Je, michango na maamuzi ya wabunge Bungeni yanahakisi michango na maamuzi ya wananchi walio wengi?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,608
6,820
Je, maamuzi yanayoshangiliwa Bungeni na wabunge walio wengi yanashangiliwa pia kwa asilimia kubwa kwa uzito ule ule na watu wanaowawakilisha kwenye majimbo yao ya uchaguzi? Wabunge kwenye swali hili ni wale waliochaguliwa tu na wananchi kwa sababu hao wa aina nyingine sijui wanamwakilisha nani na kwa sababu zipi za kidemokrasia ya uwakikilishi.

Tuchukulie mfano wa michango na maamuzi ya kuamishia tozo ya usajiri wa magari ya kila mwaka kwenye nishati inayoendesha magari hapa nchini kuanzia mwaka wa fedha 2017/ 2018. Ile shangwe na nderemo Bungeni baada ya maamuzi hayo kufikiwa, imeonekana pia kwa wapiga kura walio wengi?

Tunahitaji empirical investigations based on robust theoretical frameworks kupata majibu ya swali hili.
 
Hao wabunge wa CCM jukumu pekee wanalolijua wao humo Bungeni ni kuikingia kifua serikali ya CCM na kuimba nyimbo waliyoizoea ya NDIYOOO........ na kutoa adhabu za kuwakomoa wabunge wa upinzani kwa kuwafungia kutoingia Bungeni kwa vipindi virefu sana ambapo adhabu hizo hata kwenye kanuni za Bunge lao hazimo!
 
Back
Top Bottom