Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,220
JE MACHO YAKO YANAONA FURSA KAMA YANAVYOONA MAKOSA YA WATU WENGINE?
Kama ungeweza kuziona fursa haraka kama unavyoyaona makosa ya wengine, basi ungekuwa mbali sana.Kama ungekuwa unachukua hatua haraka kama unavyochukua kuwakosoa wengine, maisha yako yangekuwa bora sana.
Lakini hufanyi hivyo, kwasababu labda hujajua jinsi ya kufanya na nitakushirikisha hapa.
URAHISI WA KUONA MAKOSA YA WENGINE
Ni rahisi sana kuona makosa ya wengine. Hii ni kwasababu kwa tulivyozoea, tunaona mabaya haraka sana. Hii ni kwasababu tunayatafuta mabaya hayo na kwasababu unachotafuta utakipata, basi huwa tunayapata kiurahisi sana makosa ya wengine.
Kama unataka kuziona fursa iwe rahisi kama unavyoyaona makosa ya wengine, basi anza kutafuta fursa kila mahali. Kila unachofanya, kila unapokuwa, kila mazungumzo unayofanya, jiulize ni fursa gani iko hapa ambayo bado sijaiona. Jiulize ukiwa bado eneo hilo hilo.Kwa kujiuliza swali hilo mara kwa mara kutakusukuma wewe ufikiri zaidi na utaanza kuziona fursa kila utakapokuwepo.
URAHISI WA KUWAKOSOA WENGINE
Ni rahisi sana kukosoa watu wengine kwa sababu ni rahisi. Haihitaji utumie nguvu za ziada katika kukosoa, na hata unapokosoa sio wewe ambaye una mzigo mzito wa kufanyia marekebisho. Na hata hivyo huenda hujui ugumu aliokutana nao mtu mpaka hapo alipopita. Hivyo ni rahisi sana kusema, hapo singefanya hivyo, angefanya hivi.
Unaweza kuitumia hii kuweza kuchukua hatua kwenye zile fursa unazoziona. Kwenye kila fursa unayoiona ambayo inaendana na wewe, jiulize ni sehemu gani rahisi ambayo unaweza kuanzia kuchukua hatua. Tafuta sehemu rahisi sana au kitu kidogo sana unachoweza kuanza kufanyia kazi na anza mara moja.
Unaweza kuwa umepanga kufanya makubwa sana.
Sasa yagawe kwenye visehemu vidogo vidogo sana ambavyo vitaonekana rahisi kufanya na anza kuvifanya mara moja.Kuwa makini kuziona fursa kama unavyoyaona makosa ya wengine kirahisi na chukua hatua ya kuzifanyia kazi fursa hizo haraka kama unavyoweza kumkosoa mtu haraka.