Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Mambo ya real estate ni magumu sana kama endapo hutakuwa na uelewa nayo,kumiliki nyumba au kujenga nyumba ili upange ni jambo jema na zuri endapo utafata vigezo stahiki.mfano unaweza ukaamua kufanya hivyo ukawa unapangisha huku unatumia hiyohiyo nyumba yako kama security( kuombea mkopo), mbili uneweza ukaamua kufanya hivyo utakuwa umesave time ya wewe kufanya mambo mengine kwa maana nyumba hiyo itakuwa inakuingizia wewe pesa bila wewe kuifanyia kazi (money work for you= you never work for money) kwa hivyo utakuwa umesave time na kufanya mambo mengine. Tatu kufanya hivyo utakuwa upo kwenye risk ndogo ya kupoteza mtaji wako kiasi kama sio wote.4 kufanya hivyo utakuwa umeingia katika ulimwengu wa financial freedom. Ila angalizo kama nilivyosema mwanzo mambo ya real estate ni magumu sana kama endapo utakuwa huna uelewa nayo, sasa ili kufanikiwa kaatika any types of real estate/investment yeyote inakupasa kupita kwenye steg hizi tatu...

1.Elimu kuhusu real estate(uwekezaji katika nyumba au viwanya)
2.Uzoefu
3.BOOM!!!! Ongezeko la kipato
Kwa wale wanaoogopa biashara ya real estate niwadokeze tu Tajiri na billionaire wa kwanza wa babilon ametokea kwenye hii biashara ya real estate.
 
Nimesoma comments za huyo laki si pesa kwenye uzi huu mojawapo ni comment inayosema "wahindi wana hela za majini" nimechoka alafu ni gamba mwenzio. Zero brain
Bila shaka unataka kukalia fupi nene wewe na huyo Gamba mwenzako.
 
Unachosahau ni kuwa baada ya miaka 29 lazima uwe umefanya ukarabati mara kadhaa (ikiwemo kubadilisha paa, nyaya za umeme na design kadhaa za nyumba. Pia, design za miaka hiyo usidhanie utampangisha mpangaji wa maana zaidi ya wanachuo na mateja
Sawa, lakin wajua zile nyumba za NHC za Kariakoo, Ubungo na kwingineko zina zaid ya miaka 40? Ni wangapi wana uwezo wa kumudu nyumba ya NHC Kariakoo pamoja na muonekano wake wa kizaman? Kinachozifanya ziendelee 'kuuza' ni prime location. Baada ya miaka 29, hata kinzudi itakuwa prime location, kama vile Sinza ilivyokuwa mashamba ya mpunga miaka 30 iliyopita.
 
Sawa, lakin wajua zile nyumba za NHC za Kariakoo, Ubungo na kwingineko zina zaid ya miaka 40? Ni wangapi wana uwezo wa kumudu nyumba ya NHC Kariakoo pamoja na muonekano wake wa kizaman? Kinachozifanya ziendelee 'kuuza' ni prime location. Baada ya miaka 29, hata kinzudi itakuwa prime location, kama vile Sinza ilivyokuwa mashamba ya mpunga miaka 30 iliyopita.
Future ni unpredictable ndugu. Nani alijua kuwa fremu za biashara kariakoo zitakuwa obsolete miaka ya hv Karibuni? Watu walikwenda na upepo wa bandari mpya ya Bagamoyo wakanunua Maeneo huko Mlingotini na njia ya Msata kiko wapi?
 
Business kwa mazingira yetu sio guarantee, lakini pia ujenzi wa nyumba kusastain maisha yako ya kila siku nayo ni changamoto kama huna mtaji mkubwa..

Baadala ya kujenga nyumba for 100 -150mil kwa maana ya biashara ni bora ukawa na shamba la minazi au miti la 20heka for 5yrs ambayo itakugharimu labda 20mil na baada ya hapo unaanza kuuza nazi miaka nenda rudi.... Ukanunua mchele au Mpunga na mahindi ukauza sehemu mbalimbali just to sustain your daily life.. Hapo utakuwa umeinvest labda 50mil na 100mil unapigilia fixed ambayo utakupa 8mil/year...

