Je Mwanasheria mkuu AG ni kipofu ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Mwanasheria mkuu AG ni kipofu ?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Mallaba, Dec 29, 2010.

 1. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  MSIMAMO wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kutaka isiandikwe katiba mpya badala yake iliyopo iwekewe viraka, umewakera wasomi, wanasiasa na wanaharakati ambao kwa nyakati tofauti jana walimtaka akae kimya kwa kuwa hana mamlaka ya kuwaamulia Watanzania mambo yao.

  Wakati wadau hao wakizungumzia suala hilo kwa uchungu, mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Chama Cha Mapinduzi (CCM) Peter Kisumo, amekitaka chama hicho kutoa tamko linaloonyesha msimamo wake kuhusu mjadala huo.

  Kisumo amesema CCM haipaswi kuogopa kuongoza mchakato wa mabadiliko ya Katiba kwa kuwa mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa yaliyotokea nchini tangu mwaka 1977, yanalazimisha kuwapo kwa Katiba mpya.

  Kisumo, aliitahadharisha CCM na kuitaka iitazame vizuri agenda ya mabadiliko ya Katiba vinginevyo itaonekana ni agenda ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kukipa umaarufu wa bure chama hicho.


  “Tusiogope suala la kuleta mabadiliko ya Katiba na mimi naitahadharisha CCM kama haitakuwa msitari wa mbele kuongoza agenda hii basi itaonekana ni agenda ya Chadema kama ilivyotokea katika suala la vita ya ufisadi,”alisema Kisumo.

  Mwanasiasa huyo ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa mabadiliko ya Katiba mwaka 1977, alifafanua kuwa mabadiliko ya katiba ya mwaka 1977 yalisukumwa na kuungana kwa vyama vya TANU na Afro Shiraz Party (ASP).

  “Sasa tangu wakati huo kumetokea mambo mengi ambayo yanaifanya Katiba yetu ionekane haikidhi haja…mathalani Katiba yetu bado inasema tunajenga nchi ya Kijamaa hivi ni ya kweli haya kwa hali ya sasa?”alihoji Kisumo.

  Kisumo alisema hata madaraka makubwa ya kikatiba ya Rais katika kuteua watu kuingia kwenye Utumishi wa Umma ikiwamo Ubunge, ni makubwa mno na kusisitiza kuwa suala la Wabunge wa kuteuliwa na Rais limepitwa na wakati.

  Mwanasiasa huyo aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikali ya awamu ya kwanza ya Hayati Jullius Nyerere, alisema ibara hiyo iliingizwa kuhofia uwezekakno wa Rais kukosa Wabunge wenye sifa ya kuunda Baraza la Mawaziri.

  Lakini badala yake alisema hivi sasa kuna mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu ambayo ifikapo mwaka 2015, Watanzania watakuwa wamesoma hadi kidato cha nne na wakati huo huo idadi ya wenye shahada itakuwa lukuki.

  “Majimbo yatapata Wabunge wasomi tu kwa sababu kiwango cha chini ya Elimu ya lazima itakuwa kidato cha nne ifikapo 2015 kwa hiyo hakuna sababu tena ya Rais kuteua watu maalumu kuwa Wabunge,”alisema Kisumo.

  Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba jana aligoma kujibu hoja hizo za Kisumo na kusema,"Mimi kwanza nipo katika gari, lakini pamoja na hayo mimi siwezi kuongelea suala hilo, hata kama ni kuziba viraka au kuundwa kwa katiba mpya, mimi siwezi kusema lolote bwana," alisema Makamba.

  Lakini mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kitengo cha Sayansi ya Siasa na Uongozi wa Umma, Bashiru Ally alisema mwanasheria mkuu hana mamlaka ya kusema iundwe au isiundwe katiba mpya.

  “Anachofanya Mwanasheria mkuu sasa ni kulinda matakwa ya serikali yake lakini hana haki kuzima mjadala wa Watanzania,” alisema Bashiru.

  Bashiru alifika mbali zaidi na kueleza kuwa, mwanasheria huyo wa serikali hana mamlaka ya kuzungumzia suala la katiba hasa ikizingatiwa kuwa ofisi yake, imeliingiza taifa katika hasara kubwa kutokana na kuingia mikataba mibovu.

  “Nadhani, tunayo mifano mingi halisi inayoonyesha utendaji mbovu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu. Imekuwa ikisaini mikataba mibovu inayolisababishia taifa hasara na pia imekuwa ikipisha miswada mbalibali mibovu. Kwa hiyo, lazima msimamo wake utazamwe kuwa ni wa msingi sana,” alisema Bashiru.

  Kwa mujibu wa Bashiru siyo sawa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kusema katiba inahitaji viraka badala yake anatakiwa kutekeleza matakwa ya Watanzania ambao ndio waajiri wake.

  Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Agenda Participation 2000 Moses Kulaba, alisema kauli ya Jaji Werema, ni kichekesho.

  “Mahitaji ya katiba mpya ni makubwa, kauli zake za kufananisha Tanzania na India kwa kweli zimepitwa na wakati. Sasa Tanzania inahitaji Katiba mpya,” alisema Kulaba.

  Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema Erasto Tumbo alisema kitendo cha mwanasheria mkuu wa Serikali Frederick Werema kukataa mabadiliko ya katiba, kimetokana na uroho wa madaraka.

  Alisema kisheria katiba ni ya watanzania na yeye ni mshauri wa serikali juu ya mambo yahusuyo sheria na Mjumbe wa Baraza la Mawaziri asiye na kura hivyo hana sifa za kuzungumiza katiba mpya.

  “Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 Ibara ya 54 kifungu kidogo cha 4 yeye ni mshauri wa serikali juu ya mambo yahusuyo sheria na pia ni mjumbe wa baraza la mawaziri asiye na kura, sasa anapopinga mabadiliko ya katiba, anazungumza kama nani?" alihoji Tumbo na kuendelea “yeye anatakiwa akae kimya, awaache watanzania waendelea na madai yao.
  Habari hii imeandaliwa na Fidelis Butahe, Hussein Issa, Raymond Kaminyoge, Fredy Azzah na Daniel Mjema
   
 2. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  Tayari tumemuelewa uwezo wake kiutendaji,yawezekana anvyo vyeti vizuri na kashika nafasi nyingi kwa njia ya upendeleo hivyo kupewa nafasi hiyo nyeti inatuwezesha kumjua zaidi he is currently more exposed than b4
   
 3. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  unalosema ni kweli kabisa, unajua hivi vyeo vya kuteuliwa siku zote vinakuwepo kuwafurahisha waliokupa, hicho ndio tunachokiona hapa.Hivi vyeo vyote vilitakiwa kuwa elected and not just appointment based on friendship
   
Loading...