Je ni halali wananchi kugharamia dizeli magari ya polisi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni halali wananchi kugharamia dizeli magari ya polisi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Luteni, Jan 26, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kwenye miaka ya 80 wakati Mrema alikuwa waziri wa Mambo ya ndani wananchi walikuwa wakijitolea kujenga vituo vya polisi maarufu kama Polisi Post ili kuimarisha usalama kwenye maeneo yao lakini je hili la kuchangishwa kugharamia dizeli ya magari ya polisi limekaaje....waheshimiwa nawasilisha hoja.

  Hebu soma habari hii ya leo bungeni..


  WIZARA ya Mambo ya Ndani imesema, si sahihi kwa wananchi kununua dizeli na matairi ya magari ya polisi.

  Hata hivyo, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Balozi Hamisi Kagasheki, amelieleza Bunge leo kuwa, si vizuri kueleza hadharani udhaifu wa jeshi la polisi.

  Kagasheki ametoa msimamo huo bungeni mjini Dodoma baada ya Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai, kudai kuwa, wananchi jimboni humo wametakiwa kutoa fedha za kununua mafuta ya dizeli kwa ajili ya magari ya polisi, na za kununulia matairi ya vyombo hivyo vya usafiri.

  Kwa mujibu wa Mbunge huyo, wananchi hao pia wamejenga kituo cha polisi, wamejenga nyumba ya Mkuu wa Kituo hicho, na pia wamenunua samani za kituo hicho.

  Mkuu wa Kambi ya upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed, alipinga kauli ya Kagasheki ya kupinga kusema hadharani udhaifu wa polisi.

  Rashid amewaeleza wabunge kuwa, suala hilo si siri kwa kuwa lipo hata kwenye taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

  Awali, Balozi Kagasheki aliwaeleza wabunge kuwa, Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kushirikiana na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wana mpango wa kujenga vituo vya polisi na nyumba za kuishi askari katika kata ili kusogeza huduma za jeshi hilo karibu na wananchi.

  Bunge limeelezwa kuwa, hadi sasa kuna vituo vya polisi 146 vya wilaya, 493 vya tarafa, na vituo 2,068 vya kata.

  SOURCE: Gazeti la Habari Leo
   
 2. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145

  Hivi jamani hawa wabunge wetu hawafahamu hali za maisha wanayoishi polisi wetu huko uraiani? Mbona wanauliza maswali ambayo hayana msingi ishu si kununua petroli au dizeli ishu ni kuboreshwa hali ya maisha ya askari wetu.
   
Loading...