Katika kongamano la kumuenzi mwalimu lililofanyika kule Kivukoni alitambulishwa mzee mmoja silikumbuki vizuri jina lake lakini linaelekea kama KASOLI vile; huyu mzee alitoa ushuhuda jinsi alivyofanya kazi karibu sana na marehemu mwalimu na kutoa ushuhuda kwamba mwalimu siku zake za mwisho alihuzunishwa kwamba hakupata muda wa kutosha kuwa karibu na watoto wake. Mzee Kasoli akatoa rai kuwa lingekuwa jambo la busara kama warithi wake wangewasaidia hawa watoto!!
Mimi ninavyofahamu ni kwamba mjane wa mwalimu anatunzwa na serikali kutokana na kodi za wananchi. Hao watoto wa mwalimu ambao wanatakiwa wasaidiwe ni watoto gani? Watoto mwa mwalimu kama sijakosea ni watu wazima sasa ambao pengine wana wajukuu, mtoto wake wa kwanza wa kiume inawezekana ana umri wa miaka 60 hivi ssa. Je , kweli ni jukumu la serikali kuwalea watu wazima na wajukuu simply because thy carry the Nyerere name? Hata hivyo Rais Mstaafu Mkapa alijitahidi sana kuwabeba hata akamteua Rosemary kuwa mbunge! Makongoro alikuwa mweneyekiti wa CCM wa mkoa wa Mara na baadae kuwa mbunge wa Afrika Mashariki.
Tukumbuke tu kwamba mwalimu alipokuwa anang'atuka alipewa zawadi nyingi sana na wananchi ambazo kama hawa vijana wake wangekuwa ni watu serious mali zile zingweza kuwasaidia wao na vizazi vyao. Sasa sijui kama zile mali zipo au hakuna aliyeshuhulika kuzitunza hivyo kutapanywa hovyo! Sio mwalimu tu bali hata mama Maria Nyerere alikuwa na viwanja vingi uko Mikocheni na Mbezi beach ambako wakati fulani alijaribu kufuga kuku; vile viwanja vipo na inaelekea hakuna mtoto yeyote anayeshuhulika kumsaidia mama yao kuvitunza kwani kwa mfano kiwanja kilichopo Mbezi beach kimegeuka pango na wahalifu wanaouza madawa na kuvunja nyumba za watu na kuiba.
I believe kuwa kila tukio lina sababu zake , inawezekana kushindwa kwa Makongoro kupata ubunge wa Afrika Mashsriki kunaweza kumpa muda wa kumsaidia mama yao kusimamia mali zao na hivyo kuwasitili ukoo wa mwalimu ambao kisheria hawahudumiwi na serikali.