Je, ni kipi kipimo sahihi cha ubaya?

Msonjo

JF-Expert Member
Oct 13, 2019
1,308
2,224
Salaam

Wanajamvi poleni na mihangaiko ya hapa na pale.

Naomba kuuliza, hivi ni kipi kipimo sahihi cha ubaya ?

Kwa sababu wakati mwingine ubaya wa kitu si kutokana na kitu chenyewe kuwa kibaya.Bali ni mtazamo tu wa mtu kwa vile anavyokiona hicho kitu.

Kwa mfano mtu anaweza akesema chakula hiki ni kibaya, lakini kumbe si kweli kwamba chakula ni kibaya bali ni mdomo wake tu umepoteza ladha Kwa kuwa alikuwa na homa basi anakiona kibaya.

Au mjamzito anaweza akasema manukato(perfume) haya yananuka vibaya, lakini sio kweli kuwa yananuka vibaya ila hali yake tu ndio inamfanya ayaone hivyo.

Kwenye jamii, mtu anaweza kusema fulani ni mbaya, lakini kumbe huyo fulani si mbaya ila kwa kuwa tu yeye hampendi basi anamuona mbaya.

Kwenye siasa, kuna hawa jamaa wanao muita kiongozi wa nchi jiwe, wanasema jiwe mbaya, lakini huwenda jiwe sio mbaya, ila kwa kuwa ni mpinzani wao basi wanamuona mbaya.

Na hawa wa chama tawala nao, wanasema upinzani wabaya lakini huwenda upinzani sio wabaya, ila kwa sababu ni wapinzani wao basi ni wabaya.

Kuna mmoja alianzisha Uzi akisema daslama mbaya, lakini daslama si mbaya ila kwa kuwa yeye ametokea sitimbi basi anaiona dar mbaya.

Sasa ikiwa kauli ya mtu/mtazamo wa mtu hautoshi kuhukumu kuwa kitu/mtu fulani ni kibaya. Kwa sababu inaweza ikawa imeegemea katika chuki, mapenzi, itikadi, hisia zozote n.k

Basi ni kipi kipimo sahihi cha ubaya wa kitu?
 
Uzuri wa suraa unapimwa kwa golden ratio sura ikiwa symmetry ina kuwa attractive ila ivo zingine in a depend na malezi,sehemu MTU aliyokulia ko haina kipimo
 
Kipimo sahihi cha ubaya ni ubaya wenyewe kwa sababu anaeujua ubaya ni roho yako. Hakuna ubaya mkubwa wal mdogo.
kipimo ni kimoja tuu


Tujifunze kuishi na Corona kama Ukimwi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom