Wakati nikijifunza zaidi kuhusu Ndoa Za mitala katika dini na imani mbali mbali kupitia mtandao wa wikipedia, nimegundua kuwa katika Ukristo walutherani wanaruhusiwa kuoa wake wengi.
Luther alimruhusu bwana Philip wa Hesse aliyekuwa anapenda sana wanawake kuoa mke mwingine kwa siri ili kusiwe na kashfa hadharani. Hata hivyo miaka 15 baadae Luther alisema kuwa alimruhusu Philip aoe mke wa pili kwa sababu tendo hilo halikuyapinga maandiko.
Karibuni wakristu wenzangu hasa walutheri tupiganie haki yetu. Je mnalijua hili?
Kwa upande wa wakatoliki, Roma (kabla ya ukristu) ilikataza ndoa za mitala na kuwa ni kosa kisheria. Baadae kanisa liliendeleza mfumo huo. Hata baadhi ya wayahudi katika kipindi cha kutawaliwa na warumi walilazimishwa kuwa na mke mmoja tu.
Kwa mujibu wa wikipedia na kuna fungu kadhaa za Biblia zimewekwa madhehebu mengi ya Kikristu isipokuwa Katoliki tuu wanaruhusu mitala.