na Baba kwa sababu Yesu ni kitu kimoja na Sisi.

Hivyo basi, Sisi sio tu kuwa ndani ya Baba na Baba kuwa ndani yetu, Bali sisi ndio Baba.!
Huduma nzuri ya ubongo
 
Kuna mambo mengi sana yanaumana kuhusu sifa za Mungu hasa wa vitabu hivyo viwili.. inahitaji utafakari yakini kuelewa Mungu ni nini..?
Sifa alizopewa zinauma na kukinzana mi ndio maana naona Mungu anaehubiriwa ktk uislamu na ukristo ni ulaghai!.

Wengi wanashindwa kufungua bongo zao na kutafakarisha juu ya Uungu!,wametanguliza uoga,kukariri na kupigania vitu wasivyovijua ama kuvitafakari kwa kina!.. bila shaka ninasema kwa dhati watu wengi wamejaa ujinga juu ya nadharia ya Umungu/Mungu!.

Wenye akili wataendelea kupiga fedha juu ya nadharia ya Umungu,watu mtadanganywa Sana maana upofu mmejitanda wenyewe.

Inahitaji tafakari kutoka hapo ulipo na kujua hii nadharia jinsi inavyotafuna watu..
 
Unaongelea mungu yupi?
Mungu wa wakristo yupo kila sehemu hadi huko jehanam.
Mungu wa waislam yupo mbingunj huko amekalia kiti.
 
mungu ni nguvu ya uhai iyo nguvu ipo kwa kila kilicho hai kinachoonekana na kisichoonekana , shetani ni nguvu hasi ambayo ipo kusaidiana na nguvu chanya ili kuleta uwiano ( balance) Tunajaribiwa na tamaa zetu wenyewe.
 
Unaongelea mungu yupi?
Mungu wa wakristo yupo kila sehemu hadi huko jehanam.
Mungu wa waislam yupo mbingunj huko amekalia kiti.
Wewe unaongelea Mungu yupii?

Jehanamu ndo wapii?

Mbinguni ndo wapii?
 
Mimi swali nalojiuliza hadi leo, ikiwa yeye ananifahamu kabla ata sijazaliwa kwa nini nihofie maisha yangu duniani?. Kwa nini nitishiwe juu ya amri zake ikiwa yeye anafahamu leo naenda kufanya zinaa, ntakufa kwa kuiba?
 
Back
Top Bottom