Je Mungu anaweza kuwa Mungu; Je mtu anaweza kuwa Mungu?

Je Mungu anaweza kuwa Mungu; Je mtu anaweza kuwa Mungu?

Jagina

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2019
Posts
11,505
Reaction score
5,378

A: JIBU LA KILOGIC (MANTIKI)​

Je, Mungu anaweza kuwa mtu?​

Ndiyo au Hapana hutegemea ufafanuzi wa “Mungu”.

Ikiwa Mungu ni:​

1. Asiyekuwa na mwanzo wala mwisho
2. Asiyepungukiwa na chochote
3. Asiyefungwa na muda, nafasi, njaa, usingizi, maumivu, au kifo

Basi kwa logic safi:

Mungu hawezi kuwa mtu bila kubadilika asili yake . Kwa sababu:
1, Mtu hukua, hula, huchoka, huumia, hufa
2. Mungu hawezi kupoteza sifa zake bila kuacha kuwa Mungu

Hii ndiyo hoja kuu ya Uislam.

B. Je, mtu anaweza kuwa Mungu?​

Kwa logic:

1. Kiumbe aliyeumbwa hawezi kuwa Muumba
2. Kilicho na mipaka hakiwezi kuwa kisicho na mipaka
3. Aliyewahi kutokuwepo hawezi kuwa wa milele

Kwa logic pekee:

Mtu hawezi kuwa Mungu
. Hili linakubaliwa hata na wanafalsafa wasiokuwa wa dini.

C. JIBU LA KIBIBLIA​

Biblia ina mistari miwili inayovutana.

1. Biblia inasema Mungu si mtu

Hesabu 23:19 “Mungu si mtu hata aseme uongo, wala si mwanadamu hata ajute.”

1 Samweli 15:29“Yeye si mwanadamu hata abadilishe nia.”

Hosea 11:9 “Kwa maana mimi ni Mungu, wala si mwanadamu.”

Hizi ni kauli za wazi: Mungu si mtu

Lakini Biblia pia inasema “Neno lilikuwa Mungu” na “likawa mwili”​

Yohana 1:1,14 “Hapo mwanzo kulikuwapo Neno… Neno alikuwa Mungu… Neno akawa mwili.”

Hapa ndipo teolojia ya Utatu ilipojengwa:

1. Mungu alichukua asili ya kibinadamu
2. Bila kuacha kuwa Mungu

Tatizo la logic:

1. Mungu asiye na mipaka anawekewa mipaka
2. Asiyeweza kufa --- anakufa
3. Asiyejua yote --- anauliza maswali

Hii inaleta mgongano wa mantiki, ndiyo maana hata: Wayahudi na Wakristo wa mwanzo (Ebionites, Arians)
waliikataa.

Ndani ya Biblia yenyewe kuna mvutano wa kimantiki.

D. JIBU LA QURʾĀN​

Qurʾān 112:3 “Hakuzaa wala hakuzaliwa.”

Qurʾān 6:103 “Macho hayamfiki, naye hufikia macho yote.”

Qurʾān 42:11 “Hakuna chochote mfano Wake.”

Qurʾān 5:75 “Masihi mwana wa Mariamu si chochote ila ni Mtume… walikuwa wakila chakula.”

Hoja ya Qurʾān ni ya kimantiki kabisa:
1.Kula ni mahitaji
2.Mahitaji ni upungufu
3. Upungufu si Uungu

E: KWA NINI UISLAM UNAKATAA “MUNGU KUWA MTU”?​

Kwa sababu:

Inavunja Umoja kamili wa Mungu
  1. Inamfanya Mungu:
  2. azaliwe
  3. ateseke
  4. auawe
  5. Inamfanya Mungu ategemee viumbe
Qurʾān inalinda dhana ya Mungu alie juu, mkamilifu, na asiyehitaji.

F. JE, MUNGU HAWEZI KABISA KUWA MTU?​

Tofauti ya msimamo:

Uislam: Haiwezekani kiasili

Ukristo: Inawezekana kwa fumbo (mystery), si kwa logic

Falsafa: Mungu habadiliki wala hawezi kuwa mtu

Kauli ya Kimantikini ni kuwa Mungu akigeuka mtu, basi anakuwa si Mungu tena .

Mungu ni dhana tu hivyo dhana iyo inaweza kuvikwa uhusika wowote tu kati ya jamii na jamii kulingana na mapokeo yao.

