Je, nabii Tito hana kosa?

Je, nabii Tito hana kosa?

Decree Holder

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2015
Posts
2,559
Reaction score
3,749
JE NABII TITO HANA KOSA?

Zawadi B. Lupelo

Nimeona maoni mbalimbali ya wanajamii forum wenzangu wakijaribu kuelezea mkasa wa Nabii Tito. Nimeguswa zaidi na maoni ya ndugu Bashir Yakub ambaye amezungumzia zaidi uhuru wa kuabudu chini ya ibara ya 19 ya katiba na uhuru wa maoni katika ibara ya 18, ameenda mbali zaidi na kutolea mfano kesi ya Hamis Rajab Dibagula V Republic.
Kwa mujibu wa Dibagula ambaye alikamatwa kwa kosa chini ya kifungu cha 129 cha Penal Code, kwa kosa la kuongea maneno ya kuudhi dhidi ya Imani nyingine. Dibagula (muislamu) katika mhadhara wa kiislamu alitamka maneno "YESU SIYO MWANA WA MUNGU..." ambayo yalitafsiriwa kama kukashifu dini ya kikristo. Mahakama ilisema Dibagula hana hatia kwani alichokuwa akikieleza ni kwa mujibu wa dini yake ya Kiislamu hivyo ana Uhuru wa kuabudu chini ya ibara ya 19 ya katiba na uhuru wa kujieleza chini ya Ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Mahakama ilikwenda mbali zaidi na kueleza kwamba si kazi ya mahakama kusema dini ipi ipo sahihi au yupi anaamini kilichosahihi bali kinachoangaliwa ni kwa kiasi gani mtuhumiwa ametoa maneno ya kashfa kwa dini nyingine au maneno ya kuudhi na hii haizuii mtuhumiwa kufundisha kile anachoamini kwenye dini yake kuwa ni kweli kwa mrengo wake.

Sasa hili la Nabii Tito limepokelewa kwa hisia tofauti sana hasa kutokana na mafundisho yake ya kuhamasisha unywaji wa pombe, kuoa wake wengi, kutembea na House girl nk. Je kosa lake lipo wapi? Anatofauti yoyote na Dibagula?

Sidhani kama kuna tatizo juu ya anachokiamini kama wanavyompinga baadhi ya watu. Imani yake ni haki yake. Si kweli kuwa anakashfu ukristo la hasha, tunachotakiwa tujiulize ni kwamba yupo hapo kihalali? Kwa maana kwamba amesajiliwa kama madhehebu mengine? Je amesajili kama mtu anayeamini nini?

Licha ya kuwa upo uhuru w kuabudu kwa mujibu wa Katiba lakini kama nchi tunao utaratibu ambao mtu anapohitaji kuanzisha dini aka dhehebu la dini anatakiwa kujisajili ili ijuliikane anaamini katika nini na iwapo Imani yake haikinzani na manufaa ya umma, naam nimesema "manufaa ya umma". Sidhani kama itakuwa ni busara kila mtu akaja na Imani yoyote anayotaka kuna watu watasema mimi Imani yangu inahimiza kula nyama za watu nayo isajiliwe kwa kuwa tu ni uhuru wa kuabudu si tutaliwa tutaisha? Mwingine aseme dini yake inasisitiza ubakaji, ushoga tutafika?. Ndiyo maana sheria imeweka utaratibu ukitaka kuanzisha dhehebu la dini lazima usajili ijulikane unaamini katika nini. Usajiliwe RITA chini ya sheria inayojulikana kama Trustees Incorporation Act Cap. 318. Lazima usajili bodi ya wadhamini ya taasisi yako ya dini ili kukiwa na kesi yoyote ya madai washitakiwe bodi ya wadhamini.

Kwa maoni yangu kama tu NABII TITO amesajiliwa na anachokifanya ndicho kilichopo kwenye usajili aliopewa basi hana kosa na tunaweza kutumia kesi ya Dibagula kama reference Mutatis Mutandis!!!!!!

Lupelo, Z.B
 
Kwa akili zake Huyo "NABII TITO" Sijuwi kama aliwai kukunbuka kusajiliwa. Zaidi anakumbuka kukata mauno na kunywa pombo. Duuh Dunia imekweisha.
 
Katiba hujaielewa,inaposema uhuru wa kuabudu ina maanisha vitu viwili tu
1.chagua dini yoyote kati ya zilizopo
2.anzisha ya kwako mwenyewe na ufanye lolote utakalo ila usikwaze wala kuhatarisha amani

Sasa huyo tito anakosea kutumia biblia na misalab ambavyo ni vya wakristo katika ujinga wake,kama angeanzisha dini yake akaiita titonity afu asitumie biblia then akafundisha chochote atakacho asingekamtwa
 
kwani anaposema kutafuna hausigeli anakosea...maana cjui kama kwenye vitabu vya dini nabii ibrahimu alimuoa hajiri (kijakaz) kwa ndoa...na pia issue ya pombe cjui kama ndo divai kwa mujibu wa tito mbona anatoa vifungu...tito apingwe kwa vifungu kama yeye anavyoongea kwa vifungu
 
kwani anaposema kutafuna hausigeli anakosea...maana cjui kama kwenye vitabu vya dini nabii ibrahimu alimuoa sara (kijakaz) kwa ndoa...na pia issue ya pombe cjui kama ndo divai kwa mujibu wa tito mbona anatoa vifungu...tito apingwe kwa vifungu kama yeye anavyoongea kwa vifungu
Mkuu ushasema mwenyewe ibrahimu "alimuoa "sara ,tito hajazungumzia ndoa kazungumzia uzinzi and then jina divai na pombe ni majina tofauti,yaani bado tito ana kesi tu
 
nataka andiko linaloonyesha alimuoa kwa ndoa...au alizaa naye tu....sorry i mean hajri kijakazi kutoka misri
 
Mkuu swala zito hili,,ngoja tu tusubiri kesi inaishaje ila nimesikia tito kajichana tumbo na wembe
 
Back
Top Bottom