Je, majina ya vituo vya basi yanatambulika kisheria?

Je, majina ya vituo vya basi yanatambulika kisheria?

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,923
Reaction score
7,169
Amani ya Bwana iwe nanyi.

Katika muendelezo wa mada zangu za kichochezi, leo naenda kwa wale kina sisi tunaopanda gari kupitia dirishani.

Ukiacha vituo vya mwanzo na mwisho wa trip na ukiacha vituo vya mwendokasi, ni wapi kisheria majina ya vituo yanatambulika?

Hypothetical question: Mfano mtu amepitishwa kituo chake halafu labda akapata shida au usumbufu fulani mfano mgonjwa aliyekuwa anamuwahishia dawa akafariki, halafu yule abiria akaamua kuwashitaki wahusika wa lile basi. Wakiwa mbele ya Pilato, dereva na utingo wake pamoja na bosi wao wakiwakilishwa na Wakili Kibatala katika utetezi wao wakahoji hiko kituo cha basi kinachoongelewa kinatambulika wapi?

Pilato akaamuru watupwe ndani ya defender hadi katika hiko 'kituo' husika. Ukienda katika kituo, hakuna kibao chenye jina la kituo. Hakuna kibao kinachoonyesha kwamba ni kituo cha basi. Sheria za usalama barabarani zinaongozwa sana na alama za barabarani na ndiyo zinatumika kama point of reference wakati wa kutoa adhabu. Hapa naona kuna mapungufu.

Nawakilisha.
 
Back
Top Bottom