Anaweza kuwa mawazo tu au fikra isiyoshikika .

Anaweza kuwa mfano wa mtu maarufu aliyepita miaka na miaka

Anaweza kuwa jua , wanyama kama ng'ombe simba na masanamu ya kutengeneza, mapango miti na milima mikubwa.
 
Mungu ni dhana tu hivyo dhana iyo inaweza kuvikwa uhusika wowote tu kati ya jamii na jamii kulingana na mapokeo yao.

Kauli: “Mungu ni dhana tu ya jamii” ina matatizo makubwa.

Kwa logic , Kama Mungu ni dhana tu:​

1. Hakuna Mungu wa kweli
2. Hakuna ufunuo, ukweli wa juu, wala maadili ya kudumu

Lakini dini (Ukristo na Uislamu) zinadai: Mungu alizungumza , Aliongoza historia kwa hivyo Huwezi kusema ni dhana tu halafu useme alinena kweli.

Kibiblia , Mungu hajitambulishi kama wazo la jamii bali kama aliye hai na huru:​

“Mimi ndimi niliye” (Kutoka 3:14)​

Manabii waliupinga utamaduni wa jamii zao, hivyo Mungu si zao la mapokeo.

Kwa Qurʾān “Yeye ni Allah, Mmoja” (112:1)​

Ukweli hauamuliwi na jamii wala mapokeo (6:116).

Ungejibu tu kawaida bwashee , mambo ya mimi kujadiliana na akili mnemba ni uonevu na dharau bwashee
 
Ungejibu tu kawaida bwashee , mambo ya mimi kujadiliana na akili mnemba ni uonevu na dharau bwashee
Sikukudharau wala kukuonea.
Nilijibu hoja, si wewe kama mchangiaji

Ukisema “Mungu ni dhana tu ya jamii” halafu ukaamini Mungu ananena na kuongoza, hapo kuna kujipinganisha kifikra — kusema hilo si dharau, ni kujibu hoja kikawaida.
 
Ukianza kuleta uislam hapo ndipo unapofanya hoja yako iwe haina mantiki, bora usingerelea quran ungeeleweka kidogo. Kumbe unapepelea uislam! Kwenye biblia kuna mistari inashadidia uungu wa Yesu we umeipotezea ukidhani unawaandikia watu wasiosoma biblia
 
Mungu wa Akili Mnemba.

Mungu wa mchongo.

Mungu wa kutetewa na Artificial intelligence(AI).

Mungu wa Chatgpt.

Mungu bubu.

Mungu asiyeweza kujitetea mwenyewe.

Mungu mdhaifu, mchovu na goigoi.
 
Sikuleta Uislam kuthibitisha Biblia, bali kulinganisha hoja.

Ukisema “Biblia inamthibitisha Yesu kuwa Mungu” hiyo ni tafsiri ya kitheolojia, si kauli isiyopingika.

Ndiyo, kuna mistari inayotafsiriwa kuunga mkono uungu wa Yesu, lakini pia Biblia ina mistari wazi inayosema:

Mungu si mtu , Yesu anamwomba Mungu pia Mungu ni mmoja, aliye juu ya wote

Kwa hiyo kusema kuna mvutano wa maandiko si kudharau Biblia, ni uchambuzi wa maandishi yenyewe.

Kukubaliana au kukataa ni haki ya kila mtu lakini kutofautiana kwa tafsiri si sawa na kusema mtu hajui Biblia.
 
Ulimwengu uliumbwa na Mungu na viumbe vyote vilivyomo.

Solar system ,Digestion system inaonyesha kwamba kazi zilifanyika ,m/ke na m/me kushenyetana na kutoa kiumbe ni High Tek ambayo hakuna binadamu anayeweza.
 
Mungu wa Akili Mnemba.

Mungu wa mchongo.

Mungu wa kutetewa na Artificial intelligence(AI).

Mungu wa Chatgpt.

Mungu bubu.

Mungu asiyeweza kujitetea mwenyewe.

Mungu mdhaifu, mchovu na goigoi.
Naunga mkono hoja
 
Mungu ni dhana tu hivyo dhana iyo inaweza kuvikwa uhusika wowote tu kati ya jamii na jamii kulingana na mapokeo yao.

Anaweza kuwa mawazo tu au fikra isiyoshikika .

