Je Nadanganywa??? Pls nishaurini.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Nadanganywa??? Pls nishaurini..

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Boflo, Nov 4, 2010.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wana JF huyo Mdada anahitaji ushauri

  Mimi ni msichana wa miaka 29 nina elimu ya form 4 na nikasoma Secretary VETA miaka 2 pamoja na Computer n.k…Nikabahatika kupata kazi kwenye kampuni binafsi mpaka sasa hivi nina miaka 9 katika hiyo kampuni nikapandisha vyeo mbalimbali ila nafanya kwa ujuzi tu hizo kazi na sio kwa vyeti na mshahara wangu sasa hivi ni 1.million pamoja na marupurupu yote (Nimeelezea haya ili niweze pata ushauri unaofaa kwa kulinganisha kipato na hali halisi ninayoishi.) nina uhusiano na kijana mmoja hapa na nikazaa nae mtoto mmoja wa kiume ana miaka 2 sasa..tatizo kijana mwenyewe ni jeuri/dharau/hana upendo kabsaa…na kikubwa zaidi yeye ana elimu ya darasa 7 na hata ufahamu wake ni mdogo yaani kazi anayofanay ni biashara za hapa na pale elimu kwangu sio issue muhimu ni Upendo n.k Japo anaonyesha nia ya kunioa lakin mmmh NIMESHINDWA.

  Kwa bahati mbaya/nzuri nikakutana na kijana mwengine mtanzania ambae anaishi Marekani nae amezaa mtoto 1 wa kiume lakin bado hajaoa…..na ana passport ya Marekani (nimetoa hizo detailz ili mtakaponishauri mjue mnaanzia wapi) ..tulikuwa tunachat kwenye mitandao yaani tukawa tunapenda kama vile tumeonana..mpaka mwaka jana alipokuja tz tukaonana na kila mtu akaridhika na mwenzie….kwa kweli nina mpenda sana tu nay eye pia anaonyesha kunipenda…ILA TATIZO NI KWAMBA HATA NIKIWA NA SHIDA HUWA NAIELEZEA KWAKE KAMA STORY YA KAWAIDA TU ILI WALAU ASEME OK NITAKUTUMIA PESA..HASEMI WALA HAJAWAHI NISAIDIA NA NA HATA UKITAMKA PIA ANASEMA HANA…Ila hapa Dar es salaam amejenga nyumba nzuri tu amenipeleka pia kuiona n.k.

  Kilichonifanya kuwauliza....ni hili Sasa hivi anataka kunioa ila yeye ni dini nyingine lakin nilipomwambia amesema yuko tayari kubadili kuja kwenye dini yangu…Na anataka anioe na kwenda kuishi marekani na amesema atanitafutia Shule na mtoto pia atasoma n.kk…na yeye pia ni msomi na ana kazi nzuri tu, na ni mpole sana, ana busara, ni mwepesi kuomba msamaha na hapendi nikasirike hicho ndicho nilichogundua kwa miaka 2 niliyomfahamu kwa kuongea na simu na miezi 3 alokuja tz tukawa pamoja.

  1. SWALI LANGU NI HILI: JE KAMA HUYU MTU ANA UWEZO WA KUNIPELEKA U.S.A MIMI NA MTOTO NA AKATUSOMESHA SOTE IWEJE SHIDA NDOGO NDOGO TU ZA HAPA ANASHINDWA NITATULIA????? (Japo sehem kubwa ya maisha na mudu mwenyewe lakin kwasabab najenga huwa nakwama hapa na pale kibinadamu)…
  2. JE KWA MTAZAMO WENU HASA AMBAO WANAISHI U.S.A KITU KAMA HICHO KINAWEZEKANA KUMUDU MAISHA YA KUMSOMESHA MTU NA MAMA YAKE??

  3. NA KAMA HAKUFANYA AKANIDANGANYA JE NITAFANYAJE????? (Naogopa kufanya tamaa kisa nimesikia Nje baadae nikajuta).\

  4. Na kama ni kweli…ATATUMIA UTARATIBU UPI WA MIMI NA MTOTO KUISHI PALE BAADA YA VISA HALALI KWISHA??

  Niko njia panda naomba mnishauri Matusi na kejeli pia ntapokea…Ila nitashukuru kwa wale wote watakaonipa hali halisi ya maisha ya U.S.A kulingana na story yenyewe…NAKUWA NA WASIWASI SABAB KAMA NITACHEMSHA NA NIKAWA SIJAPATA CHANCE YA KUSOMA NIKIRUDI TZ NAJUA KAZI YANGU SITAIPATA TENA…NATAKA KUJUA KAMA NADANGANYWA AU HIVI VITU VINAFANANA NA UKWELI. NIKO NJIA PANDA....NAHITAJI USHAURI WA UKWELI NIFANYEJE?
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Huyu nae anadhani ughaibuni ndo kuna dili ,mwambie asiache mbachao kwa msala upitao
   
 3. E

  Edo JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Anaishi marekani, anafanya kazi kampuni gani au biashara ipi anayofanya!!!
   
 4. Enny

  Enny JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Kwanza napenda kuuliza, vipi huyo bwana mwenye mtoto mumeshaachana ? Au naye unaendelea naye ki aina? Pili, huyo bwana wa marekani ulishamuuliza anafanya kazi gani huko?
   
