- Source #1
- View Source #1
Wakuu nimekutana na kipande cha video cha mtu huko mtandaoni akieleza kuwa maji yaliyochanganya na majivu yanaweza kutumika kama njia ya kuzuia mimba. JamiiCheck hii ina uhalisia kiasi gani?
- Tunachokijua
- Madai
Kupitia mitandao ya kijamii mtumiaji mmoja alichapisha maudhui ya kuwahamasisha watu kutumia maji yaliyochanganywa na majivu kama njia ya kuzuia ama kuharibu ujauzito ndani ya saa 72.
Uhalisia wa madai hayo ni upi?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia machapisho na tafiti za kisayansi umejirirdhisha kuwa mbinu hiyo haijathibitishwa wala kupendekezwa.
Tafiti zinabainisha kuwa kumekuwa na matumizi ya njia mbalimbali za utoaji ama kuzuia mimba ikiwemo ya unywaji wa maji yenye majivu katika maeneo mbalimbali ulimwenguni ikiwemo Afrika Mashariki.
Shirika la Afya Duniani Duniani (WHO) linataja njia za kuzuia mimba ambazo ni pamoja na vidonge, kondomu, sindano na nyinginezo bila kutaja majivu ama maji yaliyokorogwa na majivu kama njia mojawapo.
Tovuti ya CDC ya serikali ya Marekani inabainisha kuwa mbali na njia nyingine za kisayansi na zile za asili zilizothibitishwa ikiwemo matumizi ya kalenda lakini wanataja njia ya dharura ya kuzuia mimba iwapo hukutumia hizo njia za awali wakati unashiriki tendo kuwa ni matumizi ya kijiti cha shaba (Copper IUD) ama vidonge.
CDC licha ya kutoa mapendekezo haya lakini pia wanaonya kuwa njia hizo hazipaswi kufanywa kuwa za mara kwa mara bali ni za dharura tu na hupaswa kutumiwa hadi ndani ya siku tano baada ya tendo kulingana na dawa husika.
Ufuatiliaji wa JamiiCheck kwa Wataaalamu wa Afya pamoja na Machapisho ya Kisayansi umebaini kuwa Dawa za Postinor-2 huwa na Homoni zinazofanya kazi kwa kuzuia yai kutolewa (Ovulation) au kuzuia mbegu za Kiume kurutubisha yai tofauti na majivu ambayo hayana homoni wala kemikali yoyote yenye uwezo wa kufanya kazi hiyo, hivyo hayawezi kuzuia Mimba.
Aidha, baadhi ya majivu yanaweza kuwa yamepatikana kwa kuunguza miti yenye sumu hivyo kuwa hatari kwa afya ikiwemo kusababisha Kuharisha pamoja na kuharibika kwa Ini na Figo.
Mfuko wa Umoja wa idadi ya watu wa kimataifa (UNFPA) inaonya kuhusu matumizi ambayo ni hatari kwa kutumia kama njia ya kuzuia mimba ikiwemo
- Vinegar
- Maji na Sabuni
- Sabuni ya kufulia
- Sabuni (dawa) za kuzuia bakteria
- Maziwa na Iodine
- Coca-Cola
- Pombe
- Alum
- Vipande (selesi) vya limao
- Manjano
- Tangawizi
- Makokwa ya maembe
- Mifuko ya plastiki
- Kifungashio chenye barafu
- Maputo
- Kondomu mbili
- Madodoki (Sponji) ya kuoshea vyombo
- Kuvusha muda wa kunyonyesha
- Kuruka
- Uterine Massage
- Maombi