Salamu,
Nimejiuliza sana lakini sijapata majibu. Ni nini kikwazo kinachoifanya serikali yetu ishindwe kuboresha kilimo kwa kutumia maji ya maziwa tuliyonayo kama Ziwa Tanganyika, Victoria, Rukwa, Nyasa n.k kwa kilimo cha umwagiliaji??
Nionavyo mimi ni aibu kwa Taifa la Tanzania kukosa miradi mikubwa ya kilimo cha umwagiliaji na wakati mwingine kulia njaa wakati tunazungukwa na maziwa makuu.
Kama serikali yetu inakusudia kupambana na upungufu wa chakula na umasikini kutoka moyoni ,kipaumbele cha kwanza ingekua kilimo. Kilimo kinategemewa na zaidi ya 75% ya watanzania wote. Hivyo, kuboresha kilimo maana yake ni kuinua uchumi wa watanzania walio wengi.
Kilimo kikiboreshwa kitazalisha mamilioni ya ajira na pia kuchochea uanzishwaji wa viwanda. Viwanda vingi hutegemea malighafi za kilimo, tunawezaje kufikia Tanzania ya viwanda kama kilimo hakipewi kipaumbele?
Inashindikaje kuanzisha miradi ya umwagiliaji mikubwa inayoendeshwa na wananchi kwa kila mkoa unaopakana na ziwa?
Kwa mfano ziwa Tanganyika linapakana na mikoa inayoongoza kwa kuzalisha chakula ambayo ni Rukwa, Katavi na Kigoma. Ziwa Nyasa hupakana na Mbeya na Ruvuma. Mikoa yote hii inaongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula hapa Tanzania na kwa sasa baadhi ya maeneo yake yamepunguza uzalishaji kutokana na uhafifu wa mvua.
Kwanini tuendelee kutegemea mvua peke yake?
Tuna mikoa 8 inayopakana na maziwa makuu ambayo ni Katavi, Rukwa, Kigoma, Mbeya, Ruvuma, Mara ,Kagera na Mwanza. Endapo kila mkoa unaopakana na ziwa ukiwa na mradi wa umwagiliaji walau kwa eneo linalolimika lenye eneo la kilometa za mraba 1000 tu tutakuwa na eneo la umwagiliaji lipatalo kilometa za mraba 8000. Je, kwa miradi hiyo bado tutalia na upungufu wa chakula?
Kuna wakati nadiriki kusema viongozi wa nchi hii wengi ni wanafiki na hawana nia ya kumkomboa mtanzania masikini.
Jiulize kwanini mbegu bora, miche bora itokanayo na tafiti pamoja na namna bora ya kulima inayovumbuliwa na Taasisi kama SUA na Uyole Mbeya hazienezwi kwa mkazo kwa wakulima huko vijinini?
Vumbuzi hizo zimekuwa zikioneshwa kwenye maonesho ya nanenane utadhani huko ndiko wakulima waliko.
Ukihudhuria shamba darasa linaloendeshwa kijijini na maafisa ugani limejaa hadithi za kumtamanisha mkulima na kumtia matumaini ambayo hayapo.
Afisa ugani anakushauri ulime maembe ya kisasa lakini miche anakuambia uifuate SUA!!Mkulima yupo Mpanda huko mashambani kabisa unamwabia asafiri kilometa 1000 kufuata miche ya maembe wakati yeye ni fukara wa kutupwa.
Kwanini serikali isianzishe Taasisi za utafiti wa kilimo sehemu nyingi zaidi au hata kufungua vituo vya usambazaji ambako mbegu na miche ya kisasa itapatika bila mkulima kusafiri umbali mrefu ili kila mtu amudu kupata miche na mbegu bora huko aliko?
Kinachohitajika ni maamuzi na kuweka kipaumbele katika kilimo .Hili likifanyika hutasikia Tanzania ikilia njaa na hata wasomi hawatalia ukosefu wa ajira kwa kuwa mazingira ya kujiajiri yatakuwepo.
Karibuni kwa maboresho.