Je msomi ni yupi ?

Je msomi ni yupi ?

HASSAN MOLLEL

Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
9
Reaction score
3
Ndugu zangu wangu jf napenda kushare nanyi hiyo mada hapo juu.

Watu wengi wanasema mtu mpaka aitwe msomi ni mpaka apate kazi ya kisomi chake wengine na wanasema mpaka apate shahada ya kwanza ndo uuitwe msomi!

Ikawa haya majibu yananichanganya ipi sahihi kwa sababu watu ambao hawajasoma wanapenda sana kuwadharau watu waliosoma kutokana haliyao ya kimaisha.

Ahsanteni sana!
 
Msomi ni mtu aliyeelimika na kufanya mambo yake tofauti na asiesoma. Kuna kusoma na kuelimika. Ni tofauti. Kama msomi akisikia maneno hayo na kuumia kwa kudharauliwa na asiesoma. Huyo hajaelimika na hafai kuitwa msomi. Nawasilisha
 
Msomi ni yule anayeweza kusoma maandishi na kuandika out of that kuna 'kujifunza' na 'kuelimika'
 
Kwanza unaweza kusoma na usielimike. Na unaweza kuelimika bila kusoma. Vipi mtu unakuwa na rundo la vyeti then unakuwa siyo mchapakazi? Mimi kwangu msomi fqla tu kama c mchapakazi
 
Msomi si lazima apate kazi ya kisomi ya taaluma yake.
Kuna Dalala moja kama sikosei ya mwenge,kuna Jamaa ana Degree moja anapiga utingo.
 
Kupata kazi baada ya kusoma sio usomi. Ukisoma na ukiwa muelewa wa mambo mbalimbali na mengineyo aliyosema mchangiaji wa kwanza ndio msomi>

Ni mtazamo tu.
 
Msomi ni mtu aliyesoma na kuelimika kwenye vyuo vya elimu ya juu na kuzishika nguzo kuu tatu za elimu nazo ni ufahamu wa jambo alilosomea, ujuzi/uhodari pamoja na tabia. Pia awepo na uwezo wa kufikiri na kujenga hoja/kufikia lengo bila kushurutishwa na asimamie misingi ya ukweli/takwimu.
 
Back
Top Bottom