waheshimiwa maisha bila mkopo chuoni ni *magumu* sijapata kuona hasa kwa sisi watoto wa wakulima ambao tumesoma st.kayumba sec. School(ukipeleka ada elfu ishirini na tano, basi unarudishiwa na chenji elfu tano)!!.nimeunga unga maisha mwaka wa kwanza umeisha na sasa naingia mwaka wa pili.ila ninachosikitika na kutokwa machozi kila ninapokumbuka ni kwamba tangu mwaka wa jana faculty(course) yangu imebadilishwa kuwa non-priority course(haina mkopo tena) na nilitegemea kuomba tena mkopo huo mwaka huu baada ya kuukosa mwaka wa jana.!.nilijaribu kutuma maombi ya mkopo hivyo hivyo(as a point of trial) kwa kutumia admision letter zangu za mwaka jana na mpaka sasa nasubiri tu bila hata matumani na majina hayajatoka mpaka sasa!.ndugu zangu wapendwa ivi naweza kupata kweli mkopo kwa staili niliyo tumia????...au ndo nifanye elimu ndo imenishinda kwa ugumu wa maisha ninao upata kule chuoni???...au nitapata niendelee kusubiri??....nifanyaje jamani masikini mimi??? May u save me on this please guys!!.