Ujenzi wa nyumba wakati mwingine ni kama uoga wa maisha maana 150mil inaweza yenyewe ikajenga nyumba ya 150mil for 5yrs na maisha mengine yakaendelea...
ONYO NA TAHADHARI : usiingie kwenye biashara na 150mil kama hukuwahi kufanya biashara, you will only be safe kwa kufanya biashara ambazo ni risk free kama daladala au ujenzi wa nyumba..

150mil inaweza kununua 3coaster zikawa daladala mjini .. Hesabu 100k mpaka 80k ukichukua 80k x 30 x 3 = 7.2month.. Assume ubovu wa gari, service, mabao, mizinguo ya dereva na konda kwenye hesabu, laza 4mil monthly kula 2mil/month weka akiba 2mil/month yearly utakuwa na 24mil ukienda 3years itakuwa 72mil uza zote kwa 25x3 = 75mil vuta nyingine tatu and the circle continue life goes on.
Tatizo uoga umetutawala sana kitu kitakacho kutoa kimaisha ndo umakiogopa kukifanya
 
Future ni unpredictable ndugu. Nani alijua kuwa fremu za biashara kariakoo zitakuwa obsolete miaka ya hv Karibuni? Watu walikwenda na upepo wa bandari mpya ya Bagamoyo wakanunua Maeneo huko Mlingotini na njia ya Msata kiko wapi?
Case ya Kariakoo ni very unique and rare. Wote hapa tunajua nan kavuruga uchumi wa nchi na kupelekea hali hiyo, sema tu tunaogopa kumtaja. Ndo hapo utajua biashara ni siasa. So kuwa na imani, hii hali itabadilika 2026.
 
Waheshimiwa

Kuna jambo moja ambalo watu wengi wamekua wanalikosea bila kujua. Kwa maoni yangu:
Ni muhimu kuelewa tofauti kati ya business na investments
Ni muhimu kuzingatia suala la return on investment au Retun on Asset wakati wowote unapofanya investment au biashara. Usipozingatia haya utasema huna bahati au unalogwa. Utakua frasturated na kuchukia biashara. Mfano


Mimi na wewe tunaweza kuchukua mkopo wa million 100, tukafungua biashara tofauti. Wewe ukawa unapata faida kubwa kwa haraka kuliko mimi. Au Wewe unaweza kuanzisha biashara ambayo ni capital intensive mimi nikaanzisha biashara ambayo sio capital intensive (haihitaji mtaji mkubwa). Au wewe unaweza ukafungua biashara yenye matumizi mengi / higher expenses kama daladala/ malori kuliko mimi. Au wewe unaweza ukafungua biashara yenye risk kubwa kuliko mimi kama vile daladala zinazopata ajali kila mara nk. Au wewe unaweza kufungua bishara yenye mzunguko mkubwa wa mauzo kuliko mimi. Yote haya yataamua nani atafanikiwa kuliko mwengine baina yetu

Wakati mwengine hata structure ya biashara inaweza kuamua nani anafanikiwa kuliko mwengine. mimi na wewe wote tunaweza kuanzisha biashara inayofanana lakini tukatofautiana katika structure ya management au operations na hapo mmoja akafanikiwa kuliko mwengine. Kwamfano wote tunaweza tukanunua bajaji kwa million 6 wewe ukaingia mkataba na dereva awe anakuletea kiasi fulani mpaka itakapofika million 10 then bajaji itakua yake. Mimi nikaweka dereva tu akawa analeta hesabu na hapo mmoja wetu akafanikiwa kuliko mwengine.

Wakati mwengine usimamizi tu unaweza kuleta tofauti kubwa sana. Wewe unaweza ukawa na Lori lako liko kijijini kwenu huko kaka zako wanasimamia na mimi nna Lori langu liko hapa Dar nasimamia mwenyewe au wote tunaweza kua na Fuso ziko dar lakini wewe ukapata dereva mwenye nidhamu mimi nikapata dereva asie mwaminifu na hapo tukapata matokeo tofauti kabisa

Tofauti hizi nyingi ndogo ndogo za kiufundi hua zinaleta matokeo tofautisana katika biashara na ni mambo ya kuzingatia kama unataka ufanikiwe kibiashara. ndio maana wewe unaweza ukawa na Daladala likakushinda ukauza mwenzako akanunua hioihilo akaa nalo miaka 10 ukabaki unashangaa

Kingine ni uvumilivu na kujifunza. Ukiwa na biashara na haiendi vizuri jitahidi kuvumilia na kujifunza na kurekebisha mapungufu yako katika biashara. Uyarekebishe na kuendelea. usiruke ruke na kuanzisha biashara mpya kila mwaka

Kingine Muhimu ni kuandika mapato na matumizi yote katika biashara yako ili baada ya mwaka au miaka 2 uweze kufanya tathimini na kuamua kama uendelee au la.

