Je, ni kweli mtu akijifungua kwa operation uzao wa kwanza hawezi tena kujifungua kawaida?

Abuu Ibrah

Senior Member
Sep 3, 2014
129
14
Mwanamke aliyezaa kwa operesheni katika mzao wake wa kwanza, hawezi tena kujifungua kwa njia ya kawaida?

Na nini kinapelekea wanawake wengi zama zetu hizi kujifungua kwa operesheni?
 
Asilimia kubwa ni njia hazifunguki mapema kutokana na kutokufanya mazoezi inavotakiwa wengine wanakua wanatoka maji ya hatari katika njia ya uzazi amabayo itamletea madhara mtoto
 
Mwanamke alozaa kwa operesheni katika mzao wake wa kwanza, hawezi tena kujifungua kwa njia ya kawaida?
na nini kinapelekea wanawake wengi zama zetu hizi kujifungua kwa operesheni?
Hiz tabia za kutumia midawa ya kuzuia mimba hali ya kuwa hana hata ndo na kubweteka pindi apatapoa mimba ndo sababu kubwa
 
Wenginee wanapenda upasuaji tena wanamwambia Dr awafanyiee kisa wanaogopa sehemu zao zitatanuka zaidi ,upasuaji mwingi sasa wanaomba wenyewee.kama hauamini Fanya utafiti Mdogo eneo unaloishii
 
Hiz tabia za kutumia midawa ya kuzuia mimba hali ya kuwa hana hata ndo na kubweteka pindi apatapoa mimba ndo sababu kubwa
jmn co kweli co kila mtu anaomba afanyiwe operation jmn wengine inatokea mtu anafanya mazoezi hatumii uzazi wa mpango rkn operation anafanyiwa
 
Kurudiwa kwa operation ya kujifungua ni kwa sababu: kama mama ana maumbile madogo hususani ya mifupa ya nyonga au alipata kupooza nyonga akiwa bado mdogo basi huyo atahitaji kufanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua. Kama sababu za kufanyiwa upasuaji sio zile zinazojirudia kama kutoka damu ukeni kwenye mimba pevu, mtoto kutanguliza matako, mapigo ya mtoto kuwa kasi au kupungua katika mimba zinazofutia si lazima kufanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua.
Mara mama anapofanyiwa upasuaji kwa mara ya pili kwa ajili ya kujifungua basi huyo anashauriwa awe anajifungua kwa njia ya upasuaji kwani kovu lake si salama.
 
Mwanamke aliyezaa kwa operesheni katika mzao wake wa kwanza, hawezi tena kujifungua kwa njia ya kawaida?

Na nini kinapelekea wanawake wengi zama zetu hizi kujifungua kwa operesheni?
Jibu la swali lako ni HAPANA.
Bali, inategemea nini hasa kilisababisha "oparesheni" katika huo uzao wa kwanza? Kama ni sababu ambayo ni permanent na haibadiliki, basi ndio hataweza tena kujifungua njia ya kawaida (mfano: njia ya uzazi "nyonga" ndogo isiyoweza kupitisha mtoto). Kwa hiyo basi, kama uzazi wa kwanza ulijifungua kwa mnjia ya oparesheni, na sababu ilikuwa ni ile ambayo sio ya permanent mfano kondo kutangulia (placenta previa), uzazi wa pili unaweza kujaribu kujifungua kwa kawaida (trial of scar). Lakini, hii inabidi ifanyike chini ya uangalizi, kuhakikisha kuwa wahudumu wa afya wamejiandaa kufanya oparasheni muda wowote ule mambo yakienda vibaya.
Baadi ya sababu ambazo zinaweza kusababisha ushindwe kujifungua njia ya kawaida na kuhitaji "oparesheni" ni kama ifuatavyo:
-Nyonga nyembamba isiyoweza kupitisha mtoto
-Kama una ugonjwa mwingine wa muda mrefu ambao utaleta shida wakati wa kujifungua kama ugonjwa wa moyo,
-Mtoto kutanguliza miguu/matako
-Kondo kutangulia (placenta previa)
-Mtoto mkubwa kupita kiasi (big baby)
-Mimba ya mapacha wawili/watatu/wanne
-mtoto kulala vibaya (transverse/oblique lie)
-Uchungu kwenda taratibu sana au kushindwa kuprogress
-Mtoto kuchoka (fetal distress).
Ni muhimu kuelewa kuwa, sababu zote hizo hapo juu (isipokuwa ya kwanza), ni sababu ambazo ni relative; kumaanisha kwamba si lazima mfano mama akiwa na mimba ya mapacha basi ajifungue kwa oparesheni, uamuzi utategemea mambo mengi ikiwa ni pamoja na hali ya mama,etc etc.

shukrani sana kwa elimu Dr. je kama operation ilisababishwa na pressure pre eclampsia nitaweza kujifungua kawaida kwa uzao wa pili? kama sio, nifanye nn ili niweze kujifungua kawaida?
 
