Je! Ni DAWASCO au mwenye nyumba?

Je! Ni DAWASCO au mwenye nyumba?

Mildred

Member
Joined
Nov 28, 2012
Posts
91
Reaction score
16
Habari zenu wana JF.

Jamani, nimepanga nyumba moja hapa Dar toka January, lakini cha kusikitisha ni kwamba Bill ya maji inayokuja kwetu imekuwa majanga sasa kwa miezi mitatu. Mwezi wa kwanza bili ilikuja elfu 70, mwezi wa pili ikaja elfu 60 na mwezi huu umekuja elfu 80. Mwezi uliyopita tulienda DAWASCO kuuliza kwanini tunalipa bili kubwa hivi wakasema ni matumizi yetu.

Ila kiukweli ni kwamba, tuko wapangaji watatu tu na wote tunafunga milango asubuhi tunapoenda kazini sasa inakuwaje matumizi yanakuwa hivi. Pliz wadau naombeni msaada tufanye nini au ni kwa sababu gani bili yetu inakuwa kubwa kiasi hicho?

Je ni bili yetu au tunapewa bili ya mteja mwingine? Kumbuka pale sisi wote ni single ila moja tu ana mfanyakazi, wengine hatuna. Je tatizo ni nini? Michango yenu ndio ukombozi wetu jamani labda kuna mwingine/wengine wanapata shida kama hii ya kwetu.

NOTE: Tumeuliza mwenye nyumba kama labda alikuwa na bili nyuma akasema kuwa ali clear kabla hatujapanga kwake.

Mchango wenu tafadhali.
 
ombeni wawafungie mita ukiwa na mita itakuonyesha matumizi sahihi ya maji unayotumia mara nyingi bill za kukadiria huwa zina matatizo
 
Asante kwa mchango wako ila kuna mita tayari.

jifunze kusoma mita nakumbuka kuna siku ililetwa bill ya 120000 badala ya 9900 kilichosaidia ninafahamu kusoma mita hivyo nikachukua bill waliyoleta nikasoma kiwango kilichotumika kisha nikawaliza kila unit moja ni bei gani.tukafanya hesabu.
walipoona nimeshtuka wakaanza kujikanyaga eti no typing errors.
 
Asante sana nitaomba msaada kwa wale wanaojua wanielekeze.
 
Hili jambo la msingi sana

Unaweza kuta mnapigwa kila mwezi





jifunze kusoma mita nakumbuka kuna siku ililetwa bill ya 120000 badala ya 9900 kilichosaidia ninafahamu kusoma mita hivyo nikachukua bill waliyoleta nikasoma kiwango kilichotumika kisha nikawaliza kila unit moja ni bei gani.tukafanya hesabu.
walipoona nimeshtuka wakaanza kujikanyaga eti no typing errors.

Pia huyo mfanyakazi mchunguzeni isijekuwa anafanya biashara ya maji hapo
 
kutakuwa na likeji ya maji baada ya mita,..mabomba yana tabia ya kupasuka na kuvujisha maji hasahasa mabomba ya chuma huliwa na kutu,kuna wakati ilinigharimu kuvunja floor ya jiko baada ya kuletewa bili ya laki mbili kwa miez mitatu mfululizo....
 
Mkuu cheki mita hiyo itakua nashida haiwezekani labda mkitoka watu wanaingiza mpira wanajaza matank yao fatilia kwanza
 
Asante sana mdau, kama kuna leakage lazima mita izunguke, jana usiku tulifungua mita sisi na mwenye nyumba lakini tukakuta mita haitembei tulipofungua maji ikawa inatembea for that nafikiri hakuna leakage yeyote.
 
pale kwetu kuna geti tena kuna mfanyakazi moja tu ambaye tunaamini hawezi kufanya hivyo kipindi hatupo bado ni mdogo.
 
Back
Top Bottom