mcfm40
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,452
- 3,151
Ni hivi. Katika mkutano wa bunge la February, 2017, wabunge walitoka wakiwa kitu kimoja, wote CCM na Ukawa, kiasi cha hata kuachiana muda wa kuchangia hoja bungeni.
Kuna mambo yaliyotokea hasa la Makonda ambayo yalifanya bunge zima kuongea kwa sauti moja dhidi ya serikali.
Ilionekana kwamba kama bunge hili la bajeti lingeanza na moto ule ule basi serikali ya Magu ingekuwa katika wakati mgumu sana. Wabunge wote CCM na upinzani walipanga kuichachafya hii serikali kweli kweli.
Ili kipunguza huo umoja ulioanza kujijenga baina ya wabunge katika kuikosoa serikali, ndipo mastrategist wa CCM na serikali wakahakikisha wanafufua bifu kati ya Wabunge wa Cccm na vyama vya upinzani. Lengo ni kuhakikisha wabunge wa ccm watasimama kuitetea serikali dhidi ya hoja za upinzani. Na lengo pia ni kuwakumbusha wabunge wa ccm kuwa mpinzani na adui yao ni Ukawa hasa chadema na sio serikali. Na hivyo hawapaswi kuungana na upinzani dhidi ya serikali. Hili linaonekana kufanikiwa ukiangalia jinsi kikao cha jana kilivyokwenda na jinsi wabunge wa Ccm walivyowafanyia undava wabunge wa chadema.
Kwa hiyo tutegemee mivutano baina ya ccm na upinzani ikitawala katika bunge hili la bajeti huku hoja zenye mwelekeo wa kuwaunganisha wabunge dhidi ya serikali zikipewa nafasi ndogo kabisa!
In fact, hata kuteuliwa kwa Kitila huko serikalini ni katika harakati za kupunguza mashambulizi yaliyokuwa dhahiri yanakwenda kuitikisa serikali. Watu kama kina Zitto weshalainika tayari.
Nina hakika si wabunge wa chadema wala ccm waligundua kuwa wanakuwa manipulated kwa malengo maalum.
Maelekezo waliyopewa wabunge wa Ccm kuwakataa wabunge wa EALA wa chadema lilikuwa na lengo tu la kuamsha bifu na hasira baina ya upinzani na wabunge wa Ccm ili isitokee tena wazungumze lugha moja dhidi ya serikali!
Hivyo tutegemee "business as usual" katika bunge hili la bajeti! Ndiooo... kwa kila pendekezo la serikali!
Ni hayo tu! Hii nchi ngumu sana!