Mkuu kuna mambo mengi sana yanafanyika nje ya matakwa ya katiba ambavyo ni sheria mama. Kuna maamuzi mengi yanafanywa kwa ajiñi tu ya kutaka kulinda maslahi binafsi ya kikundi kidogo cha watawala badala ya yale ya umma mzima wa Watanzania..
Yapo maamuzi yaliyojaa utata mwingu yanafanyika kwa kisingizio cha amri kutoka juu. Watawala wanajipa majukumu ambayo hata hayajahainishwa popote pale ndani ya vifungu vya katiba. Ukimya wa katiba iliyopo katika mambo mengi ya msingi na yaliyopitwa na wakati, ama mapya yanayopaswa kuwekwa kuendana na matakwa ya wakati, yanaipa mwanya serikali kujifanyia shughuli zake kwa mazoea, hisia na mihemko badala ya uhalisia, umakini na tija.
Mathalani, katika sakata la DPW tuliliona Bunge linajipa jukumu jipya na la ziada kutoa elimu kwa umma ili liweze kushawishi watu badala ya jukumu lake la msingi katika kuisimamia na kuishauri serikali. Aidha, tunashuhudia hivi sasa kuna takwa la wakati la hitaji la uwepo wa katiba mpya, lakini badala yake tunaishuhudia serikali ikijipa jukumu jipya la kutaka kuelimisha wananchi ili eti wailewe vyema katiba!
Hakuna anayejali kuhusu gharama kubwa iliyokwisha kutumika katika mchakato wa awali wa rasimu ya Warioba. Kuna mgogoro mkubwa sana wa kifikra, kimaudhui na kimantiki kutokana na akili ndogo kutawala akili kubwa.