Mwisho nimalizie na mfano ulioko kwenye kichwa cha habari ya bandiko hili - case study. Nimekutana na rafiki zangu kama 4 ambao wanajilaumu kwa uamuzi wao wa kujenga nyumba na kuanza kukusanya kodi. Wamekuja kugundua baadae kua faida hua ni ndogo na inachukua muda mrefu sana kupata - inachukua zaidi ya miaka 20 kubreak even na kuanza kupata real profit. Yuko mmoja ameachiwa nyumba ya urithi na anasema anatamani angeweza kuuza na hizo fedha akaingiza kwenye biashara nyingine yenye high and quick return - familia haiwezi kumruhusu. Nyumba haimpi faida yoyote ya maana tena ni kubwa mno na wapangaji hamna. Yuko mwengine yeye alichukua mortgage kama million 200 pamoja na wife wakajenga nyumba. Wamekaa wamepiga hesabu na kugundua watakapomaliza kulipa baada ya miaka kama 15 watakua wamelipa kama million 400 kwa mbinde maana malipo ya mwezi ni zaid ya million 1 ambayo inawatesa sana kwasasa. Wanajilaumu. Kwamfano: ukijenga nyumba kwa million 150 na kuanza kukusanya kodi ya 600,00 kwa mwezi itachukua miaka 21 kuweza kukusanya kodi ya million 150. Kama unajenga nyumba ya kuishi ni sahihi lakini nyumba kama biashara it might be a challenge. Furthermore, kama una million 150 wapo wanaodhani unaweza kuiingiza kwenye biashara kisha ukatumia faida ya hiyo biashara kujenga nyumba polepole

Tupe maoni yako, tujadiliane, tubadilishane mawazo, tufundishane

Ukiwa unapokwa hiyo 600.000 at the same time land and property Ina appreciate in Value! Mi nimefanya biashara, nimefanikiwa, ila ikiamua kukukata Inakata kweli ~

Ukiweka 150m kwenye nyumba, na kuwa unakula 600.000 kwa mwezi in 10 years that house and land can have a value of 300m
 
Case ya Kariakoo ni very unique and rare. Wote hapa tunajua nan kavuruga uchumi wa nchi na kupelekea hali hiyo, sema tu tunaogopa kumtaja. Ndo hapo utajua biashara ni siasa. So kuwa na imani, hii hali itabadilika 2026.
2019-2026 tunaishije? Hapo ndio ujue Real estate/Property business kwa Tanzania ni kujiletea umaskini
 
Biashara hua haipo hivyo hakuna biashara ya kusema mwezi mzima ninaweza kujaza vyumba viwe full sana sana utajaza nusu vyumba..robo etc biashara hua haipo constant kiivyo..hapo hujapiga hesabu ya kuibiwa hata vyumba vikiwa full utaletewa i.em watu watano au 10 ndo walilala
... assumption boss. Hata kama vikijaa robo tu kwa mwezi mzima bado inalipa kuliko nyumba ya kupangisha kwa mwezi.
 
Ukiwa unapokwa hiyo 600.000 at the same time land and property Ina appreciate in Value! Mi nimefanya biashara, nimefanikiwa, ila ikiamua kukukata Inakata kweli ~

Ukiweka 150m kwenye nyumba, na kuwa unakula 600.000 kwa mwezi in 10 years that house and land can have a value of 300m
Unaishi nchi gani ndugu? Tembelea viwanja Goba,Mbweni, Bunju uone maajabu ya maporomoko ya bei
 
Unaishi nchi gani ndugu? Tembelea viwanja Goba,Mbweni, Bunju uone maajabu ya maporomoko ya bei

Kwa mda Huu kila kitu kimeporomoka, na biashara ndio zaidi kabisa, but msimu mgumu ukipita investment ya nyumba will last!

Sisemi watu wasifanye biashara, ila kuna factors nyingi sana kuwa considered kwenye biashara!

Kama is a inject hiyo 150m kwa biashara ya mda yenye faida tayari sawa, ila kama ndo unainza utaanguka ~ ukifaulu ni bahati sana
 
2019-2026 tunaishije? Hapo ndio ujue Real estate/Property business kwa Tanzania ni kujiletea umaskini
Tuwe wakweli, biashara zote halali bongo zimeyumba sana. Hivyo kuja wakat you just need to survive, to just be operational. Ukipigwa na dhoruba na uko katikati ya bahari, usijitie ujuaji wa kutaka kuogelea ufike ufukweni, just keep yourself afloat and wait for rescue.
Mimi nazielewa sana hoja za upande wako. Ila natambua udhaifu wa wengi. Hawana financial literacy. Sio wajasiliamali. Sio wachaga, wakinga, wapemba au wahindi ambao wana fursa ya kupata informal education ya biashara. Hawa wanahitaji biashara ambayo haihitaji micromanagement. Tukitaka kuwadaidia tuwaelekeze biashara mbadala.
 
Uwekezaji kwenye real estate, shares au Treasury bill una faida mbili (1) Ni return on investment (2) Appreciation in value of investment. Nyumba kama nyumba utaona hiyo kodi ya TZS 600,000 ni ndogo sana lakini ukiuza hiyo nyumba utapata zaidi mfano hiyo nyumba ya TZS 150,000,000 unaweza ukauza TZS 300,000,000.

Kwa wale tunaowekeza kwa ajili ya elimu ya watoto wetu; bado kuwekeza kwenye nyumba ni bora zaidi kuliko "Fixed deposit" kwani wakati nyumba ikiongezeka thamani kuendana na wakati, Principal amount kwenye Fixed Deposit haiongezeki thamani kinyume chake inapungua thamani (inflation).

Ushauri wangu wekeza kwenye nyumba pesa ambayo huna matumizi nayo yaani mtaji uliozidiki kwenye biashara yako na usiwekeze kwa matazamio ya kuvuna faida
Hujamuelewa labda usome kuanzia story za mwanzo hapo juuu, ukifanyia biashara 150.000.000 ndani ya miaka mitano utakuwa umeishapata zaid ya 600.000.000
 
Thread nzuri sana hapa ndio utagundua tofauti ya:
1. KUSOMA na KUELIMIKA
2. Dhana Thoughts tofauti tofauti kwa kila taaluma yaani dhana ya
accountants, Finance Managers, Economists, Entrepreneurs
3. Lugha tofauti tofaut kulingana na taaluma

Mfano mzuri accountant anakuambia Nyumba ni asset nzuri sana maana siku zote value yake ina appreciate inapanda thamani eti kunakuwa na capital gain

Finance manager , Investment analysis anasema kwenye asset kama nyumba compare capital gain na Inflation then return yake ndio utajua kama una gain or lose

Economist ataangalia Feasibility study atakuambia nyumba haina hasara.

Entreprenuer ataangalia kwanza Cashflow then Return On Investment ndio ita determine either ni Asset or Liability

Sorry sijaiweka vizuri sana lakini najaribu tu kuonyesha changamoto tullizonazo kwa wasomi wetu hawa na kila mmoja anajiona yuko sahihi sana na anadiliki kuwashauri wateja/ jamii/ kwa hizo fikra zake

Ebu kwa mfano huo hapo accountant anaamini siku zote duniani land or House inapanda thamani yaan kuna capital gain je anasahau pia kuna Inflation ?

Aisee nimefurahi sana

Sikuwahi kuliangalia hili from this point of view. You comments shows that majority of wachangiaji hapa wanaweza kuwa sahihi depending on what faculty they are looking at the matter at hand

Mimi ni muumini wa Robert Kiyosaki anaefundisha kwamba Asset is anything that brings you money/income and liability is anything that uses/spends your money. Katika mchanganua wako i am guessing mimi naangukia kwenye kundi la Entrepreneur.

Umedadavua mada in a highly intelligent fashion and your comments are highly educational. Mtazamo wako wa mambo ni mpana na mrefu tena wa tofauti
 
Back
Top Bottom