Je, mitaala ya elimu yetu inaendana na kasi ya ajira ya dunia ya leo?

code4494

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
798
1,204
Nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya 2000 nikiwa nimemaliza darasa la saba nilipangiwa katika moja ya shule kongwe za sekondari (bweni) hapa nchini iliyopo mkoani Kilimanjaro, ilikuwa ni boys tupu.

Kutokana na shule ilikuwa ni ya serikali, ilikuwa inachukuwa wanafunzi kutoka mikoa mbalimbali.

Nakumbuka kipindi nipo kidato cha kwanza, alfajiri wakati tunajiandaa kabla ya kuingia madarasani ilikuwa ni kawaida kumuona mwanafunzi wa kidato cha nne au cha tano na sita kukwangua kidevu kilichojaa ndevu, kwa kifupi tulikuwa tunasoma na vijeba, yaani mwanafunzi wa kidato cha sita kuwa na miaka 28 ilikuwa ni kawaida sana na kulikuwa na sheria ya kunyoa ndevu. Nakumbuka Head Prefect alikuwa mtu mzima kabisa na alikotoka alikuwa na familia.

Lakini kadiri miaka ilivyokwenda vijeba walikuwa wanapungua hadi leo hii unakuta mwanafunzi wa chuo hata ndevu hajaanza kuota.

Sasa cha kujiuliza ni kipi kimetokea Hadi Hali imekuwa tofauti hivi?

Zipo sababu mbalimbali zilizochangia mabadiliko hayo kama kuongezeka kwa shule, sera ya serikali, kupungua kwa soko la ajira, kukua kwa teknolojia. Zipo sababu nyingi lakini sababu nyingine ya msingi ni kuongezeka kwa uelewa.
Uelewa wa Mtanzania wa leo ni tofauti na wa miaka ya 70.

Mtoto wa darasa la kwanza wa leo anauelewa mkubwa kuliko mtoto wa darasa la kwanza wa miaka ya zamani.
Hvyo basi, kulingana na mabadiliko hayo pia hata mitaala yetu ilipaswa iboreshwe zaidi iendane na nyakati hizi

Hvyo basi, badala ya mwanafunzi kusoma darasa la kwanza mpaka la saba, halafu kidato cha kwanza mpaka sita, kwa mtazamo wangu mwanafunzi angesoma darasa la kwanza mpaka la tano, la sita na la saba engesoma vitendo zaidi, sekondari asome kidato cha kwanza mpaka cha nne, kidato cha tano na sita iwe ni vitendo.

Hii ingemsaidia chuoni kuchagua fani ambayo angebobea kwa hali ya juu maana misingi aliyopitia imemjenga kwenye kuelewa zaidi kuliko kukariri.
 
Back
Top Bottom