 5. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #5
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  yaani kuwa mwangalifu sana ... kwa kweli kama unauwezo nenda peke yako kwanza kaweke mambo sawa halafu rudi umchukue mwanae... kwani ukiwa mwenyewe itakuwa rahisi kidiogo.... na unatakiwa utumie ujanja sana ili usipoteze kazi yako ya sasa.. sema tu unachukua holiday ya miezi 3 au kitu kama hicho ... o just say is emergence ... kwa sababu hatujui Mwenyezi Mungu ametupangia nini hapa duniani labda wewe kwenda kuishi nje ndo ridhiki yako ... know one knows.... take care be caution
   
 6. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  matapeli ni wengi mwaya kuishi nje haina maana kuwa hawezi kuwa tapeli kuwa makini sana,,,huyo uliyezaa nae kinachomsumbua ni ulimbukeni na inferiority,nahisi mkifunga ndoa utakuwa umejibebesha mzigo.Tulia jipange vizuri pia muombe Mungu
   
 7. W

  Wakuchakachua JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli hapo dada ni cross roads na unahitaji ushauri, sasa wewe tulia hayo maswali uliyo yauliza hapa jitahidi kumuuliza na huyo muhusika wa marekani na kama ana busara i belive atakujibu na utapata taswira nzur, kwani sis twaweza sema ni mkweli kumbe si, ingawaje wew unaonyesha kumuamini basi ask him first then yote utayajua kutoka kwake, kumbuka nyota njema huonekana asubuhi, huyo uliezaa nae achana nae kabisa
   
 8. mdoe

  mdoe JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 436
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wapige chini wote, Tulia chini ufikirie jinsi ya kumlea mwanao na umtengenezee mwanao future iliyo simama. We jiingize uone. ohooooo.
   
 9. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Ushampa tundi? kama bdo hiyo ndo gia ya kuombea,,afu anakula kona.
   
 10. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Yale yale, wale wale
   
 11. Enny

  Enny JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Mwambie wewe na mtoto awasomeshe kwanza hapahapa kabla hamjaenda
   
 12. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Wakina nani? toa ushauri
   
 13. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Anakudanganya..! Mwanaume halisi/mume mtarajiwa lazima akate mshiko ukiolewa unaweza kuwa na complains kama hizo but not now. Achana nae huyo. Huyu mwingine wa kibongo hebu kuwa open kwake chukulia kama yuko pekeyake mpe care stahiki then angalia kama bado una mfeel kama sio mpotezee. mind you umemuona na kasoro kibao sababu ya huyo wa USA. My opinion non of them is perfect, Kwenda US! :nono: ukirudi baada ya kuchemsha hata huyo mstd7 atakukacha kwa shule yako ni bahati kupata hako ka mshiko tunza hiyo DONT GOOO:A S angry:
   
 14. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Form 4 ... Amefanya kazi miaka 9... Analipwa Net 1,000,000/= : You must be very lucky!

  Achana na mapenzi, jiendelezi kelimu!
   
 15. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Jamaa anabeba maboksi USA. ......Halafu wewe unafanya kazi kisha bado unaomba omba pesa kwa mwanaume, halafu mkitoswa mlalamika!
   
 16. k

  kisukari JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2010
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,763
  Likes Received: 1,052
  Trophy Points: 280
  huwezi jua,pengine huyo wa usa ni member wa j.f.maana j.f kuna member kila kona.kuhusu mada yako,kama una uwezo wa kwenda usa ni bora ungeenda kimatembezi ili uone hali halisi ya maisha ya huko,maana maisha ya nje ya nchi nayo yanachosha.kwa kifupi sometimes mapenzi yanataka sacrifice kama mnapendana kwa dhati.
   
 17. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #17
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Swali zuri umejiuliza, kama anashindwa kukusaidia kitu kidogo huko marekani ataweza? tafakari na ufanye uamuzi sahihi.
   
 18. dazenp

  dazenp Senior Member

  #18
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 101
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Uamuzi upo juu yako......tunaweza kukushauri kesho ikawa ni vice versa, umefanya kazi kitambo....umekuwa mjanja kwakuwa umekaa kwenye kazi muda mrefu na sitaki kuamini ni mwanaume mmoja tuu aliyekutongoza....umeweza beba maksi kibao toka kwa watu tofauti ila naweza kukuambia first listen to your Heart then consult your head.....naamini hakuna ushauri mzuri kwenye mapenzi kama sio moyo wako na kichwa chako vikishauriana.....Mwanaume anayekujali atakupa hata kama ni shillingi 1000 ilimradi anajua kuwa unastahili kwakuwa wewe ni kipenzi chake sasa kama huyo....hakupi sijui kama anakujali ilaa.....isije ikawa ulimpenda kwakuwa yuo marekani na anaishi nchi za watu ukajua hapa nimepata mteremko maana nanyi nyie mwapenda mdondo....la kufanya kuwa muwazi na mueleze unalo hisi na kufikiria......unajua nashangaa ingekuwa mwanaume ameanza kukuliza na wewe upo nje ingekuwa so different scenario.....huwezi amini...
   
 19. ENZO

  ENZO JF-Expert Member

  #19
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,057
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  Kama u.s.a ya tandale kw tumbo kweli utakupeleka
   
 20. b

  bwanashamba Senior Member

  #20
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  acha tamaa dada kwa nini uyo mwanamke aliyezaa naye asimuoe,tafuta detail zake zaid
   
Loading...