Wanaume wa mjini wana vibamia, hawazibui kisawasawa njia za kuingilia duniani .... vijijini wanaendelea kujifungua kawaida.
 
shukrani sana kwa elimu Dr. je kama operation ilisababishwa na pressure pre eclampsia nitaweza kujifungua kawaida kwa uzao wa pili? kama sio, nifanye nn ili niweze kujifungua kawaida?
Ahsante kwa kushukuru mkuu.
Kama sababu ya oparesheni uzazi wa kwanza ilikuwa ni pre-eclampsia, basi uzazi wa pili mama anaweza kabisa kujaribu kujifungua kwa njia ya kawaida; Kinachotakiwa ni
-Kuanza kliniki mapema, na kuhudhuria kliniki kwa kadri alivyopangiwa-hii ni muhimu kwa sababu wahudumu wa afya watakuwa wakimpima pressure yake kila anapoenda kliniki ili kuhakikisha si kubwa kuliko kawaida; kwa vile huyu anakuwa katika uwezekano mkubwa zaidi wa kuweza kupata pre-eclampsia tena,
-Kufanya kipimo cha ultra sound kwa kadri itakavyoshauriwa ili kuhakikisha ukuaji wa mtoto uko vizuri,
-Kuhakikisha kuwa wakati wowote atakaposikia dalili za pre-eclampsia (kuumwa kichwa,kuona maluwe luwe,mkojo kupungua,maumivu ya chembe ya moyo) aweze kwenda kituo cha huduma ya afya upesi ili kuhakikisha kuwa kama kuna shida inashughulikiwa haraka ipasavyo
-Ushirikiano na utayari wa mama pale ambapo uchungu tuu unaanza, awahishwe mapema kituo cha huduma ya afya, na aweze kufuata maelekezo atakayopewa na wahudumu wa afya, ili muda utakapofika aweze ku-push mtoto wake vizuri,

Two ten
 
asante sana mkuu, barikiwa sana Dr .
 
ukishajifungua mtoto wa kwanza kwa operation, uwezekano wa kuja kujifungua watoto wengine kawaida ni mdogo sana
 
Kurudiwa kwa operation ya kujifungua ni kwa sababu: kama mama ana maumbile madogo hususani ya mifupa ya nyonga au alipata kupooza nyonga akiwa bado mdogo basi huyo atahitaji kufanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua. Kama sababu za kufanyiwa upasuaji sio zile zinazojirudia kama kutoka damu ukeni kwenye mimba pevu, mtoto kutanguliza matako, mapigo ya mtoto kuwa kasi au kupungua katika mimba zinazofutia si lazima kufanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua.
Mara mama anapofanyiwa upasuaji kwa mara ya pili kwa ajili ya kujifungua basi huyo anashauriwa awe anajifungua kwa njia ya upasuaji kwani kovu lake si salama.
safi sana
bila kusahau muda aliotumia kubeba mimba nyingine baada ya kupasuliwa
 
asante sana mkuu, barikiwa sana Dr .
lakini pia pre-eclampsia sio sababu tosha ya mama kufanyiwa upasuaji, ila inawezekana katika hiyo pre- eclampsia ilokupata huenda mapigo ya moyo ya mtoto yalibadilika( to low or high) ndio kupelekea kufanyiwa operation
 
Kurudiwa kwa operation ya kujifungua ni kwa sababu: kama mama ana maumbile madogo hususani ya mifupa ya nyonga au alipata kupooza nyonga akiwa bado mdogo basi huyo atahitaji kufanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua. Kama sababu za kufanyiwa upasuaji sio zile zinazojirudia kama kutoka damu ukeni kwenye mimba pevu, mtoto kutanguliza matako, mapigo ya mtoto kuwa kasi au kupungua katika mimba zinazofutia si lazima kufanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua.
Mara mama anapofanyiwa upasuaji kwa mara ya pili kwa ajili ya kujifungua basi huyo anashauriwa awe anajifungua kwa njia ya upasuaji kwani kovu lake si salama.

