Je, ni kwanini JPM hajapiga marufuku uagizaji wa mitumba?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
38,875
44,926
Ni kama tulivyozuia sukari used toka nje, hivyo hivyo tuzuie nguo used toka nje. Hii itafufua viwanda na kutengeneza ajira pamoja na kuwapa wakulima wa pamba soko la ndani la uhakika. Vp bulldozer..?!
 
hapana, viwanda vyetu bado havina ufanisi wa kutosha
nguo za mtumba zinauzwa bei rahis sana, viwanda vyetu kuzalisha nguo za kutosha halafu ziuzwe kwa bei rahisi vile ni haiwezekani kwa sasa hivi
 
Havina ufanisi kwa sababu having soko. Let's break this vicious cycle

swala la ufanisi linaanzia kwenye kuboresha teknolojia yako ya uzalishaji na kuwa na wataalamu wa kutosha,

then unapanua scale yako ya uzalishaji

ukiona sasa unaweza kuzalisha na ku cover mahitaji yote ya watanzania, haitakiwi upige marufuku utapandisha kodi kwa nguo zinazotoka nje, zikifika zinakua na bei kubwa kuliko zile za ndani, zitakosa soko na uingizaji wake utakua mdogo
 
Zipigwe marufuku kwanza ndio tutapata uwezo Wa kuboresha huo ufanisi.najua umenielewa hata Kama hutaki kunielewa
 
Ni kama tulivyozuia sukari used toka nje, hivyo hivyo tuzuie nguo used toka nje. Hii itafufua viwanda na kutengeneza ajira pamoja na kuwapa wakulima wa pamba soko la ndani la uhakika. Vp bulldozer..?!
Mbona umeenda mbali? Kwa nini usiulize ni lini ataacha madiwani wamchague meya wanaemtaka badala ya kutumia upuuzi wa kijinga wa kuhahirisha uchaguzi? Tunahitaji kuziondoa hizi tongo tongo za kibabe ili tuweze kupanga na kuchagua kihalali maisha yetu tuyatakayo sio kama wanavyotaka madhalimu!
 
kabla ya mitumba kuna toohpick, furniture, vitunguu, ngano, nyanya, mchele n.k ambavyo tunatoa nje, hivi ndio vitu ambavyo tukijikaza angalau tunaweza tukajitosheleza wenyewe na tusihitaji vya nje

ila sio mitumba
 
Ni kama tulivyozuia sukari used toka nje, hivyo hivyo tuzuie nguo used toka nje. Hii itafufua viwanda na kutengeneza ajir
a pamoja na kuwapa wakulima wa pa

mba soko la ndani la uhakika. Vp bulldozer..?!

Una hoja nzuri kabisa lakini tofauti na
viwanda vya sukari ambavyo vipo vinafanya kazi lakini vilikuwa vinaathiriwa na uingizwaji wa sukari ya magendo isiyolipiwa kodi; viwanda vya nguo vingi ama vimekufa kabisa au vimebadilishwa matumizi na kufanywa magodown kwa hiyo akiziba mwanya wa mitumba kabla viwanda havijafikia uzalishaji wa kuridhisha kuna hatari ya wananchi wetu wengi kutembea uchi! Yes kuna haja ya kuchukua hatua mtambuka kuelekea huko; japo mitumba sio rahisi sana kuizuia kabisa hata kama viwanda vinafanya kazi @ full capacity kwani kama mitumba leo hii inauzwa Paris katika masoko yale ya underground na kwingineko; je kuna tatizo la viwanda huko au ni utashi wa mlaji na nguvu ya soko?!
 
Wakati tunaendelea na mchakato wa kuongeza ufanisi wa viwanda.., nguo mpya ziruhusiwe kwa kipindi hicho cha mpito, ila mitumba ipigwe marufuku in the process
 
  • Thanks
Reactions: MTK
hapana, viwanda vyetu bado havina ufanisi wa kutosha
nguo za mtumba zinauzwa bei rahis sana, viwanda vyetu kuzalisha nguo za kutosha halafu ziuzwe kwa bei rahisi vile ni haiwezekani kwa sasa hivi
Hilo uliloliona katika nguo za mtumba lipo pia ktk sukari kabla JPM ya kuzuia sukari kutaka nje kiloba cha sukari cha kg 25 kilikua kinauzwa kwa Tsh 41500 na sasa kinauzwa kwa Tsh 49000 na huu na mwanzo tu kwakua bado kwenye magulio haijaisha hadi kufikia Apr bei itakua za idi ya hiyo
 
...hivyo viwanda vya nguo vilivyopo vilikuwa vinatengeneza vitambaa aina ya merekani vigumu kweli, viatu kulikuwa na asante mpare,
it were only khanga made in standards.
 
Wakati tunaendelea na mchakato wa kuongeza ufanisi wa viwanda.., nguo mpya ziruhusiwe kwa kipindi hicho cha mpito, ila mitumba ipigwe marufuku in the process

Kwa sababu za uchumi duni wa wengi wa wananchi wetu ni lazima kuwapa dirisha la kukimbilia; penye bei nafuu na wepesi wa upatikanaji maana mitumba inatembezwa mpaka maofisini na majumbani kitaaa! Tuwajali watu wetu jamani tuache mitazamo na mienendo ya kVasco da Gama; if you get what I mean!! Asante
 
Lazima watu waumie ili tusonge mbele. Hakuna namna!
 
Mmmmh bora azuie nguo za China kuliko Mitumba, mnataka watu wavae disposable clothings?
 
hujafikiri kuwa atakpositisha uingizaji wa mitumba watu wangapi watakosa ajira mpaka kiwanda kizalishe ni leo?
 
Back
Top Bottom