Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,091
Tumeshazoea kila ikifika msimu wa sikukuu za kidini, basi hutoka nyaraka kutoka kwa taasisi mbalimbali za kidini ambazo huwa na lengo la kuionya jamii na kushauri mambo ambayo yatadumisha amani na upendo nchini.
Naamini utamaduni huu mzuri bado unaendelea na pengine tunahitaji zaidi nyaraka hizi hasa katika kipindi hiki ambacho nchi yetu inapitia katika hali mbaya ya kiuchumi na wasiwasi mkubwa.
Mwaka jana, ulitoka waraka kutoka kwa KKKT ambao kidogo ulileta mtafaruku baina ya Serikali na taasisi hiyo ambapo ilifikia hatua Serikali kuagiza Kanisa hilo kufuta waraka wao kwa madai ya uchochezi.
Sasa, tumeingia mwaka 2019 na leo ni Sikukuu ya Pasaka.. Sijasikia waraka wowote mpaka wakati huu..
Naomba kama upo tuuwasilishe humu ili tuendelee kujitazama na kujiponya kiroho na kijamii!
Heri ya Pasaka!