Ahsante kwa ushauri
 
Jibu la swali lako ni HAPANA.
Bali, inategemea nini hasa kilisababisha "oparesheni" katika huo uzao wa kwanza? Kama ni sababu ambayo ni permanent na haibadiliki, basi ndio hataweza tena kujifungua njia ya kawaida (mfano: njia ya uzazi "nyonga" ndogo isiyoweza kupitisha mtoto). Kwa hiyo basi, kama uzazi wa kwanza ulijifungua kwa mnjia ya oparesheni, na sababu ilikuwa ni ile ambayo sio ya permanent mfano kondo kutangulia (placenta previa), uzazi wa pili unaweza kujaribu kujifungua kwa kawaida (trial of scar). Lakini, hii inabidi ifanyike chini ya uangalizi, kuhakikisha kuwa wahudumu wa afya wamejiandaa kufanya oparasheni muda wowote ule mambo yakienda vibaya.
Baadi ya sababu ambazo zinaweza kusababisha ushindwe kujifungua njia ya kawaida na kuhitaji "oparesheni" ni kama ifuatavyo:
-Nyonga nyembamba isiyoweza kupitisha mtoto
-Kama una ugonjwa mwingine wa muda mrefu ambao utaleta shida wakati wa kujifungua kama ugonjwa wa moyo,
-Mtoto kutanguliza miguu/matako
-Kondo kutangulia (placenta previa)
-Mtoto mkubwa kupita kiasi (big baby)
-Mimba ya mapacha wawili/watatu/wanne
-mtoto kulala vibaya (transverse/oblique lie)
-Uchungu kwenda taratibu sana au kushindwa kuprogress
-Mtoto kuchoka (fetal distress).
Ni muhimu kuelewa kuwa, sababu zote hizo hapo juu (isipokuwa ya kwanza), ni sababu ambazo ni relative; kumaanisha kwamba si lazima mfano mama akiwa na mimba ya mapacha basi ajifungue kwa oparesheni, uamuzi utategemea mambo mengi ikiwa ni pamoja na hali ya mama,etc etc.
Abuu Ibrah

Ahsante sana kwa ushauri wako Dr.
Mke wangu alijifungua kwa Op. Mara ya kwanza, sasa ana mimba nyingine ndo nikauliza hivyo, mi natamani sana ajifungue kawaida ila sijuwi cha kufanya ili itimie tamani yangu.
 
Sio kweli!

Nami nimewahi fungua uzi humu kuuliza hii. Na pia nimeuliza baadhi ya madaktari na pia kusoma baadhi ya articles ktk mtandao.
Sababu ya kuzaa kwa operation yaweza kuwa ni sababu zinazosababishwa na mzazi yaani mama au sababu zinazosababishwa na mtoto, mfano mtoto kakaa vibaya, au mtoto kuwa mkubwa kuliko njia ya kupita. Kama ni hatari kwa afya ya mmojawapo, basi operationa ni njia sahihi!

Pia inasemekana ili uwe na chansi za kujifungua tena kwa njia ya kawaida ni lazima ule mpasuo wa awali uwe umepona kabisa la sivyo unaweza chanika!! Hivyo hakikisha kati ya kujifungua mtoto na mtoto kunakuwa na nafasi ya kutosha kwa mshono kupona kabisa, kwa wanawake walio chini ya thirties, mishono hupona haraka kuliko wanawake wazima zaidi yaani thirties na kuendelea. Hivyo wanawake wa below thirties na hasa below 27 wana chansi kubwa ya kuja kuzaa kwa kawaida kama uzazi wa kwanza ulikuwa ni wa operation na wanataka kuzaa kwa VAginal Birth After Caesarian ( VBAS).

Pia wanawake wengi wana condition inaitwa CEPHALOPELVIC DISPROPOTION yaani nyonga ndogo, hii haina dawa, kama nyonga ni ndogo itabidi tu afanyiwe operation ila sababu kubwa ya kuwa na nyonga ndogo ni mtoto kuwa mkubwa, hamna kitu cha kama nyonga ndogo, ishu ni mtoto kuwa mkubwa zaidi ya njia ya kupita.
Ebu google VBAC (Vaginal Birth After Caesarian) utapata elimu ya kutosha!

Ila jibu la Swali lako ni SIO KWELI ila kutokana na baadhi ya conditions yaweza ikawa hivyo, yaani itabidi uzae kwa operations mimba zinazofuata kutokana na mimba ya kwanza kuwa ya operation!!
 
Back
Top Bottom