Anaweza kuwa mfano wa mtu maarufu aliyepita miaka na miaka

Anaweza kuwa jua , wanyama kama ng'ombe simba na masanamu ya kutengeneza, mapango miti na milima mikubwa.
Hata ng'ombe ni Mungu kwa wahindu,lakini hapa inajadiliwa Mungu muumba,muweza wa kila kitu na si kitu chochote kiitwacho Mungu
 
Mungu wa Akili Mnemba.

Mungu wa mchongo.

Mungu wa kutetewa na Artificial intelligence(AI).

Mungu wa Chatgpt.

Mungu bubu.

Mungu asiyeweza kujitetea mwenyewe.

Mungu mdhaifu, mchovu na goigoi.

Hiyo si hoja, bali ni kejeli.

Kumkosoa Mungu kwa kumtukana hakuthibitishi kuwa hayupo, wala hakubatilishi hoja za wanaoamini.

Mawazo, hoja, na maandiko hutetewa na akili za binadamu, si kwa sababu Mungu ni dhaifu, bali kwa sababu ndivyo mjadala wa kibinadamu unavyofanyika.
Kumtukana Mungu ni hisia, si hoja.
 
Kama Mungu hayupo Ulimwengu ulitokeaje? yaani chanzo wala usiniambie mambo ya Big Bang kwani hiyo Big Bang ilistart vipi? ,kama Mungu hayupo Binadamu alitokeaje? Kwanini viumbe vipo vya Ke na Me ni nani aliyebuni kwamba kuwe na Me na ke kwa ajili ya kuzaliana?
 
Hili swali ukijibu ni Mungu kafanya itakulazimu formula hiyohiyo uliyotumia kuuliza hili swali , ujiulize na kuhusu aliye mfanya Mungu awepo pia , tofauti na hivyo ni ( first cause paradox )
 
Mungu ni product ya mtu

Ndio maana ana jinsia (Me) na ukitaka kubisha, jaribu kuangalia watu waliowahi kumuita Mungu ni mwanamke utaona jinsi jamii ilivyo react.

Mungu ana mapungufu vitu kama emotions vinamtatiza pia.

Tumeona kwenye vitabu vya dini vikionesha mara kadhaa masononeko ya Mungu kwenye baadhi ya mambo ambayo hafurahishwi nayo.
Screenshot_20260214-164203_Chrome.jpg

Kwa hiyo wewe unayekumbana na stress za kimaisha na kufikiri njia sahihi ya ku overcome hiyo situation ni kufanya maombi Mungu akupe tulizo la nafsi.

Jua kabisa stress ni tatizo kubwa hata Mungu wako hajaweza kupata ufumbuzi wa hii changamoto.
 
Mungu ni product ya mtu

Ndio maana ana jinsia (Me) na ukitaka kubisha, jaribu kuangalia watu waliowahi kumuita Mungu ni mwanamke utaona jinsi jamii ilivyo react.

Mungu ana mapungufu vitu kama emotions vinamtatiza pia.

Tumeona kwenye vitabu vya dini vikionesha mara kadhaa masononeko ya Mungu kwenye baadhi ya mambo ambayo hafurahishwi nayo.
View attachment 3543757

Na wivu pia
 
DUh
 
Kama Mungu hayupo Ulimwengu ulitokeaje? yaani chanzo wala usiniambie mambo ya Big Bang kwani hiyo Big Bang ilistart vipi? ,kama Mungu hayupo Binadamu alitokeaje? Kwanini viumbe vipo vya Ke na Me ni nani aliyebuni kwamba kuwe na Me na ke kwa ajili ya kuzaliana?
Swali ni je, Kila kilichopo lazima kiwe na chanzo?

Kama jibu ni ndiyo basi hili swali litakuwa na mantiki ikiwa huko mbeleni hautoweka mipaka.

Isifike mahali lipatikane jibu kuwa kuna kitu ambacho chenyewe ndio kisababishi cha vitu vyote halafu hicho kitu hakina chanzo.

Hapo utakuwa umeharibu msingi wa saali na kulazimisha majibu ambayo hayaheshimu sheria na kanuni ya upatikanaji wa jibu.

So kwa kifupi itakuwa ni swali ambalo linakuleta kwenye majibu ambayo ni infinite.

Lakini pia hata ukajibu hapana kwenye lile swali kwamba si lazima kilichopo kiwe na chanzo, basi kumbe tunaweza kusema hata ulimwengu pia upo na hauna chanzo kwasababu si lazima kilichopo kiwe na chanzo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom